Kada Mashuhuri wa CCM Newala ajiunga CHADEMA

Kada machachari wa CCM jimbo la Newala Mtwara Adam Lawi Sijaona amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM.Kada huyo aliyekuwa msaada mkubwa kwa CCM jimboni humo na kipenzi cha wana-Newala amesema CCM sasa imepoteza mwelekeo na kuwataka wakazi wote wa jimbo hilo kumfuata ndani ya CDM.
Kada huyo ni mtoto wa mpigania uhuru wa Tanzania na muasisi wa TANU na CCM.Akihutubia umati mkubwa wa watu kada huyo aliishukuru CDM kwa kupeleka M4C kusini na kusema tangu uchaguzi mwaka juzi si mbunge wala diwani aliyeita wananchi walau hata kushukuru kwa kura walizopata.Kada huyo alikabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa .
 
Amefanya maamuzi bora kabisa, we unasubiri nini Hamia CDM.[/QU mim naogopa sijawah kuwa mwanchama wa chama pinzan nahgoja uchaguzi mwaka 2015 cdm ikishinda ntahamia ikishindwa naki humuhumu.
 
Wala si Mkatoliki na pia Familia yake ni WaAnglikana.Yeye kwa mujibu wa taarifa za uhakika nilizonazo ni Mtu wa Meditation katika Nuru na Sauti na ni strict vegetarian hali nyama ya aina yoyote wala mayai,
 
bandu bandu humaliza gogo,acha masisiem yajifariji kuwa alikuwa mzigo kumbe yanazidi kupungua kila uchao.T2015 CDM
 
yes YOU MADE A RIGHT CHOICE ITS A TIME NOW FOR OTHER NYINYIEM TO FOLLOW IN YOUR FOOT STEPS.
 
Ovyo kabisa, yaani mnafurahi kupata mtu ambaye ameshindwa kuendana na kasi ya chama bora Tz? Nyie wana chadema mna matatizo gani. Nahisi hata kama ikitokea siku mkaambiwa Jk amejiunga na chama chenu mtamkaribisha ili hali sasa mnamponda.
The unseen is illustrated by the seen.

mkuu sijakuelewa
mbona unasema chadema wamempokea mtu aliyeshindwa kuendana na kasi ya chama bora Tanzania, halafu unamtaja uliyemtaja eti naye akijiunga na chadema watafurahia kwani ni nani aliyekuambia ameshindwa kwenda na kasi ya hicho chama? uliimanisha nini?
 
Tarehe 9/01/2013 Uongozi wa Kitaifa UWT ulifika maalum kumshambulia Adam pale kijijini kwake Mnyambe.Yaliojiri pale yalionyesha dhairi ni jinsi gani wanamuogopa Kamanda huyu na Chadema kwa ujumla.Kumbe Ccm ndio wakabila na wadini.
 
mkuu sijakuelewa
mbona unasema chadema wamempokea mtu aliyeshindwa kuendana na kasi ya chama bora Tanzania, halafu unamtaja uliyemtaja eti naye akijiunga na chadema watafurahia kwani ni nani aliyekuambia ameshindwa kwenda na kasi ya hicho chama? uliimanisha nini?

Hatakujibu mkuu. Umemvua nguo hadharani
 
Baadhi ya maneno yao ni "Analeta mambo ya Kilimanjaro(2 Mmakonde na Mchaga wapi na wapi(3 Kwamba Adam ni Kibaraka na mengine mengi kiasi cha kustajaabisha kwa wamemfunga safari toka Dar maalum kwenda kumshambulia.hajasaidia kwani watu wanavua gamba%
 
Na bado watakuja wengi tu ila cha msingi ni kuwaangalia wanakujaje?! Isiwe kama hawa wengine wanaojifanya wanajua misemo kumbe wanafiki tu.
 
Back
Top Bottom