KADA wa CHADEMA Mahakamani kwa kubaka mwanafunzi

KADA wa CHADEMA Mahakamani kwa kubaka mwanafunzi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Shafii Yatera (40) ameuanza vibaya Mwaka 2013 baada ya kusherekea Mwaka Mpya akiwa Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi.

Yatera alipandishwa kizimbani juzi mbele ya Hakimu mkazi, Sophia Masati, akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Msasani.

KADA huyo ndiye ambaye katika uchaguzi mkuu wa 2010 alichuana na mbunge wa sasa wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushika nafasi ya pili.

Akisomewa mashtaka yake, Wakili wa serikali Kanda ya Moshi, Oscar Ngole alidai kuwa Novemba 1, 2012 MSHTAKIWA ALIMWINGILIA KIMWILI MWANAFUNZI HUYO WA KIDATO NNE KINYUME CHA SHERIA.

Wakili huyo alidai kuwa kitendo alichokifanya mtuhumiwa huyo ni kunyume cha kifungu 130 (2) (e) na 131 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha miaka 30 jela. Hata hivyo kada huyo wa Chadema ambaye ni mkazi wa Pasua, mjini Moshi alikanusha mashtaka hayo, lakini upande wa mashtaka ukaiomba mahaka kuzui dhamana kwa sababu za kiupelelezi.

Wakili Ngole alidai kuwa endapo mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana ataathiri uchunguzi wa kesi hiyo kwa kile kinachodaiwa amekuwa akishawishi mwanafunzi huyo kutokutoa ushirikiano kwa polisi.

Hakimu Masati anayeisikiliza kesi hiyo allikubali ombi hilo la upande wa mashtaka na kuamuru mshtakiwa apelekwe rumande katika Gereza Kuu la Karanga hadi Januari 14, 2013 kesi hiyo itakapotajwa tena.


Source: Mwananchi.
 
Mkuu edit ulichokiandika sio chasema ni chadema.Halafu ndo tuendelee
 
Kada Maarufu wa CHADEMA,Shafii Yatera (40),ameuanza mwaka 2013 akiwa Gereza kuu la karanga Mjini Moshi.

Alipandishwa kizimbani juzi mbele ya hakimu mkazi Sophia Masati,akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 17 ambae ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Msasani.

Kada huyu ndiye ambae alichuana kwenye Uchaguzi mkuu wa 2010 jimbo la mwanga na Waziri wa Maji,Jumanne Maghembe na kushika nafasi ya pili.

Akimsomea mashtaka yake,wakili wa Serikali kanda ya Moshi,Oscar Ngole alidai kuwa Nov 1,2012,mshtakiwa alimwnglia kimwili mwanafunzi huyo wa kidato cha 4 kinyume na sheria.
Wakili huyo alidai kuwa mtuhumiwa alichokifanya ni kinyume na kifungu 130(2) (e) na 131 cha kanuni ya adhabu sura ya 16,adhabu yake ni jela miaka 30.

Kada alikanusha mashtaka hayo na kurudi rumande.

Source-Mwananchi,jumatano,januari 2,2013
 
umemaliza?haya nenda kachukue posho kwa nchemba,najua chadema inawaumiza sana kichwa ata baba yako mwigulu leo star tuongee asubuhi anaulizwa maswala ya cuf anajibu ya chadema,ata kijana yeyote akifanya kitu ni chadema tu,mabadiliko ni lazima kwenye nchii.
 
umemaliza?haya nenda kachukue posho kwa nchemba,najua chadema inawaumiza sana kichwa ata baba yako mwigulu leo star tuongee asubuhi anaulizwa maswala ya cuf anajibu ya chadema,ata kijana yeyote akifanya kitu ni chadema tu,mabadiliko ni lazima kwenye nchii.

Mkuu hakuna cha kumaliza ni aibu mgombea wenu wa ubunge wa CHADEMA kubaka.
 
umemaliza?haya nenda kachukue posho kwa nchemba,najua chadema inawaumiza sana kichwa ata baba yako mwigulu leo star tuongee asubuhi anaulizwa maswala ya cuf anajibu ya chadema,ata kijana yeyote akifanya kitu ni chadema tu,mabadiliko ni lazima kwenye nchii.
sasa na wewe mbona unatoka kwenye mada kama Nchemba?
 
Inasikitisha sana huyu kada wa Chadema mpaka anaamua kubaka.
Mkuu kwani wewe ujawahi kubaka?ikumbukwe kuwa siyo wote waliobaka waliweza kufikichwa mahakamani!
 
Duh hili nalo neno kutoka kwenye kugombea ubunge hadi kubaka.
Hila hako ka she kalitoa chenyewe .
 
Jopo la wanasheria wa Chadema wakiongozwa na Tundu Lissu, Prof Safari, Mabere Marando.

Kamanda kabaka mteteeni mpaka ashinde kesi.
 
Mtoto kumweleza mtoto mwenzie mambo ya kitoto tunasema wanacheza
 
Ha haa ha. Habari ya siasa imeletwa habari mchanganyiko...wakati habari za Nchemba zimeachwa jukwaa la siasa.
 
Back
Top Bottom