Kaeni chonjo na wachungaji/manabii/maaskofu hawa

Kaeni chonjo na wachungaji/manabii/maaskofu hawa

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,953
Reaction score
24,843
Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, wazee wa upako, mitume wa fedha, nk ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo. wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisasi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!

Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.

Kwao huduma kwa maskini haiwavutii kwa sababu moja tu, watu hawa ni maskini hawana sadaka ya kutoa, hivyo achana nao.

Hapo ndipo wenye akili wanaweza kuona ni wangapi kati ya hawa maskofu, wachungaji, manabii na mitume wanaishi kama Kristo Yesu alivyoagiza

Unaweza ukapita mwaka mzima hata mitatu bila kusikia wakihubiri neno UPENDO! Injili haisimami kama neno hilo halihubiriwi. UPENDO ndio yote katika yote.

Wafuatilie katika mahubiri yao na urekodi wanahubiri kuacha dhambi na KUMPENDA jirani mara ngapi kwa mwaka?

Utashangaa mwenyewe!

Utakachosikia kila siku ni habari ya jinsi ya kupata pesa, safari za nje, kupona ugojwa, sawa..... lakini hayo yote vilevile hayana maana kama hakuna UPENDO. Pesa bila upendo ni bure na mafanikio yoyote bila upendo hakuna kitu.

Hicho ndicho kipimo kikubwa cha ufuasi wa Kristo wa kweli kitumie utaona ukweli na utagundua kwamba siku hizi INJILI imevamiwa na majambazi na wanaohubiri dhidi ya mpinga Kristo kumbe mpinga Kristo ni wao wenyewe!

Kaa chonjo na mbwa mwitu hawa
 
seriously , watu wengi wanafilisiwa na hawa watu , na wengine wanaacha kazi zao kwa ajili ya hawa watu. Hivyo mwenye macho haambiwi tazama.
 
Nashindwa kuelewa watu wanao enda kwenye makanisa hayo.Naamini kama una akili timamu
Na busara huwezi kwenda kwa hao watu hii ni sawa na watu wanao enda kucheza karata tatu,
wakati wanaelewa fikra hutaweza kushinda.
 
Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, wazee wa upako, mitume wa fedha, nk ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo. wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisasi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.Kwao huduma kwa maskini haiwavutii kwa sababu moja tu, watu hawa ni maskini hawana sadaka ya kutoa, hivyo achana nao.Hapo ndipo wenye akili wanaweza kuona ni wangapi kati ya hawa maskofu, wachungaji, manabii na mitume wanaishi kama Kristo Yesu alivyoagizaUnaweza ukapita mwaka mzima hata mitatu bila kusikia wakihubiri neno UPENDO! Injili haisimami kama neno hilo halihubiriwi. UPENDO ndio yote katika yote.Wafuatilie katika mahubiri yao na urekodi wanahubiri kuacha dhambi na KUMPENDA jirani mara ngapi kwa mwaka?Utashangaa mwenyewe!Utakachosikia kila siku ni habari ya jinsi ya kupata pesa, safari za nje, kupona ugojwa, sawa..... lakini hayo yote vilevile hayana maana kama hakuna UPENDO. Pesa bila upendo ni bure na mafanikio yoyote bila upendo hakuna kitu.Hicho ndicho kipimo kikubwa cha ufuasi wa Kristo wa kweli kitumie utaona ukweli na utagundua kwamba siku hizi INJILI imevamiwa na majambazi na wanaohubiri dhidi ya mpinga Kristo kumbe mpinga Kristo ni wao wenyewe!Kaa chonjo na mbwa mwitu hawa
Fazili wewe ni mkristo?Kama siyo unahangaika nini na kibanzi ktk jicho la mwenzio wakati wewe unaboriti ktk jicho lako!Kwenye dini yako kuna matatizo mengi mno mashehe wanafuga majini, wanageuka waganga wa kienyeji,wanaoa wanaume wenzao na matope mengine...
 
mkuu umenena, naamini c akili yako ya kibinadamu. hawa jamaa kwa namna walivyojichumia money
wangeanzisha hata kituo kimoja cha kulelea yatima walau
 
Kweli RC hata siku moja sijawahi kusikia wanahubiri khs mambo ya utajiri, kwenda ulaya na mengineyo mengi ya kipumbavu hawana. RC wana vituo vingi vya kulelea yatima, mahospitali, mashule, miradi mbali mbali ya kusaidia mpaka usuluhishi wa NDOA! Ndo maana wanahubiri UPENDO na bado wanatenda KIUPENDO NJE YA KANISA! Viva RC, Lutheran Anglikana!
 
heheee,.happy are those who are poor,for the kingdom of GOD is theirs,.!
 
fazil inaelekea we ni mkristo wa ukwee japo jima lako mmh! kanisa la kweli shart na sio ombi wakemee dhambi kwa nguvu. kusaidia yatima na wajane ni jukum la kila m2 kama unataka baraka. makanisa ya leo au modern churches wanapenda kuhubir mafanikio na baraka tu. en yet watu wao hawafanikiwi. neno la Mungu linasema utafuten kwanza UFALME WAKE NA HAKI YAKE na hayo yote mtazidishiwa. pale kwa kakobe nilijifunza hilo na ndo mana kila siku ntasema KAKOBE ni mtumish wa MUNGU wa ukweli
 
Fazili ningefurahi ungeenda step further kwa kutoa mifano ya hawa watu unasema!! vinginevyo inakuwa kama wanasiasa wa ccm amabao wanasema wapo watu wanatugawa kwa udini....watu mafisadi.....lkn hatasiku moja hajawahi kutaja ni akina nani?
 
Naunga Mkono Hoja,Kakobe ni Mashine Kubwa ndiyo maana serikali ya Ccm tangu wakati wa Mkapa na hawa watumishi wa Mungu Uchwara hawaachi kupiga kelele na hila za Kila aina!!!
 
fazil inaelekea we ni mkristo wa ukwee japo jima lako mmh! kanisa la kweli shart na sio ombi wakemee dhambi kwa nguvu. kusaidia yatima na wajane ni jukum la kila m2 kama unataka baraka. makanisa ya leo au modern churches wanapenda kuhubir mafanikio na baraka tu. en yet watu wao hawafanikiwi. neno la Mungu linasema utafuten kwanza UFALME WAKE NA HAKI YAKE na hayo yote mtazidishiwa. pale kwa kakobe nilijifunza hilo na ndo mana kila siku ntasema KAKOBE ni mtumish wa MUNGU wa ukweli
Hivi Kakobe ni maaskini eti eeeh? hamiliki mali? hajikusanyii zaka na kujinufisha mwenyewe au anagawia waumini wake maskini?, sio yeye anaewasema wenzie vibaya na kuwaombea mabaya ati wanafanya kazi ya shetani? sio yeye anajiona Mungu mtu hapa duniani ni mhubiri pekee na hakuna anaeweze kuhubiri ktk kanisa lake kama asipokuwepo anaweka CD aliojirekodi??? mhh nina mashaka sana.SII kokobe,sii mama rwakatale wala mwingira wote wanahubiri utajiri,na wamejaa usanii mtupu.Si ndio yeye alisema umeme wa tanesco hautawaka kwa vile umepita ktk kanisa lake??? si ndio huyu huyu hufunga safari za Nigeria kila wakati kuongeza nguvu za upako???? niishie hapa manake maswali hayataisha.
 
hivi huwa wanawalazimisha muende kwenye makanisa yao?nyie nendeni mkapigwe cha juu tu,after all wajinga ndiyo waliwao!
 
Fazili wewe ni mkristo?Kama siyo unahangaika nini na kibanzi ktk jicho la mwenzio wakati wewe unaboriti ktk jicho lako!Kwenye dini yako kuna matatizo mengi mno mashehe wanafuga majini, wanageuka waganga wa kienyeji,wanaoa wanaume wenzao na matope mengine...
don't judge the messenger but judge the message!
 
fazil inaelekea we ni mkristo wa ukwee japo jima lako mmh! kanisa la kweli shart na sio ombi wakemee dhambi kwa nguvu. kusaidia yatima na wajane ni jukum la kila m2 kama unataka baraka. makanisa ya leo au modern churches wanapenda kuhubir mafanikio na baraka tu. en yet watu wao hawafanikiwi. neno la Mungu linasema utafuten kwanza UFALME WAKE NA HAKI YAKE na hayo yote mtazidishiwa. pale kwa kakobe nilijifunza hilo na ndo mana kila siku ntasema KAKOBE ni mtumish wa MUNGU wa ukweli
Wako wakristo wengi ninaowajua wenye jina kama hilo
 
Fazili ningefurahi ungeenda step further kwa kutoa mifano ya hawa watu unasema!! vinginevyo inakuwa kama wanasiasa wa ccm amabao wanasema wapo watu wanatugawa kwa udini....watu mafisadi.....lkn hatasiku moja hajawahi kutaja ni akina nani?
Ingekuwa vyema awataje ili tudili nao sawia...
 
Hivi Kakobe ni maaskini eti eeeh? hamiliki mali? hajikusanyii zaka na kujinufisha mwenyewe au anagawia waumini wake maskini?, sio yeye anaewasema wenzie vibaya na kuwaombea mabaya ati wanafanya kazi ya shetani? sio yeye anajiona Mungu mtu hapa duniani ni mhubiri pekee na hakuna anaeweze kuhubiri ktk kanisa lake kama asipokuwepo anaweka CD aliojirekodi??? mhh nina mashaka sana.SII kokobe,sii mama rwakatale wala mwingira wote wanahubiri utajiri,na wamejaa usanii mtupu.Si ndio yeye alisema umeme wa tanesco hautawaka kwa vile umepita ktk kanisa lake??? si ndio huyu huyu hufunga safari za Nigeria kila wakati kuongeza nguvu za upako???? niishie hapa manake maswali hayataisha.
Unachosema hapo ni UDAKU au Fact, kwani hizo safari za NIGERIA ni lini kakobe kaenda Nigeria? Mimi nimewahi kuhudhuria siku kadha pale church kwake, kipindi Kakobe ameenda Korea, na kulikuwa na Wachungaji wengine tu wanaohubiri pale kwake. Ishu ya Umeme sitaki kumtetea Kakobe lakini mbona serikali yetu haijatoa Tamko kuwa Umeme unatumika from UBUNGO-KIJITONYAMA 132Kv Jaribu kufuatilia utaona. Nadhani utaona kwamba vilevile yeye ndiye sababu ya Mgao wa Umeme na kupingwa na kutokufanikiwa kwa Mhe. Ngeleja..... hahahah
 
Fazili wewe ni mkristo?Kama siyo unahangaika nini na kibanzi ktk jicho la mwenzio wakati wewe unaboriti ktk jicho lako!Kwenye dini yako kuna matatizo mengi mno mashehe wanafuga majini, wanageuka waganga wa kienyeji,wanaoa wanaume wenzao na matope mengine...

Kumbe wale maaskofu mashoga ni mashehe? asante sana kwa kujidanganya. Ama katika uislam ukimuona mtu yeyote anamiliki jini jua huyo ni muasi. Uzuzu huo huwezi kuukuta kwa kiongozi wa dini. Tatizo lenu wakristo hamjui nani ustadh na nani sheh nyie kila muislam mnakimbilia kumuita ustaz au shehe, wengine mnawapachika hivyo vyeo hali ya kuwa uislam hawaujui. Ila kwa kanisa machafu makubwa zikiwemo na biashara haramu zinafanywa na viongozi wa makanisa. Je kama kiongozi wako wa kanisa ndiye drug dealer, ndiye mgonga wake za waumini wake na kuwaingilia kinyume na maumbile watoto wadogo hapo unategemea huyo anamjua Mungu?
 
Unachosema hapo ni UDAKU au Fact, kwani hizo safari za NIGERIA ni lini kakobe kaenda Nigeria? Mimi nimewahi kuhudhuria siku kadha pale church kwake, kipindi Kakobe ameenda Korea, na kulikuwa na Wachungaji wengine tu wanaohubiri pale kwake. Ishu ya Umeme sitaki kumtetea Kakobe lakini mbona serikali yetu haijatoa Tamko kuwa Umeme unatumika from UBUNGO-KIJITONYAMA 132Kv Jaribu kufuatilia utaona. Nadhani utaona kwamba vilevile yeye ndiye sababu ya Mgao wa Umeme na kupingwa na kutokufanikiwa kwa Mhe. Ngeleja..... hahahah

kumbe na wewe ndio miongoni mwa wale mazuzu ambao huwekewa kanda ikawaongoza katika ibada? kuna baadhi ya wasomi huitwa wasomi wajinga, yaani anakuwa amesoma lakini elimu yake bado haimsaidii lolote kumtambua Mungu, sasa jipime mkuu ili uchukue hatua kabla hujachukuliwa hatua.
 
Back
Top Bottom