Kafulila: CAG amekwepa jukumu lake kwa kushindwa kuweka msingi wa zilipo sh 1.5 trilioni

Kupitia kipindi cha Clouds 360 Kafulila akihojiwa kwa njia ya simu amesema CAG alipaswa kusema ni wapi alipoona upungufu wa hizo sh 1.5 tril.

Kafulila anasema CAG ameamua au kudanganya ama kuwachanganya wananchi kwa kusema tu kuwa hizo fedha zilikusanywa halafu hazijulikani zilipo huu ni upuuzi.

CAG alitakiwa aende mbali kuelezea ni wapi fedha hizo zimepotelea na kamwe hilo siyo jukumu la bunge.

Chanzo: Clouds tv!
Waliohama chadema kwa sababu ya kumuunga mkono utendaji wa rais, sasa midomo wazi hawajui pa kwenda. Kinachoendelea kinanikumbusha msemo wa kiingeraza unaosema" he laughs better he who laughs last".
 
Tanzania ina takribani vijiji 16,000 nchi nzima. Nakumbuka wakati wa kampeni rais Magufuli aliahidi kugawa milioni 50 kwa kila kijiji, baada ya miaka miwili madarakani alikuja kukaririwa akisema serikali haina pesa za kugawa bure.

Hizi pesa zaidi ya trn 1.5 zilizopotea yaani matumizi yake hayajulikani serikali ingeweza kugawa million 100 kwa kila kijiji.

Kupanga ni kuchagua lkn wao wamechagua kuziweka kwenye mifuko ya watu binafisi halafu wanajiita ni wazalendo wanaopambana na ufisadi.
Msiojua uchumi mnakuwa na matatizo sana. Pesa haigawiwi bali hupokelewa kama malipo, mtaji, faida au transfer income kutokana na shughuli iliyofanyika, itakayofanyika au maandalizi ya kufanyika shughuli fulani.
 
Kupitia kipindi cha Clouds 360 Kafulila akihojiwa kwa njia ya simu amesema CAG alipaswa kusema ni wapi alipoona upungufu wa hizo sh 1.5 tril.

Kafulila anasema CAG ameamua au kudanganya ama kuwachanganya wananchi kwa kusema tu kuwa hizo fedha zilikusanywa halafu hazijulikani zilipo huu ni upuuzi.

CAG alitakiwa aende mbali kuelezea ni wapi fedha hizo zimepotelea na kamwe hilo siyo jukumu la bunge.

Chanzo: Clouds tv!

Hahaa yule mtu mahiri wa zamani kawa kituko cha mwaka. Kazi CAG nikukagua matumizi ya serikali. Alichokiona ni kwamba 1.5 trillion hazionekani zimetumika wapi. Na accounting officers walitakiwa waeleze ndani ya siku 21 . Hawa kuweza kutoa majibu. Sasa unaposema CAG aeleze hela hizo zipo wp sio kazi yake n hajui. Kafulila acha njaaa
 
HAWA MAODITA WANANISHANGAZA. MFANO WANAKUTA GARI LIMENUNULIWA WANALIONA ILA HAJAONA DELIVERY NOTE AU RISITI TU. HUNDI ILIYOLIPIWA LABDA NAYO WAMEIONAA NA KWENYE LEJA IMEWEKWA SASA UNAJUA WATARPOTI KWA NI HASARA KWA SERIKALI!!! HAYO TU NDIO MUELEWE HIYO 1.5 TR YAWEZA KUWA NYINGI NI KTK KUNDI HILI INGEBIDI WAWEKE BAYANA NI NINI KIMEKOSEKANA .
Mtahangaika sana, kama receipt haionekani wakaguzi watahoji hadi itakapopatikana ushahidi wa kiasi kilicholipwa. Receipt ikiwepo, mali imeingizwa kwenye leja husika, hakuna mkaguzi atakaye leta hoja ya ukaguzi ya kipuuzi kiasi hicho. Ukiona hoja nzito kama ya kuhoji iliko Trillioni 1.5 ujue hakuna majibu ya maana yametolewa. Na kwa bahati nzuri CAG huwezi kumuachicha kazi kirahisi kama ambavyo imekuwa ikifanyika. Mtu mwenyewe, mbobezi katika uhasibu na ukaguzi na kubwa zaidi mcha Mungu. Hili mnalo na ndivyo Richmond ilivyoanza. Mhe. Lowasa akatishia watu, akatoa maelezo, wapambe wakajifunga vibwebwe, hatimaye ikathibitika, akajiuzulu. Hili mnalo.
 
Sasa CAG kasema pesa imepotea,afu kafulila anauliza imepotelea wapi,kwan nin maana ya neno kupotea??....sijawahi ona bongo finyu kama za wanasiasa,ni bora kukaa kimya tu
 
Huyu kafulia anaongea nini? CAG kafanya ukaguzi kakuta kuna pesa hizo hazijulikani ziko wapi, kawapa muda wahusika wampe majibu wameshindwa. Unafikiri hatua gani zaidi CAG anaweza kuchukua? Hapo imebaki kazi ya bunge kuihoji serikali.
 
Huyu jamaa hana tofauti na NABII TITO.
Kupitia kipindi cha Clouds 360 Kafulila akihojiwa kwa njia ya simu amesema CAG alipaswa kusema ni wapi alipoona upungufu wa hizo sh 1.5 tril.

Kafulila anasema CAG ameamua au kudanganya ama kuwachanganya wananchi kwa kusema tu kuwa hizo fedha zilikusanywa halafu hazijulikani zilipo huu ni upuuzi.

CAG alitakiwa aende mbali kuelezea ni wapi fedha hizo zimepotelea na kamwe hilo siyo jukumu la bunge.

Chanzo: Clouds tv!
 
Billion 7 zilizoliwa na chadema kwa kununua helkopita hewa ni sawa na bajeti nzima ya wizara ya maji na chenji inabaki
Chadema siyo chama tawala, in sawa wewe kumpangia MTU matumizi ya pesa ambayo hujui alikopata, huo ni uzwazwa
 
Uwezo wa Kafulila kufikiri umepungua mno na kama anachoongea anakiamini basi anakaribia kupata ugonjwa wa akili
 
Back
Top Bottom