Kafulila afunguka tena, sasa aituhumu Ikulu kuhusika na suala la ESCROW

Walimuita tumbiri,this time watamuita sokwe!!

wanahamu tena wa kumuita tumbili.imebidi wakazitazame sura zao upya ili kubaini ni wao tumbili ama kafulila duuu nahisi saga linaendelea jamaa kaamua kuwachojoa mpaka waliojificha hapo ikulu
 
Kwa hiyo huyo Tumbili aliyapata huko PCCB?
........kuhusu amepata wapi; hapo na mimi mgeni, ila ninachofahamu ni kwamba majina ya stabink yataendelea kufichwa, pengine mpaka pale wahusika itakapokuwa sio ishu hata wakijulikana, lini? ni suala la wakati
 
Huyu jamaa mbona hili suala kalifanya personal sana kuna nini nyuma yake..? Halafu mbona hayo majina ya hao vigogo hawayataji, wanaishia kusema kuna vigogo tu..???


Mwache akomae na Escrow; Skandali hii ni ya kihistoria; umewahi kuona wapi Tumbili akamkamata Mwizi?! tumezoea Mbwa wa Polisi na wa kujitegemea ndio hukamata wezi lakini kwa mara ya kwanza duniani; Tumbili kamkamata Mwizi!
Another first for Tanzania. david Kafulila komaaa mpaka kieleweke; umeandika historia; itakuwa vigumu sana rekodi yako kuvunjwa; at least not in the foreseable future; Tumbili kamkamata Mwizi; Go Go GO Kafulila!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi mbna huyu tumbili anatusumbua?hakuna wa kujitolea mhanga?
Ni kweli huyu MuHa sasa anajitafutia balaa kwani hili suala la Escrow
  1. Lilishajadiliwa Bungeni ambako ndiko kunakohusika
  2. Bunge limeshakabidhi kunakohusika ili walichukuliwe hatua wahusika
  3. Mahakama ilishakataza suala hili liko Mahakamani lisijadiliwe kwanza popote
  4. PAC imeshachunguza taarifa zote na kuziwakilisha kunakohusika ili Serikali ichukue mkondo wake
  5. Kafulila keshawavua nguo wapinzani wake hadharani sasa tunasubiri km ni kweli walichukua pesa si yao waadhibiwa na km ni yao basi wakazile salama sasa kuwachokonoa zaidi ni kujitafutia mabaya zaidi
Labda kwa ushauri tu Kafulila Siasa ni mchezo mchafu, hao Waandishi watakuponza kwani yameshawakuta wengi
kubali matokeo Serikali ichukue Mkondo kwani ikikataa huna la kuifanya kwani pesa ni za Habinder Singh
 
Namshauri Kafulila kama ana mapya zaidi kuhusu escrow,ni bora akawasiliana na kamati ya Zito kuliko kulipeleka peke yake!
 
Aisee hii ngoma mbichi ngoja tusubiri kauli ya ikulu
 
Nilijua tu ikulu inahusika na uchafu huu, ndo maana muhongo amegoma kujiuzulu!
Siyo Muhongo tu, hata Werema, Maswi na mama Tibaijuka, nao wamegoma katakata kujuuzulu.

Kwa kuwa wanajua hivyo vijisenti walivyoambulia, ni kama 10%. commission yao kwa kazi ya 'utarishi' wa kuvisambaza vimemo vya maelekezo ya mkulu, kuhusu namna ya kufanikisha dili zima hilo la Escrow account!
 
Toka lini repoti ya TAKUKURU ikawekwa kwenye public domain?

Halafu cha kushangaza, mtu anasimama kwa waandishi wa habari halafu anasema repoti ya TAKUKURU imetaja majina ya waliochukua pesa benki ya Stanbic, halafu hakuna mwandishi/waandishi wanaohoji kwa nguvu ya hoja mbele yake awatajie hayo majina.

Kwa lugha nyingine, Mhe. Kafulila atakuwa ameiona repoti ya TAKUKURU au ameelezwa majina ya waliotajwa kwenye repoti ya TAKUKURU.

Mhe. Kafulila hataki kuwataja ila anasubiri mtu anayesikia kutoka kwake ndiyo awataje?.

Hii ni sawasawa na hoja ya kusema watu walitumia magunia na rumbesa kubebea pesa halafu usiwataje hao watu.

Halafu kuanza kulijengea hoja suala la Tegeta Escrow account kwa mlengo wa chama ni kulifanya likose nguvu katika section ya jamii.

Kweli siasa za Tanzania siyo za wapita njia!
 
Wewe Lizabon kwanini ikulu isijibu na kumfungulia kafulila mashtaka maana huko ni kuchafua white house? Wewe umebakia kumuhujumu hon kafulila
 
Last edited by a moderator:
unauliza makofi polis? Jk na genge lake wamepageuza magogoni sehemu ya kuficha wezi wa mali za umma!
Tunayakumbuka sana sasa maneno ya hekima sana ya Mwalimu Nyerere, alipotanabaisha kuwa;

Ikulu ni mahali patakatifu, Ikulu siyo pango la walanguzi.

Kwa bahati mbaya sana, hawa mapresidaa wa awamu hizi zilizoongozana, wameigeuza Ikulu kuwa ni pango la walanguzi, wa design ya watu kama akina singasinga, ambao wameigeuza Ikulu kuwa sitting room yao, ambayo wakati wowote wautakao, wanakunywa kahawa hapo!
 
Huyu Tumbili anahangaika sana. Hili suala lilishafika kwenye kamati ya PAC, iweje yeye asimame peke yake?

jana nakuona unakatika tu kwenye mkutano wa kampeni za serikar za mitaaa yan mkuu unavituko wewe.
 
Back
Top Bottom