Kafulila afunguka tena, sasa aituhumu Ikulu kuhusika na suala la ESCROW

MJITA HALISI 176

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
537
0

Kafulila alipuka tena,sasa ni ikulu lawamani

Wakati rais jakaya kikwete akisuasua kuwachukulia hatua viongozi waliotajwa na bunge kuhusika katika wizi wa zaidi ya bilioni 320 kwenye akaunti ya tegeta esrcow ,naye mbunge wa kigoma kusini david kafulila ameibuka upya na ameivaa ikulu

Baada ya kusema ikulu ya rais jakaya kikwete inamedhamilia kuwalinda wezi waliohusika katika kuiba pesa hizo,baada ya kumzuia mkurugenzi wa ofisi ya kuzuia na kupambana na rushwa pccb dk edward hosea kutoiwasilisha taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la esrcow kwa umma kutokana na ripoti ya pccb kuwataja vigogo wa ikulu kuhusika katika kuchota pesa kwenye benk ya stabink.

Hayo yamebuliwa mda huu jijini dar es salaam na mbunge wa kigoma kusini david kafulila wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo kafulila huku akizungumza kwa uchungu alisema inasikitisha kuona jinsi ikulu inavyotumia ubabe wake kumzuia dk hosema kutoiweka wazi ripoti yake ya uchunguzi.

"tunafahamu wazi serikali inataka kuwalinda watu waliochota pesa,kutokana na kitendo chake kumzuia pccb asiweka hadharani ripoti kwa kisingizia uchunguzi ujakamilika,ujakamilika kivipi wakati tunakumbuka wazi mkurugenzi wa pccb dk hosea wakati kongamano la sadc kuhusu rushwa uliofanyika mkoani mwanza mwezi novemba"

"alisema ripoti yake ya uchunguzi kuhusu akaunti ya escrow umekamilika na tayari wameshamkabidhi waziri mkuu ingawa waziri huyo mkuu alikana,na hii yote inafanyika hivi ni kutokana na ripoti ya pccb kuwepo na majina ya vigogo wa ikulu ambao walichota pesa kwenye benki ya stabink"alisema kafulila

Kafulila aliongeza kuwa leo majina ya watu waliochota pesa kwenye benki ya mkombozi tu wanatajwa ,huku wengine kwenye benki ya stabink benki wakiachwa kwa kuwa ni vigogo wa ikulu.

"leo majina ambao kamati ya pac waliyopewa na pccb ni ya benki ya mkombozi huku majina ya benki ya stabink ambao watu walichota pesa kwa maboksi,sandalusi,magunia ambao wengi wao ni vigogo wakubwa wa ikulu wakiachwa,na ndio maana ikulu hii inakataza ripoti ya pccb iwekwe wazi kwakuwa itaweza kuvuruga nchi kwasababu wahusika waliochota pesa wengi ni watu wa ikulu"aliongeza kafulila.

Kuhusu jeuri ya mmiliki wa IPTL bwana seith

Kafulila ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha nccr mageuzi alisema jeuri aliyekuwa nayo bwana seith kwa kuzivimbia mamlaka zote ikiwemo mamlaka ya ukusanyaji kodi tra inatokana na kigogo huyo kufahamu wizi huo ameufanya na vigogo wa kubwa wanchi.

"huyu bwana seith anakuwa jeuri sana kwakuwa anauhakika pesa za escrow amekula na wengi hata akifanya jambo anajua wazi hakuna wakumchukulia hatua kwakuwa wako wengi, na hii inatokana kutokuwa na serikali makini ndio maana inamuacha huyo taperi kufanya anavyotaka ila serikali ijue huyo mtu avyojisifu hivi atakujakuleta machafuko nchini"alitabainisha kafulila.

Katika hatua nyingine mbunge huyo wa kigoma kusini alisema kwa sasa chama chake cha nccr kwa kushirikiana na umoja wao wa vyama vya upinzani nchini waanza rasmi kwenda kwa wananchi kuwaeleza kuhusu suala nzima lilivyo la escrow na wamepanga kuanza na mkoa wa kigoma.

"tuanza tena ziara mkoani kigoma kuhamasisha umma uelewe kuhusu ufisadi huu,na tunatawajulisha watanzania kuwa ccm haina uhalali wa kuchaguliwa kwasababu imeshindwa kuisimia serikali yake kwani makam mwenyekiti taifa na katibu wa ccm wamesisitiza kuwa wahusika wawajibike lakini wamegoma"alisema kafulila.

Chanzo:Habari24
 

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
593
500
Huyu jamaa mbona hili suala kalifanya personal sana kuna nini nyuma yake..? Halafu mbona hayo majina ya hao vigogo hawayataji, wanaishia kusema kuna vigogo tu..???
 

Komeo

JF-Expert Member
May 3, 2011
2,493
2,000
Haka nako ni ka uzi! Kuna mashindano ya kuanzia nyuzi? Tulia jaza magepu ili taarifa ije kamili.
 

stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,611
2,000
attention seeker, haya baba tumekusikia, this time around utakua maarufu zaidi. Hongera.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,939
2,000
Angewataja hao vigogo na kupeleka malalamiko yake pahali husika, ila hizi ngonjera sasa zinachosha.
 

time2ball

JF-Expert Member
Feb 4, 2014
289
500
Mh!! Nimeanza kuwa na wasiwasi na uhai wa Kafulila! he is trying to take on the mighty....... Mungu amlinde aisee! Wahusika ni wakubwa mno na pesa husika ni nyingi mno for him to be safe....
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
Huyu Tumbili anahangaika sana. Hili suala lilishafika kwenye kamati ya PAC, iweje yeye asimame peke yake?
 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,871
2,000
attention seeker, haya baba tumekusikia, this time around utakua maarufu zaidi. Hongera.
Tehetehetehe. Anatafuta umaarufu kwa njia za kijinga. Kala fedha za watu ili wamwadabishe Muhongo na Maswi. Sasa wanahangaika kusaka huruma ya wananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom