Kadhia ya IPTL: Kumbe CCM na Baraza la Mawaziri walikuwa wamegawanyika!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Maelezo aliyoyatoa David Kafulila na Zitto Kabwe kuhusu kadhia ya Tegeta Escrow Account yamenifanya nishangae kidogo na katika mshangao huo yakanijaza fikra tunduizi kuhusiana na saga za IPTL.

Maelezo ya David Kafulila yanabainisha Baraza la Mawaziri lilikuwa limegawanyika ambapo mawaziri watano akiwezo Rais Magufuli walimwambia Kafulila kuwa akomae mpaka kieleweke kwa sababu ESCROW ni dili la wizi.

Kafulila amenukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema ‘’ Hatimaye imekuwa! Vinara katika ufisadi wa IPTL/ESCROW Singasinga Seth na Rugemarila watiwa nguvuni. Huu ni uamuzi mkubwa uliosubiriwa sana. Na siku zote sikujua kwanini Mhe Rais alikuwa anahofu kuagiza hatua hii. Sikujua kwanini, kwasababu wakati wa mnyukano wa hoja hii, Mhe Rais alikuwa bungeni na alikuwa sehemu ya maazimio ya Bunge kutaka mitambo ya IPTL itaifishwe na wahusika watiwe nguvuni. Nakumbuka nikiwa kwenye kipindi kigumu hata kutishwa kuondolewa kichwa na kuitwa majina ya wanyama, yeye alikuwa miongoni mwa mawaziri 5, walionidokeza kwamba ESCROW ni dili nikomae tu mpaka kieleweke! Nampongeza Mhe Rais kwa uamuzi huu muhimu uliosubiriwa siku nyingi kuamua hatma ya ufisadi huu uliomshinda vibaya mtangulizi wake’’.

Haikuishia kwa Kafulila pekee, hata Zitto kabwe amebainisha kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Mangula, Spika wa Bunge, Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai walikuwa upande wa Kamati ya PAC chini ya Zitto kuhakikisha mbivu na mbichi za sakata la IPTL zinawekwa wazi na kujulikana.

Zitto Kabwe amenukuliwa akisema, ‘’Spika Makinda na kabla yake Naibu spika Ndugai walitupa ushirikiano mkubwa. Ndugai alitwambia wakati wa kukabidhiwa ripoti, namnukuu "waelezeni Watanzania ukweli. Nipo nanyi". Kweli alikuwa nasi na ili kutupunguza nguvu akapewa safari ya ghafla kwenda Paris’’.

Aliendelea kusema, ‘’Pia tulijua kuwa wabunge wa CCM wakiweka msimamo wa kupinga, taarifa yetu itakwama. Siasa za kibunge uamuliwe kwa msingi wa Demokrasia wa "wengi wapi". Wabunge wa CCM ndio wengi bungeni, ukitaka jambo lako ni lazima ujenge ushawishi kwao. Ilibidi niongee na aliyekuwa Katibu Mwenezi, ndugu Nape Nnauye akiwa kwenye ziara mikoa ya Kusini na kumwambia amwombe Katibu Mkuu wao, ndugu Abdulrahman Kinana kuwa pasiwe na msimamo wa Chama chao kwenye jambo hili. Kuwe na Uhuru wa Wabunge wa CCM kuzungumza. Ndugu Kinana akatuhakikishia hilo. Deo Filikunjombe akazungumza na Mzee Mangula ambaye alikuwapo dodoma kumwomba hivyo hivyo’’.

Hoja za David Kafulila na Zitto Kabwe zinaleta maswali mbali mbali ambayo kuna uwezekano ikawa ni vigumu sana kupata majibu kutokana na viapo vya Mawaziri na watumishi wa serikali lakini ni muhimu kuuliza.

Je, ni nani aliyemshauri Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete kuhusiana na hili suala la IPTL wakati viongozi wengine wakuu wa CCM (Kinana na Mangula) wakionekana kuwa kinyume na baadhi ya maelezo ya Rais Kikwete?

Je, Mwanasheria Mkuu na Ofisi ya Rais walimpotosha Rais Kikwete kuhusiana na Tegeta Escrow Account?

Je, Suala la Tegeta Escrow Account halikujadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri?

Kama Suala la Tegeta Escrow Account lilijadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri, hawa Mawaziri watano akiwemo Rais Magufuli, walitoa hoja gani wakati wanajadili suala la IPTL kabla ya Rais Kikwete hajalihutubia Taifa.

Je, suala la Tegeta Escrow Account lilijadiliwa kwenye vikao vya juu vya CCM?

Kama lilijadiliwa kwenye vikao vikuu vya CCM, Kwa nini viongozi waandamizi wa CCM walimuacha Mwenyekiti wao wa Taifa akautangazia ulimwengu kuwa pesa za Tegeta Escrow Account hazikuwa za umma wakati wanajua zilikuwa niza umma?

Je, Nguvu ya CCM ni ipi katika kuisimamia serikali yake?

Je, CCM imejifunza nini kutokana na kadhia hii ya Tegeta Escrow Account?

Je, nini nafasi ya wananchi wengi katika usimamizi wa serikali na viongozi wake?
 
Nakubaliana na wewe, watu wanaogopa kukamatwa.


kweli mkuu mi najua ccm ni filikunjombe alikuwa mstari wa mbele kutetea hadi kuilinda ripot baadae akaja kigwangala


hao wakina magufuli walijificha kwenye migongo ya watu unafiki wake anauendeleza hadi leo kwenye mikutano anatangaza kwamba sisi wa tanzania tulibaki kidogo kuuzwa sasa hao wauzaji ni wa kina nani kama sio mkapa na kikwete ambapo chato ana mpongeza muuzaji ajabu sana nchi hii!!!!
 
kweli mkuu mi najua ccm ni filikunjombe alikuwa mstari wa mbele kutetea hadi kuilinda ripot baadae akaja kigwangala


hao wakina magufuli walijificha kwenye migongo ya watu unafiki wake anauendeleza hadi leo kwenye mikutano anatangaza kwamba sisi wa tanzania tulibaki kidogo kuuzwa sasa hao wauzaji ni wa kina nani kama sio mkapa na kikwete ambapo chato ana mpongeza muuzaji ajabu sana nchi hii!!!!
Huyu mzee kipindi nikiwa mtoto miaka ya 2000 kuja 2013 nilikuwa najua ni bonge la mchapakazi na mpenda watu kumbe nilikuwa najidanganya nimpenda sifa tu hakuna lolote.
 
Huyu mzee kipindi nikiwa mtoto miaka ya 2000 kuja 2013 nilikuwa najua ni bonge la mchapakazi na mpenda watu kumbe nilikuwa najidanganya nimpenda sifa tu hakuna lolote.

alitukamata kwa kukariri ma umbali ya barabara kumba mzee wa kamba balaa ndo mana kila siku anaongea mambo mapya anasahau alichotangulia cha awali
 
~~~>>>Magufuli huyu huyu aliyeshiriki kuuza nyumba za serikali ama yupi???

Magufuli huyu huyu wa kivuko kibovu ama yupi???


Magufuli huyu huyu wa barabara na madaraja yaliyo chini ya kiwango...



Kafulila kuwa makini ktk maandishi yako
 
Huyu mzee kipindi nikiwa mtoto miaka ya 2000 kuja 2013 nilikuwa najua ni bonge la mchapakazi na mpenda watu kumbe nilikuwa najidanganya nimpenda sifa tu hakuna lolote.
Kwa hiyo kwa sasa umekua?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom