Kada CCM avamiwa, acharangwa mapanga Dar

Kada CCM avamiwa, acharangwa mapanga Dar

Inawezekana kwa makusudi mmeamua kupoteza maana halisi ya wasiojulikana. Kwanini vibaka muwaite watu wasiojulikana!
Kada wa chama tawala, chama dume hawezipigwa mapanga kisiasa awamu hii!
 

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa mgombea ubunge wa Vunjo kupitia chama hicho mwaka 2015, Innocent Melleck amenusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Melleck ambaye katika uchaguzi huo mwaka 2015 alichuana vikali na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) amecharangwa mapanga maeneo ya mwili eneo la kichwani, mabegani, mgongoni na kwenye mguu wa kushoto.

Akizungumza kwa taabu na Mwananchi leo Jumatatu Septemba 9,2019 amesema tukio hilo lilitokea usiku saa 5, Alhamisi iliyopita ya Septemba 5, 2019 akiwa jirani na nyumbani kwake Goba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

"Vijana wawili wakiwa na pikipiki walikuwa jirani na nyumbani kwangu, walionekana kama kuhitaji msaada, mmoja akasogea kwenye gari yangu akagonga," anasimulia.

Anasema alishusha kioo ili kumsikiliza, lakini kabla ya kuzungumza naye chochote alimfunika usoni na kitambaa na akapoteza fahamu.

"Sikujua kilichoendelea hadi nilipozinduka nikiwa hospitali ya Kairuki ambapo niliambiwa nilitupwa njia panda ya Kawe, nilisaidiwa na madereva bodaboda ambao walitoa taarifa Polisi Kawe," anasema

Anasema waliomvamia walichukua fedha Sh11 milioni ambazo alikuwa nazo kwenye gari, flash mbili, laptop na simu mbili za mkononi.

"Nafikiri walikuwa na nia ya kuniua, kwani walinicharanga mapanga kichwani nikiwa nimepoteza fahamu, kwenye gari kulikuwa na vitu vingine vya thamani lakini hawakuchukua zaidi ya flash mbili, laptop, simu mbili za mkononi na fedha," anasema

Anasema tukio hilo limepeleka kuogopa kurejea nyumbani hata baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ambako amefanyiwa upasuaji mkubwa uliochukua saa nane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu alipoulizwa amesema wakati tukio linatokea alikuwa Shinyanga kikazi.

"Anayepaswa kunipa taarifa ni OCD ambaye nimejaribu kuwasiliana naye bahati mbaya yuko katika shughuli za mitihani," amesema Kamanda Taibu.

Mkuu wa Upelelezi Kawe, Alfred Lugamara amesema tukio hilo limeripotiwa polisi Kawe na upelelezi bado unaendelea.

"Mtu mmoja anaitwa Innocent Shirima (Melleck), kesi yake bado inachunguzwa, sababu mwenyewe hakuweza kutoa maelezo yoyote kutokana na hali yake kiafya, alichukuliwa Goba akatelekezwa njia panda ya kawe akiwa amejeruhiwa," alisema Alfred.


-Mwananchi-
Kama ni mccm powa tu
 
  • Kicheko
Reactions: BAK
Mil 11 anatembea nazo kwenye gari, saa 5 usiku, alafu unagongewa dirisha la gari unafungua. Jamani, security alerts ndogo ndogo mjue zitawasaidia sana maishani..!!
Kujiamini kwingi halafu watu hawajui sio wote walioko karibu yao ni watu wazuri naamini hii ni inside job!
 
Hao waliomvamia watakuwa Chadema tu , Dar hakuna vibaka , mambosasa kaisafisha kabisa !
 
Hilo ni jiji la kifutu imekuaje tena wakati ni juzi tu hapa anamwagiwa misifa kua jiji liko shwari kabisa!
Mkuu walisema wanaimarisha ulinzi kipindi cha mkutano,kwasababu umeisha nadhani shughuli za wahuni zemerejea.
 
Mil 11 anatembea nazo kwenye gari, saa 5 usiku, alafu unagongewa dirisha la gari unafungua. Jamani, security alerts ndogo ndogo mjue zitawasaidia sana maishani..!!
Hata mimi nimewaza sana hili jambo..
Yani unatembea na milioni 11 usiku halafu unawakuta watu usiowafahamu kwenye boda boda unasimama hovyo tu bila kuwa na tahadhari yoyote..
Mimi hata nikute mtu kafa au mahututi njiani wakati nina huo mzigo wala sisimami..
Sanasana ntaingia home ntaweka mzigo ndani kisha nitoke tena na mtu mwingine kwenda kucheki nini kinaendelea...
 
Back
Top Bottom