HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Huyo nae, kwanza kabisa kama anajali sana ya watu wengine awaambie wamchagulie.
Pili , anamuoa dada wa watu kisa kamlelea watoto tu basi? Nauliza maana sijaona sehwmu inayosema "anampenda".Kama hampendi badala ya kumuingiza dada wa watu kwenye ndoa isiyo na mapenzi bora aendelee kumlipa tu dada mpaka dada atakapobahatika kupata mtu anaeeleweka. Hivyo kama hana mapenzi nae sishauri, atakua hamtendei haki dada wa watu.Ila kama anampenda aangalie kwanini hao ndugu wanamnyima.Kama kisa ni vile anewahi kuwa dada wa kazi awapotezee hao ndugu na kumuoa huyo dada ikiwa nae anaridhia.
Lizy,
Hata kama haijasemwa, ila nimeelewa kuwa anapenda house girl wake wa zamani kwa sababu anawapenda watoto wake na kuwalea vizuri. Na kwa mjane, hilo ni jambo kubwa sana.
Is that not a strong reason to justify his love for the maid???
Babu DC!!
Helo Babu DC,
Mie dada mkubwa salimia wewe.
Naomba lift.
Babu DC bado sijashawishika kwamba anampenda bali anam-appreciate na anatafuta namna ya kumfunga huyo dada kamba ili aendelee kuwepo.Na hata kama anampenda kwa sababu hiyo tu, bado sioni kama inatosha kumtia dada wa watu pingu alafu baadae aanze kumwambia "mtu mwenyewe nilikuoa tu ili uendelee kunilelea watoto". . . . sio haki kwa mdada.
Lizzy please,
How many times should be saying this....
Ni vigumu sana, tena sana kwa mwanamume kupenda aisee....Tatizo ni kwamba ama mnasahau haya maneno au hamuyaamini.. Na mbaya zaidi mnadhani tuko sawa!! Mwanamume anatafuta maslahi na vigezo vyake kabla hajaanza kuu-condition moyo wake kumpenda mwanamke!!
Ngoja niishie hapa kwanza!!
Babu endeleeni hivyo hivyo na ugumu wenu, mimi bado ntaendelea kupinga na sitomshauri mtu aoe/aolewe na mtu iwapo yeye au huyo mwenzake hampendi kwa dhati maana ndio mwanzo wa kutengeneza viota nje bila kusahau kuleteana dharau na magonjwa ndani.
Lizzy please,
How many times should be saying this....
Ni vigumu sana, tena sana kwa mwanamume kupenda aisee....Tatizo ni kwamba ama mnasahau haya maneno au hamuyaamini.. Na mbaya zaidi mnadhani tuko sawa!! Mwanamume anatafuta maslahi na vigezo vyake kabla hajaanza kuu-condition moyo wake kumpenda mwanamke!!
ninayakumbuka na kuyaamini ila sikubaliani nayo hata kidogo.Kwa nini umuoe mtu kwa sababu sijui ni msafi,ana miguu mizuri,anajua kupika chakula kizuri bila kuwa na mapenzi? siku akipata ajali akapoteza mikono na kushindwa kupika hicho chakula kilichokuvutia kwake ndoa itakuwaje?