Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, wazee wa upako, mitume wa fedha, nk ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo. wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisasi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!
Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.
Kwao huduma kwa maskini haiwavutii kwa sababu moja tu, watu hawa ni maskini hawana sadaka ya kutoa, hivyo achana nao.
Hapo ndipo wenye akili wanaweza kuona ni wangapi kati ya hawa maskofu, wachungaji, manabii na mitume wanaishi kama Kristo Yesu alivyoagiza
Unaweza ukapita mwaka mzima hata mitatu bila kusikia wakihubiri neno UPENDO! Injili haisimami kama neno hilo halihubiriwi. UPENDO ndio yote katika yote.
Wafuatilie katika mahubiri yao na urekodi wanahubiri kuacha dhambi na KUMPENDA jirani mara ngapi kwa mwaka?
Utashangaa mwenyewe!
Utakachosikia kila siku ni habari ya jinsi ya kupata pesa, safari za nje, kupona ugojwa, sawa..... lakini hayo yote vilevile hayana maana kama hakuna UPENDO. Pesa bila upendo ni bure na mafanikio yoyote bila upendo hakuna kitu.
Hicho ndicho kipimo kikubwa cha ufuasi wa Kristo wa kweli kitumie utaona ukweli na utagundua kwamba siku hizi INJILI imevamiwa na majambazi na wanaohubiri dhidi ya mpinga Kristo kumbe mpinga Kristo ni wao wenyewe!
Kaa chonjo na mbwa mwitu hawa