KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
KadaMpinzani,
Hata kama unamchukia Mbowe hivyo, kweli unataka ahojiwe kwa hili?
Huo muda si afadhali tuwahoji hao majambazi wa EPA, Richmond, Meremeta nk. badala ya kuhangaika na akina Mbowe?
Nafikiri pia ni muumini wa freedom of speech kama ambavyo wewe mwenyewe unafaidika na uhuru huo haja JF, kweli kuna haja ya kuandika uliyoyaandika hapo juu?
Mwacheni Mbowe afanye kazi za chama chake.
wewe unaiita freedom of speech wakati ndio kitu kitakachomjenga kisiasa ! anajua akipakazia vitu vya uongo ndo atajijenga zaidi kisiasa, lakini sidhani kama nina chuki dhidi ya mbowe ! sipendi na sipendi kuona viongozi zaidi wakiuliwa wakati mbowe anajua njia inayotumika kuwaua hao viongozi ! ahojiwe ili matukio zaidi yasitokee !
KadaMpinzani,
Hata kama unamchukia Mbowe hivyo, kweli unataka ahojiwe kwa hili?
Huo muda si afadhali tuwahoji hao majambazi wa EPA, Richmond, Meremeta nk. badala ya kuhangaika na akina Mbowe?
Nafikiri pia ni muumini wa freedom of speech kama ambavyo wewe mwenyewe unafaidika na uhuru huo haja JF, kweli kuna haja ya kuandika uliyoyaandika hapo juu?
Mwacheni Mbowe afanye kazi za chama chake.
Nakupongeza kada mpinzani kwa hoja yako namimi. Nakuunga mkonokwamba Mbowe ahojiwe na wala sio swala la kumchukia huyo ni kiongozi wa chama kikubwa cha siasa.
Hivyo kauli yake una ushawishi mkubwa mbele ya wanachama wake na wananchi kwa ujumla. Ili kukomesha kauli hizo kwa maana yeye anawatambua wauwaji wa viongozi hao aisaidie polisi kwa kuwataja wauwaji hao ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mbele ya sheria nakupongeza sana.
Tutumie nguvu zetu zote kwa pamoja kushambulia ufisadi.
Kada Mpinzani
Sijui hili jina unalitumia kwa nini!! Narudia kukuuliza tena wewe unapojiita kada Mpinzani Unapinga nini?? Sisi tunajiita Wapinzani maana tunapinga UFISADI wa CCM!!!
Kada Mpinzani
Sijui hili jina unalitumia kwa nini!! Narudia kukuuliza tena wewe unapojiita kada Mpinzani Unapinga nini?? Sisi tunajiita Wapinzani maana tunapinga UFISADI wa CCM!!!
Unamshambulia Mbowe mpaka kila mmoja wetu amesharidhika kuwa assignment uliyopewa ni kum-embarass Mbowe. Najua wazi unafanya kazi ambayo huijui. Pili najua kuwa unamshambulia mtu ambaye humjui!!
Kama ungeijua task uliyopewa na ungejua unapambana na nani ungekuwa umeshaacha zamani. Maana kelele zako, unafiki wako, majungu yako, ushambenga wako na kila maudhi unayoingiza katika jukwaa dhidi ya Mbowe hayamshtui hata dakika moja.
Sana sana anakuhurumia tu mlala hoi wewe unatumiwa hovyo bila kujua thamani yako halisi.
Kwaheri.
Mkuu KM,
Naona umehitimu sasa maana hata mkapa wakati anaambiwa kuwa watu wanapora pesa za wananchi na yeye alijibu kama wewe kuwa mwenye ushaidi apeleke, lakini sasa ushaidi upo njenje, subiri siku moja mizimu ya watu mnaowaua itakapoamka na kudai haki yao ndo utajua kuwa na wewe umeponea chupuchupu kwa kuwa hauropoki hovyo au huna data za kutosha kusababisha wenzako wakuone kama tishio na kukukolimba.
mzee nashukuru sana kwa hili swali lako ! lakini nakushauri bonyeza profile yangu then angalia posts zangu za mwanzoni kabisa, nafikiri ndio utajua kwa nini nina jina la KadaMpinzani !! Hili swali nafikiri sio wewe tu unayeuliza, bali ni wengi sana humu ndani. Kama utaweza pia, jaribu kuuliza members wachache ambao walikuwa hapa from the beginning kabisa ndio utaelewa zaidi !
Nilipoingia humu kazi yangu ilikuwa ni moja na moja TU ! Kuipinga, kuishauri, kupendekeza machache kwa serikali lakini sikuwa based on any chama ! Lakini baadae nikagundua uchochezi unaongezeka humu ndani, kipindi hicho hata mbowe alikuwa member humu ndani, na nakumbuka nikamwandikia email mbowe kuhusu kumshauri masuala ya kuishinda ccm kwenye chaguzi, na haki ya Mungu alinijibu papo hapo ! But thats not what i was turned off by, lakini kulikuwa na increasingly pressure na uchochezi uliojaa na uonevu dhidi ya chama kimoja. Nilijaribu kugeuza mtazamo wa forum, kuhusu kuwajadili na wapinzani pia, lakini wapi, watu wakasema kwa nini wewe kada usiendelee kuwajadili hao wapinzani ? well, sikukata tamaa, lakini trust me mambo mengi i was turned off by. for more info, nenda kwenye posts zangu za mwanzoni kabisa !!
thats my own personal welfare, and i dont think kadampinzani here is the talk of the thread ! ishu hapa ni mbowe kuhojiwa kwa kauli alizotoa na sio kadampinzani ! shukrani !
CCM naichukia kupita kiasi, lakini kama ni wajanja, hii ni golden opportunity, yani golden opportunity ya kunawisha mikono yao inayoshutumiwa ina damu ya Ballali.
Wamfungulie Mbowe kesi ya madai ya defamation and libel. Akishindwa kuthibitisha kwamba Ballali kauawa, kina Mbowe na wenzake watajifunza kwamba conspiracy theories sio za kuzisema hadharani kana kwamba una uhakika, na wataacha kuendekeza kupotosha Umma na vitu visivyo thibitika.
Lakini sidhani kama ni nguvu ya dola itumike. Kesi isiwe Criminal inayoendeshwa na Serikali, bali Civil case ya CCM dhidhi ya Mbowe. Ubaya wa kamata-hoji inayotumia nguvu za dola ni kwamba nchi inaweza kugeuka Police State, ambamo kila tamshi la maoni ya mtu linakuwa Criminal. Katika Civil Law framework, aliye udhiwa akashitaki bila kuingiza nguvu za dola.
CCM kama wajanja hapa lazima wamshtaki Mbowe.