Kada CCM avamiwa, acharangwa mapanga Dar

Uko kwenye gari usiku mtu anakugongea yuko na pikipiki unakubali fungua
 
Sasa uccm wake umehusikaje hapo kwani hafahamiki mpaka atambulishwe kwa uccm wake?!
Huyu yeye hakujiteka na kujichanja wembe?! Na sio mambo ya mapenzi?!
 
Kuna mengi Sana juu ya kuvamiwa kwa TL.... Haiwezekani wakivamiwa Chadema tuseme tuu Ni CCM na akivamiwa CCM tuseme Ni CCM wenyewe... Uvivu was kufikiri hutoa majibu ya uongo sana
 
Tusifike huko ila uvccm wakiachwa bila kuonnywa wanaweza kuliingiza Taifa kwenye Rabsha.
Hao kuzichapa ni kawaida. Ni kama jumba LA wachawi
cccm2.jpeg
 
Kuna uwezekano alikuwa tingasi...
Mil 11 anatembea nazo kwenye gari, saa 5 usiku, alafu unagongewa dirisha la gari unafungua. Jamani, security alerts ndogo ndogo mjue zitawasaidia sana maishani..!!
 
Kuna mengi Sana juu ya kuvamiwa kwa TL.... Haiwezekani wakivamiwa Chadema tuseme tuu Ni CCM na akivamiwa CCM tuseme Ni CCM wenyewe... Uvivu was kufikiri hutoa majibu ya uongo sana
Sasa ajabu nini wakati roho ya kuua na kujeruhi iko ndani ya miili ya wanaccm?
Hujasikia kauli za Kigwangwala, Msafiri, yule RC wa Mbeya? Hata na wakati fulani Bashe aliongea maneno ya ajabu sana! Sasa kama viongozi wako hivyo hao wafuata upepo watakuaje?
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa mgombea ubunge wa Vunjo kupitia chama hicho mwaka 2015, Innocent Melleck amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Melleck ambaye katika uchaguzi huo mwaka 2015 alichuana vikali na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) amecharangwa mapanga maeneo ya mwili eneo la kichwani, mabegani, mgongoni na kwenye mguu wa kushoto.

Akizungumza kwa taabu na Mwananchi leo Jumatatu Septemba 9,2019 amesema tukio hilo lilitokea usiku saa 5, Alhamisi iliyopita ya Septemba 5, 2019 akiwa jirani na nyumbani kwake Goba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

"Vijana wawili wakiwa na pikipiki walikuwa jirani na nyumbani kwangu, walionekana kama kuhitaji msaada, mmoja akasogea kwenye gari yangu akagonga," anasimulia.

Anasema alishusha kioo ili kumsikiliza, lakini kabla ya kuzungumza naye chochote alimfunika usoni na kitambaa na akapoteza fahamu.

"Sikujua kilichoendelea hadi nilipozinduka nikiwa hospitali ya Kairuki ambapo niliambiwa nilitupwa njia panda ya Kawe, nilisaidiwa na madereva bodaboda ambao walitoa taarifa Polisi Kawe," anasema

Anasema waliomvamia walichukua fedha Sh11 milioni ambazo alikuwa nazo kwenye gari, flash mbili, laptop na simu mbili za mkononi.

"Nafikiri walikuwa na nia ya kuniua, kwani walinicharanga mapanga kichwani nikiwa nimepoteza fahamu, kwenye gari kulikuwa na vitu vingine vya thamani lakini hawakuchukua zaidi ya flash mbili, laptop, simu mbili za mkononi na fedha," anasema

Anasema tukio hilo limepeleka kuogopa kurejea nyumbani hata baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ambako amefanyiwa upasuaji mkubwa uliochukua saa nane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu alipoulizwa amesema wakati tukio linatokea alikuwa Shinyanga kikazi.

"Anayepaswa kunipa taarifa ni OCD ambaye nimejaribu kuwasiliana naye bahati mbaya yuko katika shughuli za mitihani," amesema Kamanda Taibu.

Mkuu wa Upelelezi Kawe, Alfred Lugamara amesema tukio hilo limeripotiwa polisi Kawe na upelelezi bado unaendelea.

"Mtu mmoja anaitwa Innocent Shirima (Melleck), kesi yake bado inachunguzwa, sababu mwenyewe hakuweza kutoa maelezo yoyote kutokana na hali yake kiafya, alichukuliwa Goba akatelekezwa njia panda ya kawe akiwa amejeruhiwa," alisema Alfred.

-Mwananchi-
Inatuhusu nini sissi kwanini hakufa
 
Pole sana. Maeneo ya Goba na Mbezi sasa hivi siyo salama sana majambazi ni wengi hada wakijua una pesa na hasa kama umetokea bank watakufuata kokote hata mpaka kanisani. Huyu walisha muotea ndiyo maana wakamfuata
 
Hili ni wazi ni tukio la ujambazi ingawa mtoa mada anataka liangaliwe kwa mlengo wa kisiasa. Lakini na muathirika naye alijisahau mno mil 11 anazunguka nazo kwenye gari mpaka saa 5 usiku! Huyu ina maana jamaa wameshinda naye mchana mzima wakimfuatilia nyendo zake

Back
Top Bottom