Kadi ya ccm

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,162
2,000
Jamani mimi ni kijana ambaye najisikia vibaya kuendelea kuitwa mwana sisisem, nina kadi ya sisisem na nataka niachane nao nijiunge na CHADEMA, naomba mnisaidie maswali yafuatayo yananitatiza:-
1. Ni lazima niende nikarudishe hii kadi ya sisisem au naweza kuitupa tu then nikachukua ya CHADEMA?
2.Kama nilazima niirudishe hii kadi ya sisisem, Kuna madhara yeyote ninayoweza kuyapata kikazi? kwasababu mimi ni mtumishi wa Serikali inayoongozwa na sisisem na mbaya zaidi mabosi wangu ni makada wa sisisem ambao wanamawasiliano ya karibu na viongozi wa chama. Maana nakumbuka mwaka 1994 Mzee wangu alikuwa sisisem akarudisha kadi yake wakati wa kampeni na akajiunga na NCCR Mageuz na baada ya mwezi mmoja na nusu alihamishwa kikazi kutoka Wizara fulani makao makuu Dsm na akapelekwa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwenda kuwa desk officer wa kawaida tu na ilimlazimu kuacha kazi maana ilikuwa ngumu kuhamisha familia ambayo alikuwa kaiwekea misingi yoote Dsm.

Plz nishauri.:hug:
 

Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,934
2,000
Kaa nayo tuu weka kwenye makumbusho yako kuwa ulikuwa mwanachama wa sisim! Mi mwenyewe siludishi na ipo makumbusho tuu!
 

kinya

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
495
225
uanachama ni imani then kama umiamu kwa dhati kuwa mwaCDM chakufanya chukua kadi na uwape hiya ya chama cheti kimya*2 au ukae nayo nyumbani unakuwa mwana chama mfu kwan utakuwa hulipi ada na vikao vya chama huhuzuri taratibu wanakusahau.
 

semango

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
532
195
Karibu kundini mzee...vyovyote ufanyavyo na hiyo kadi ni sawa tu.sisiem sio Mungu na hupaswi kuwaogopa kiasi hicho
 

Kiherehere

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,808
2,000
itupe ndugu yangu maana hapo baadae itakuwa inakukumbvusha machungu, so ni vyema ukaondokana na mnyumbuliko wa kimaisha baadae kwa kukaa nayo... fanya maamuzi haya sasa
 

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,403
0
hizi kadi ziliwahi tolewa high school ili uweze kujiunga na JKT pia university...... hivyo isikupe taabu.... its just a cardboard with printed hoe and hammer.... please neglect this grand corruption smart card and you are welcome to ..... born again
 

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,672
2,000
tembelea website ya chadema angalia jinsi ya kuchangia chama ukishachanga autonatikali unakuwa mwanachama. Achana na makadi hayo,
uwe na kadi ya ppf/nssf/gepf/lapf et al
uwe na kitambulisho cha kazi
uwe na kitambulisho cha bima ya afya
uwe na business card ya Mzito Kabwela et al
uwe na licence
uwe na kadi ya UVCCM
upewe kadi mpya na chadema.......
Changanya na zako.....
 

Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,874
2,000
Jamani mimi ni kijana ambaye najisikia vibaya kuendelea kuitwa mwana sisisem, nina kadi ya sisisem na nataka niachane nao nijiunge na CHADEMA, naomba mnisaidie maswali yafuatayo yananitatiza:-
1. Ni lazima niende nikarudishe hii kadi ya sisisem au naweza kuitupa tu then nikachukua ya CHADEMA?

Plz nishauri.:hug:
Tafadhali sana ilejeshe katika tawi lolote la karibu la CCM.
 

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,058
2,000
yangu iko museum! nikipata siku nkaonana na mzee malecela ntamkabishi maana ndo alinipa tehetehetehe! sasa nnayo ya chadema na kwa kutekeleza wajibu natembea nazo kwenye gari naziuza kisha kufanya marejesho ofisini chadema mkoa!!!

ezan! ukiishaipata kadi yako ya chadema ni jukumu lako la msingi kuingiza na wenzio kundini!!!

CCM imekuzeesha meza ebu angalia hiyo picha yako tehetehetehet!!
 

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,593
2,000
Iweke katika zile nyumba za Nyasi pale makumbusho ili kila anayeingia ktk nyumba hiyo akumbuke umaskini aliopewa na CCM.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom