KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,716
- 86
Naam ni yule mwenyekiti chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Aikaeli Mbowe. Wiki iliyopita aliweza kutoa maneno makali ambayo kwa kweli ukiangalia kiundani kama unaipenda nchi yako basikamwe hutoweza kuacha hizo kauli ziende tu hivi hivi !
Mbowe ambae anakabiriwa na kesi ya kutolipa mamilioni ya shilingi aliyokopa NSSF aliyokopa kuendesha biashara yake, alisema kwamba vifo vya Marehemu Amina Chifupa na Ballali ambae alikuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania wameuliwa na CCM.
Sidhani kama kweli mtu ambae hakumaanisha anaweza kuongea mambo mazito kama haya. Hata kama tofauti za kisiasa mtu mwenye akili timamu hawezi kuongea maneno mazito kama haya halafu ategemee asihojiwe na vyombo vya dola. Kwa kweli nchi yangu ya Tanzania naipenda, na ndio maana nasema Mbowe ahojiwe ili aweze kutoa ushahidi wa kutosha na hao walioshiriki waweze kukamatwa na sheria ishike mkondo wake.
Bwana Mbowe alinukuliwa akisema, "Kuteketea kwa Ballali, tutaamini kuna mkono mchafu wa baadhi ya viongozi wa serikali, kwa sababu ni shahidi muhimu katika vita ya ufisadi. Wasifikiri kufa kwa Ballali, ndiyo mwisho wa mapambano, lakini nawaambia ndiyo kwanza vita ya ufisadi itapamba moto." hapo hapo pia aliendelea na kusema, "Ufisadi na mchezo mchafu wa CCM, umewatesa watoto wetu, wazazi wetu na sasa basi, tutapambana hadi watakapouana wote waishe. Wamemuua Ballali, Amina Chifupa wataendelea kuuana, . Hata hivyo Mbowe aliendea kuongea maneno hayo bilaya kutoa ushahidi wa kina ambao unaweza kuwafunga CCM na hao marehemu waliofariki.
- - - - - - - - - - - - - -MWISHO - - - - - - - - - - - - - - - -
Nini kinachotakiwa kifanyike:
(a) Kwa kuwa mbowe ana uhakika kwamba ccm imewaua hao watu, basi afikishwe kwenye vyombo vya dola na kuhojiwa ili kutoa ushahidi mzima.
(b) Kutokana na ushahidi atakaotoa, hao wafuatiliaji waweze kulinganisha na hali halisi ya matukio yaliyotokea ili kupata ukweli !
Naamini Mbowe atakuwa anajua zaidi ya hayo aliyosema, hivyo ahojiwe ili kupatikana ukweli !