Kada Mashuhuri wa CCM Newala ajiunga CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Kada machachari wa CCM jimbo la Newala Mtwara Adam Lawi Sijaona amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM.Kada huyo aliyekuwa msaada mkubwa kwa CCM jimboni humo na kipenzi cha wana-Newala amesema CCM sasa imepoteza mwelekeo na kuwataka wakazi wote wa jimbo hilo kumfuata ndani ya CDM.
Kada huyo ni mtoto wa mpigania uhuru wa Tanzania na muasisi wa TANU na CCM.Akihutubia umati mkubwa wa watu kada huyo aliishukuru CDM kwa kupeleka M4C kusini na kusema tangu uchaguzi mwaka juzi si mbunge wala diwani aliyeita wananchi walau hata kushukuru kwa kura walizopata.Kada huyo alikabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa huku umati wa watu ukilipuka kwa shangwe.

Source:Tanzania Daima
 
Ovyo kabisa, yaani mnafurahi kupata mtu ambaye ameshindwa kuendana na kasi ya chama bora Tz? Nyie wana chadema mna matatizo gani. Nahisi hata kama ikitokea siku mkaambiwa Jk amejiunga na chama chenu mtamkaribisha ili hali sasa mnamponda.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Tunawakaribisha na wengine. Nape vipi, fanya maamuzi fasta.

Nape yuko busy kuwapachika majina walioona ukombozi.. Juzi aliwaita oil chafu.. Leo anawaita vinyago na kwamba ati kinyago ukichonge mwenyewe vpi kikuogopeshe.. Atayameza maneno yake huyu..
 
Ovyo kabisa, yaani mnafurahi kupata mtu ambaye ameshindwa kuendana na kasi ya chama bora Tz? Nyie wana chadema mna matatizo gani. Nahisi hata kama ikitokea siku mkaambiwa Jk amejiunga na chama chenu mtamkaribisha ili hali sasa mnamponda.
The unseen is illustrated by the seen.

Jionee aibu mwenyewe.Shame!
 
Aliombwa na Mbowe kugombea ubunge 2010 akakataa ila naona sasa amekubali rasmi kuwa kamanda. Anakubalika sana kwa umma. Jimbo hilo ni lake 2015.
 
Aliombwa na Mbowe kugombea ubunge 2010 akakataa ila naona sasa amekubali rasmi kuwa kamanda. Anakubalika sana kwa umma. Jimbo hilo ni lake 2015.

Hakika kwa jinsi alivyokuwa anashangiliwa na umma hilo jimbo hana mpinzani kabisa.
 
Back
Top Bottom