Kada CCM: Serikali ndiyo inayochochea machafuko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada CCM: Serikali ndiyo inayochochea machafuko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Mar 7, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  7th March 2011
  Asema imeshindwa kudhibiti matumizi mabaya ya rasilimali
  Asema Chadema kinapaswa kupongezwa kwa kusema ukweli
  Amkosoa Tendwa kwa kauli zinazoonyesha anatumiwa na CCM
  Operesheni Sangara kuingia mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

  Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameibuka na kusema kuwa serikali ndio inayochochea machafuko na kuhatarisha amani iliyopo nchini kutokana na kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa, matumizi mabaya ya rasilimali za umma, vitendo vya rushwa na ufisadi.

  Kauli ya kada huyo wa CCM, Balozi Paul Ndobho, imekuja siku chache baada ya serikali na CCM kulaani maandamano Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kauli za viongozi wake kuwa zinalenga kuleta machafuko na kuhatarisha amani nchini.
  Akizungumza na NIPASHE jana, Balozi Ndobho, alisema kinachofanywa na Chadema kinapaswa kupongezwa na ni jukumu la chama cha siasa kuzungumzia mambo ambayo yanashindwa kushughulikiwa na serikali iliyopo madarakani.

  " Mimi ni mwana CCM kabisa ila maoni yangu ni kwamba serikali na chama ndivyo vinavyohatarisha amani ya nchi na kuleta machafuko kwa kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi pamoja na kushindwa kutatua kero ya umeme inayolikabili taifa," alisema Balozi Ndobho ambaye amewahi kuwa balozi wa Tanzania katika nchi kadhaa na Mbunge wa Musoma Vijijini 1995-2000 kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kabla ya kurejea CCM.

  Alisema kauli za viongozi wa serikali na CCM kukishutumu Chadema ni wasiwasi wanaoupata baada ya kuona chama hicho kinaungwa mkono na idadi kubwa ya Watanzania hasa kinapozungumzia matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa.
  "Kwanza sisi CCM tuna wasi wasi na ushindi tulioupata kutokana na madai kuwa kulikuwan na uchakachuaji. Hii ndiyo inayotutia hofu kwamba je, umati mkubwa wa wananchi katika mikutano ya Chadema unaweza kutuletea shida, sasa tunabuni hata vitu ambavyo havipo," alisema na kuongeza kuwa:

  "Mimi nadhani serikali na viongozi wa chama tungesikiliza hoja za wenzetu na kuzipatia ufumbuzi, lakini kuzuia maandamano yao ndivyo unazidi kuzidisha hasira kwa wananchi."

  "Unasema sukari ishuke je, kilichopanda hapa nchini ni sukari tu… kila kitu kimepanda, hali ya maisha ndio inayofanya watu kuichukia serikali na cha kufanya hapa ni vyema ukadhibiti hali hiyo, ufisadi na mambo mengine kama vile malipo ya Dowans na si kukimbia kulalamika tu, " alisema.

  Aliwashauri baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao walijitokeza hadharani kupinga Chadema kutafakari kuwa kinachofanywa na chama hicho kina maslahi ya taifa hivyo kuacha kulinda maslahi yao badala ya wananchi waliowafikisha hapo.
  Akizungumzia kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa kuwa anaweza kuifuta Chadema, alimuonya kuacha kuzitoakwa kuwa zinaonyesha kuwa anaegemea upande wa chama tawala.

  "Huyo Msajili anaweza kukifuta Chadema kwa kipi? " alihoji na kumuonya kuwa kwa kuchukua hatua hiyo anaweza kusababisha nchi isitawalike.

  Balozi Ndobho alimtaka Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, kufanya maamuzi magumu ndani ya chama hicho kwa kuwaondoa viongozi wote ambao ni mzigo kwake kuanzia kwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

  "Hivi Makamba anafanya kazi gani ndani ya chama, hata baadhi ya wajumbe wa NEC hawastahili hata kidogo kuendelea kuwa ndani ya chama. Huku kulindana kubaya na kama hawataki kubadilika wasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, Watanzania wa leo si wa jana," alisema.

  Aliongeza kuwa CCM imekuwa ikijidanganya kuwa bado inapendwa bila kutambua kuwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 45 sasa hawako tayari kuendelea kuwa na kadi za chama hicho na kuwataka viongozi wakuu wa chama kujipanga kuhakikisha wanarejesha imani kwa wananchi.

  Kuanzia Februari 24, mwaka huu hadi Alhamisi iliyopita, Chadema kilifanya ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza, Mara, Shimyanga na Kagera ambapo wananchi wengi walijitokeza katika maandamano ya amani na mikutano ya hadhara katika miji ya makao makuu ya mikoa na wilaya.

  Madhumuni ya maandamano na mikutano yalikuwa ni kuishinikiza serikali isiilipe Kampuni ya kufua umeme ya Dowans fidia ya Sh. Bilioni 94 kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) baada ya kulishitaki Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kukatisha mkataba wa kuzalisha na kuliuzia umeme.
  Chadema pia kilikuwa kinaishinikiza serikali kushusha bei ya umeme pamoja na kulalamikia kupanda kwa gharama za maisha.

  Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa mwishoni mwa mwezi uliopita, aliyalaani maandamano ya Chadema kuwa yana mwelekeo wa kuvunja amani na yanawachochea wananchi kuichukia serikali yao.
  Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwemo Augustino Mrema wa TLP) na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, walidai kuwa maandamano ya Chadema yana lengo la kutaka nchi isitawalike.

  NYANDA ZA JUU KUSINI MWEZI UJAO


  Wakati huo huo, Chadema kimepanga kuanza kuanza ziara ya Operesheni Sangara katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini hivi mwezi ujao.

  Wabunge wote na viongozi wa juu wa chama hicho wataweka kambi mkoani Mbeya hivi karibuni kwa ajili ya kuendelea kuhamasisha umma kujiunga na chama hicho. Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, alitoa taarifa hiyo juzi wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika wilayani Mbozi. Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano hayo yatakayofanyika baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Aprili.

  Imeandikwa na George Marato (Musoma) na Emmanuel Lengwa (Mbeya).


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  CCM wakiambiwa ukweli wanasema watu wanachochea machafuko tatizo kubwa ni kuwa hawana hoja za msingi za kujibu tuhuma ambazo Chadema wanaelekeza kwao.
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tutamnyang'anya kadi huyu!
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwani kadi ndio ina determine nini???
   
 5. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Ila msinyang'anye uraia wake. Utasikia huyu ni Mkikuyu toka kenya
   
 6. m

  mtimbwafs Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama balozi na kada wa ccm anasema hivi basi wajue kwamba mwisho wa udhalimu umekaribia.

  Mimi naona serikali ya kikwete itoe shukrani kwa chadema kwa kuibu changamoto zinazoikabili na kutafuta njia sahihi za kutatua changamoto hizo ili wawe na chakutuambia mwaka 2015 na wasiwe waoga wa kupinduliwa kwa kuwa watanzania sasa tunataka maendeleo na si maneno matupu yasiyo na tija.
   
 7. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mapenzi kwa chama hayapimwi na kadi, Nyerere alikuwa kinara wa CCM lakini alipata kusema CCM sio mamake kiasi kwamba unshindwe kum-trash.
  Mnyang'anyeni kadi lakini ujumbe umefika.

  Hoja hujibiwa kwa hoja!

  Wakitumia nguvu kujibu hoja za Chadema mliowaona wakiandamana Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera nao watatumia nguvu.
   
 8. A

  Anaruditena Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanatumia njia siositaiki kujibu CDM - Watanzania wanataka maisha yao yaboreshwe. sio kuwapa uongo mara tatu kwa kutwa kama panadol( kupunguza maumivu). Serikali haina msemaji, wote wanasema ovyo ovyo tu.
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  imewashika pabaya-uwezo wa kuugeuza ukweli aambao umeelezwa na CDM kuwa uongo ipo kazi kubwa. wananhci wa leo sio wa 1950's
   
 10. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Baada ya Sinkala atakuja Tambwe. CCM wakikosolewa wanasema hao wakosoaji wanleta vurugu.
  Ngoja tuone. CCM matofali wanayotaka kujengea waliyachanganya kwa ratio yenye mchanga mwingi!
   
 11. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  wazo la great thinker hilo......................heeeee kazi iiipo sa sijui ungesoma na shule za kata ingekuaje hiyo bongo yako
   
 12. S

  SUWI JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Safi balozi... vitawekwa vikao kwa ajili yako ila usiogope mtegemee Mungu maana yeye husimama upande wa mwenye haki. Msema kweli ni kipenzi cha Mungu. BIG UP!!!:A S 112:
   
 13. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawa CCM bado wamelewa chakari na hangover za zama zile:
  1: Wakati ule wa zama za ..Zidumu fikra za Mwenyekiti,.. , kidumu CHAMA..
  2: za CHAMA kimoja kwa maana bila CCM hakuna chama kingine, pamoja na kuwa na demokrasia ya vyama vingi
  3: Udikteta wa chama kimoja kushika hatamu za uongozi wa nchi, kama ilivyo leo hii
  4: za Watanzania kudanganyika kwa kila aina ya UOZO kwa sababu ya mambo ya ki-analogue (lack of info)
  .
  .
  Inabidi wakumbuke tu kwamba ni kweli HATUDANGANYIKI tena kama zama zile. People are informed, are aware of their POWER. It is imminent that PEOPLES POWER shall persist. Reform au PERISH
   
 14. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Haa haa haaa! Mkuu, mimi sipo huko kwa mafisadi, niliweka hiyo kuashiria quote ya typical Sisiem member asiyependa ukweli! Nilimpigia kura Slaa, Mnyika na diwani wa CHADEMA, na mbunge na diwani wakashinda!
   
 15. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I know u are joking!!...Waanze tu waone na nyingine zitazofuata....petroli ishamwagika ansubiriwa wa kuwasha kiberitu tu..kwa taarifa yako na Jakaya, hata wana CCM wamechoka na udhaifu wa mwenyekiti wao na ugumu wa maisha,ufisadi nk nk
   
 16. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  Sasa CCM mawazo kama ya huyu PNdobho ndiyo wanaona hatari kabisa kwa usalama wa taifa.....hongera balozi!!!!
  CCM imekufa!
   
 17. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nawaonea huruma hawa wehu ccm eti wanalalamika wananchi wanasumbuliwa kulazimishwa kwenda kwenye maandamano lakini hakuna hata mwananchi mmoja aliyehojiwa na kutoa malalamiko kuwa maandamano yanawaletea usumbufu?
  "CCM kama mavi hawabebeki tena ukiwabeba utaishia kunuka na kuzomewa na nzi"
   
 18. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  well said balozi ccm bado wana ishi kwenye ndoto za chama kimoja wote wanatakiwa wapigwe vibao km mzee ruksa alivyonaswa na yule dogo
   
 19. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ndobho daaah,enzi hizo nakumbuka tulikuwa tunaimba "ndobho mbunge wetu,mkapa raisi wetu" duh kumbe bado yupo hai?

  Long tyme,utotot huu ni balaa
   
 20. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kumbe ndani ya CCM bado kuna watu wanauwezo wa kufikiri na kuyaona mambo kwa upana wake! Hongera Balozi labda wewe ukiwaambia watakuelewa, maana tukisema sisi tunaambiwa "tunataka kuipindua serikali"! Sasa balozi ungana na Sumaye mkatembelee pale Ikulu mumkumbushe mwenyekiti kuwa " akiwa msituni hawezi kuona msitu, atakachoona ni miti tu" ninyi mlio nje ndio mnauona msitu!
   
Loading...