Kada CCM: Serikali ndiyo inayochochea machafuko

7th March 2011
Asema imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali
Asema Chadema kinapaswa kupongezwa kwa kusema ukweli
Amkosoa Tendwa kwa kauli zinazoonyesha anatumiwa na CCM
Operesheni Sangara kuingia mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameibuka na kusema kuwa serikali ndio inayochochea machafuko na kuhatarisha amani iliyopo nchini kutokana na kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kauli ya kada huyo wa CCM, Balozi Paul Ndobho, imekuja siku chache baada ya serikali na CCM kulaani maandamano Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kauli za viongozi wake kuwa zinalenga kuleta machafuko na kuhatarisha amani nchini.
Akizungumza na NIPASHE jana, Balozi Ndobho, alisema kinachofanywa na Chadema kinapaswa kupongezwa na ni jukumu la chama cha siasa kuzungumzia mambo ambayo yanashindwa kushughulikiwa na serikali iliyopo madarakani.

" Mimi ni mwana CCM kabisa ila maoni yangu ni kwamba serikali na chama ndivyo vinavyohatarisha amani ya nchi na kuleta machafuko kwa kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi pamoja na kushindwa kutatua kero ya umeme inayolikabili taifa," alisema Balozi Ndobho ambaye amewahi kuwa balozi wa Tanzania katika nchi kadhaa na Mbunge wa Musoma Vijijini 1995-2000 kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kabla ya kurejea CCM.

Alisema kauli za viongozi wa serikali na CCM kukishutumu Chadema ni wasiwasi wanaoupata baada ya kuona chama hicho kinaungwa mkono na idadi kubwa ya Watanzania hasa kinapozungumzia matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa.
"Kwanza sisi CCM tuna wasi wasi na ushindi tulioupata kutokana na madai kuwa kulikuwan na uchakachuaji. Hii ndiyo inayotutia hofu kwamba je, umati mkubwa wa wananchi katika mikutano ya Chadema unaweza kutuletea shida, sasa tunabuni hata vitu ambavyo havipo," alisema na kuongeza kuwa:

"Mimi nadhani serikali na viongozi wa chama tungesikiliza hoja za wenzetu na kuzipatia ufumbuzi, lakini kuzuia maandamano yao ndivyo unazidi kuzidisha hasira kwa wananchi."

"Unasema sukari ishuke je, kilichopanda hapa nchini ni sukari tu… kila kitu kimepanda, hali ya maisha ndio inayofanya watu kuichukia serikali na cha kufanya hapa ni vyema ukadhibiti hali hiyo, ufisadi na mambo mengine kama vile malipo ya Dowans na si kukimbia kulalamika tu, " alisema.

Aliwashauri baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao walijitokeza hadharani kupinga Chadema kutafakari kuwa kinachofanywa na chama hicho kina maslahi ya taifa hivyo kuacha kulinda maslahi yao badala ya wananchi waliowafikisha hapo.
Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuwa anaweza kuifuta Chadema, alimuonya kuacha kuzitoakwa kuwa zinaonyesha kuwa anaegemea upande wa chama tawala.

"Huyo Msajili anaweza kukifuta Chadema kwa kipi? " alihoji na kumuonya kuwa kwa kuchukua hatua hiyo anaweza kusababisha nchi isitawalike.

Balozi Ndobho alimtaka Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, kufanya maamuzi magumu ndani ya chama hicho kwa kuwaondoa viongozi wote ambao ni mzigo kwake kuanzia kwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

"Hivi Makamba anafanya kazi gani ndani ya chama, hata baadhi ya wajumbe wa NEC hawastahili hata kidogo kuendelea kuwa ndani ya chama. Huku kulindana kubaya na kama hawataki kubadilika wasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Watanzania wa leo si wa jana," alisema.

Aliongeza kuwa CCM imekuwa ikijidanganya kuwa bado inapendwa bila kutambua kuwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 45 sasa hawako tayari kuendelea kuwa na kadi za chama hicho na kuwataka viongozi wakuu wa chama kujipanga kuhakikisha wanarejesha imani kwa wananchi.

Kuanzia Februari 24, mwaka huu hadi Alhamisi iliyopita, Chadema kilifanya ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza, Mara, Shimyanga na Kagera ambapo wananchi wengi walijitokeza katika maandamano ya amani na mikutano ya hadhara katika miji ya makao makuu ya mikoa na wilaya.

Madhumuni ya maandamano na mikutano yalikuwa ni kuishinikiza serikali isiilipe Kampuni ya kufua umeme ya Dowans fidia ya Sh. Bilioni 94 kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) baada ya kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kukatisha mkataba wa kuzalisha na kuliuzia umeme.
Chadema pia kilikuwa kinaishinikiza serikali kushusha bei ya umeme pamoja na kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha.

Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa mwishoni mwa mwezi uliopita, aliyalaani maandamano ya Chadema kuwa yana mwelekeo wa kuvunja amani na yanawachochea wananchi kuichukia serikali yao.
Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo Augustino Mrema wa TLP) na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, walidai kuwa maandamano ya Chadema yana lengo la kutaka nchi isitawalike.

NYANDA ZA JUU KUSINI MWEZI UJAO

Wakati huo huo, Chadema kimepanga kuanza kuanza ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hivi mwezi ujao.

Wabunge wote na viongozi wa juu wa chama hicho wataweka kambi mkoani Mbeya hivi karibuni kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha umma kujiunga na chama hicho. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika wilayani Mbozi. Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano hayo yatakayofanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Aprili.

Imeandikwa na George Marato (Musoma) na Emmanuel Lengwa (Mbeya).

CHANZO: NIPASHE

Safi saaaana Mzee Ndobho kwa hisia zako zilizojaa ukweli na dira kwa Taifa letu. Tunao wachache Tanzania hii wanaoweza kuona mwanga kama uluouona ktk Chadema. Wengine wote wamemezwa na Ufisadi, waoga, wanakimbia vivuli vyao na wanaogopa hata wakisikia Dr Slaa au Mh Mbowe wanakohoa tu, sembuse na kutoboa ukweli kama wafanyavyo sasa....ambao ndio kilio cha wananchi wamefichwa ukweli kwa miaka karibia 50! HAKUNA WA KUZUIA ukweli!!

Kwa kweli kilichobaki CCM sasa sio chama ila ni vivuli vya watu wanaoogopa, wanaomba msaada kulindwa na majeshi na usalama wa taifa pamoja na msajili wa vyama - mamluki huyu aliyejaa porojo zisizo na dira kwa taifa.

CCM inakufa....nata kada wa siku nyingi na Mkiti wa Mkoa wa Dodoma Mh Ndejembi alisema ktk Mwananchi jana kuwa CCM inaingia shimoni, inakufa, inakosa hata wa kumfundinsha mwenzake ndani ya chama namna ya kukiongoza chama. wanabaki kulalama wenyewe kwa wenyewe, na kutafuta visingizio ili waonewe huruma na wananchi wakati wao ndio wameangamiza maisha ya wananchi hao hao...!

Sumaye naye amewaambia maneno kama hayo. wanabaki kumkimbia...wanaomba polisi wawalinde huku walianza na uchochezi wa kutumia udini wamekwama, wameenda ktk ukabila wamekwama na sasa wanaenda kwa 'uhaini' napo watakapoishia ni pabaya...! tupo makini tunafuatilia...

SANGARA ISAMBAE NCHI NZIMA, UKOMBOZI HAUPO UKUTA WA KUUZUIA...NCHI NI YA WANANCHI, WANAHITAJI KUUJUA UKWELI WA NCHI YAO, NDICHO WAFANYACHO CHADEMA - NDICHO WAFANYACHO DR SLAA, MH MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA, NDIO CHAMA CHA UKOMBOZI KWA TANZANIA.....CCM WAPOTELEE MBALI, WAJIFICHE, WAMESHINDWA KUSIMAMA, WANATAWALIWA NA MAFISADI WATAONGEA NINI, KWA MASLAHI YA NANI??!
 
7th March 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Asema imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali
Asema Chadema kinapaswa kupongezwa kwa kusema ukweli
Amkosoa Tendwa kwa kauli zinazoonyesha anatumiwa na CCM
Operesheni Sangara kuingia mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameibuka na kusema kuwa serikali ndio inayochochea machafuko na kuhatarisha amani iliyopo nchini kutokana na kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, vitendo vya rushwa na ufisadi.
Kauli ya kada huyo wa CCM, Balozi Paul Ndobho, imekuja siku chache baada ya serikali na CCM kulaani maandamano Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kauli za viongozi wake kuwa zinalenga kuleta machafuko na kuhatarisha amani nchini.
Akizungumza na NIPASHE jana, Balozi Ndobho, alisema kinachofanywa na Chadema kinapaswa kupongezwa na ni jukumu la chama cha siasa kuzungumzia mambo ambayo yanashindwa kushughulikiwa na serikali iliyopo madarakani.
" Mimi ni mwana CCM kabisa ila maoni yangu ni kwamba serikali na chama ndivyo vinavyohatarisha amani ya nchi na kuleta machafuko kwa kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi pamoja na kushindwa kutatua kero ya umeme inayolikabili taifa," alisema Balozi Ndobho ambaye amewahi kuwa balozi wa Tanzania katika nchi kadhaa na Mbunge wa Musoma Vijijini 1995-2000 kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kabla ya kurejea CCM.
Alisema kauli za viongozi wa serikali na CCM kukishutumu Chadema ni wasiwasi wanaoupata baada ya kuona chama hicho kinaungwa mkono na idadi kubwa ya Watanzania hasa kinapozungumzia matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa.
" Kwanza sisi CCM tuna wasi wasi na ushindi tulioupata kutokana na madai kuwa kulikuwan na uchakachuaji. Hii ndiyo inayotutia hofu kwamba je, umati mkubwa wa wananchi katika mikutano ya Chadema unaweza kutuletea shida, sasa tunabuni hata vitu ambavyo havipo," alisema na kuongeza kuwa:
" Mimi nadhani serikali na viongozi wa chama tungesikiliza hoja za wenzetu na kuzipatia ufumbuzi, lakini kuzuia maandamano yao ndivyo unazidi kuzidisha hasira kwa wananchi.”
" Unasema sukari ishuke je, kilichopanda hapa nchini ni sukari tu… kila kitu kimepanda, hali ya maisha ndio inayofanya watu kuichukia serikali na cha kufanya hapa ni vyema ukadhibiti hali hiyo, ufisadi na mambo mengine kama vile malipo ya Dowans na si kukimbia kulalamika tu, " alisema.
Aliwashauri baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao walijitokeza hadharani kupinga Chadema kutafakari kuwa kinachofanywa na chama hicho kina maslahi ya taifa hivyo kuacha kulinda maslahi yao badala ya wananchi waliowafikisha hapo.
Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuwa anaweza kuifuta Chadema, alimuonya kuacha kuzitoakwa kuwa zinaonyesha kuwa anaegemea upande wa chama tawala.
" Huyo Msajili anaweza kukifuta Chadema kwa kipi? ” alihoji na kumuonya kuwa kwa kuchukua hatua hiyo anaweza kusababisha nchi isitawalike.
Balozi Ndobho alimtaka Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, kufanya maamuzi magumu ndani ya chama hicho kwa kuwaondoa viongozi wote ambao ni mzigo kwake kuanzia kwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.
" Hivi Makamba anafanya kazi gani ndani ya chama, hata baadhi ya wajumbe wa NEC hawastahili hata kidogo kuendelea kuwa ndani ya chama. Huku kulindana kubaya na kama hawataki kubadilika wasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Watanzania wa leo si wa jana," alisema.
Aliongeza kuwa CCM imekuwa ikijidanganya kuwa bado inapendwa bila kutambua kuwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 45 sasa hawako tayari kuendelea kuwa na kadi za chama hicho na kuwataka viongozi wakuu wa chama kujipanga kuhakikisha wanarejesha imani kwa wananchi.
Kuanzia Februari 24, mwaka huu hadi Alhamisi iliyopita, Chadema kilifanya ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza, Mara, Shimyanga na Kagera ambapo wananchi wengi walijitokeza katika maandamano ya amani na mikutano ya hadhara katika miji ya makao makuu ya mikoa na wilaya.
Madhumuni ya maandamano na mikutano yalikuwa ni kuishinikiza serikali isiilipe Kampuni ya kufua umeme ya Dowans fidia ya Sh. Bilioni 94 kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) baada ya kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kukatisha mkataba wa kuzalisha na kuliuzia umeme.
Chadema pia kilikuwa kinaishinikiza serikali kushusha bei ya umeme pamoja na kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha.
Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa mwishoni mwa mwezi uliopita, aliyalaani maandamano ya Chadema kuwa yana mwelekeo wa kuvunja amani na yanawachochea wananchi kuichukia serikali yao.
Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo Augustino Mrema wa TLP) na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, walidai kuwa maandamano ya Chadema yana lengo la kutaka nchi isitawalike.
NYANDA ZA JUU KUSINI MWEZI UJAO
Wakati huo huo, Chadema kimepanga kuanza kuanza ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hivi mwezi ujao.
Wabunge wote na viongozi wa juu wa chama hicho wataweka kambi mkoani Mbeya hivi karibuni kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha umma kujiunga na chama hicho.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika wilayani Mbozi.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano hayo yatakayofanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Aprili.
Imeandikwa na George Marato (Musoma) na Emmanuel Lengwa (Mbeya).
CHANZO: NIPASHE

get more here www.lifeofmshaba.com
 
Ukweli uko wazi ila waporipori wengine wa ccm wagumu kuelewa, wanapindisha hoja tuuuuu, yaani watu wengine bana sasa tendwa naye amekuwaje?
 
Kumbe ndani ya CCM bado kuna watu wanauwezo wa kufikiri na kuyaona mambo kwa upana wake! Hongera Balozi labda wewe ukiwaambia watakuelewa, maana tukisema sisi tunaambiwa "tunataka kuipindua serikali"! Sasa balozi ungana na Sumaye mkatembelee pale Ikulu mumkumbushe mwenyekiti kuwa " akiwa msituni hawezi kuona msitu, atakachoona ni miti tu" ninyi mlio nje ndio mnauona msitu!

Tupo wengi tunaoona ukweli, ila wengine waoga kusema hadharini, lakini kweye vikao vyetu vya siri, tuanaambiana ukweli huo.
 
Kwa kauli za balozi Ndobho tutamsikia makamba aidha tambwe hiza wanasema jamaa sio raia na pia hawamtambui kama mwanachama wao.
Natamani kama Mwl. Nyerere arudi ajionee mwenyewe uozo wa vijana wake aliowaachia chama jinsi walivyolewa madaraka na kusahau kabisa kuwatumikia wananchi. Bila shaka hata yeye angerudisha kadi ya ccm na kujiunga na chadema bila hata kujiuliza mara 2
 
well said balozi kimsingi hapa serikali inatakiwa kutatua haya matatizo na si kuzuia maandamano. maandamano haya yanatakiwa kuungwa mkono hata na kikwete mwenyewe na wanasisiem wote. kwani maada zinazozungumzwa huko ni uhalisia wa maisha ya watanzania na si awanachadema. mfumuko wa bei za bidhaa na matatizo ya umeme si kwambayanawahusu wanachadema tuu bali watanzania wote. ukiona unamkanyaga mtu halafu hasemi ujue huyo si mzima ana matatizo. serikali inatukanyaga iache tuseme kwani sisi ni wazima.
 
Barozi kanena, Sijui kama Kikwete kamsikia! au katia pamba sikioni!, au kafunikwa na Blanketi la Ufisadi hasikii? au yupo ndani ya jumba la Udini haoni matatizo ya watanzania wala hasikii kelele zao? Kweli sikio la kufa halisikii dawa
 
Back
Top Bottom