Kada CCM akufuru usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada CCM akufuru usiku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JuaKali, Nov 15, 2008.

 1. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mgombea mmoja wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi wa CCM taifa amemwaga `lazi` kuanzia mchana wa jana hadi usiku wa kuamkia leo baada ya kuwalisha misosi wajumbe kibao wa jumuiya hiyo wa kata za Dar na kisha kuwatembezea takrima ya mshiko kabla ya kuwasafirisha kwa mabasi yake matatu.

  Kada huyo (jina tunalo), amefanya mambo hayo yaliyo kinyume na taratibu za chama chake kwenye kumbi maarufu mbili za pale Chang`ombe na Msasani, kabla ya wengine kuendelea kunufaika na kampeni zake hizo pembezoni mwa bahari ya Hindi.

  Taarifa kutoka kwa baadhi ya wajumbe waliojichana misosi ya mgombea huyo na kudai kuwa nao wamebahatika kulamba `mshiko` wake wa sh. 5,000 kwa kila mmoja pale Chang`ombe na Sh. 10,000 kwa kila mmoja aliyekuwepo Msasani, zinadai kuwa mgombea huyo alijinadi kuwa ana pesa za kutosha na hivyo wajumbe wanapaswa kumchagua bila kusita.

  ``Alitulisha, akatunywesha, akatupa pesa zake, kisha akadai kuwa tumchague kwa sababu yeye ana fedha za kutosha... kwamba eti, nia yake ni kukisaidia chama na wala si kutumia mgongo wa uongozi ili kujikwamua kiuchumi kama walivyo wagombeaji wengine wa nafasi yake,`` akadai mmoja wa wajumbe hao.

  ``Binafsi, sikufurahishwa na jambo hili kwa sababu linakwenda kinyume na taratibu halali za CCM. Lakini nilivutiwa na vyakula vyake na pia pesa zake na ndio maana nikavichangamkia ... lakini sidhani kama wagombea wa aina hii wanaweza kuijenga CCM,`` akadai mjumbe mwingine ambaye kama alivyokuwa mwenzie, kamwe hakuwa tayari kujitaja jina wala kata anayotoka.

  Mtiririko wa tukio lenyewe ulikuwa hivi:Mishale ya saa sita mchana jana, mgombea huyo aliwachukua wajumbe zaidi ya 30 watokao katika maeneo tofauti ya wilaya tatu za Dar na kuwapelea katika ukumbi huo wa Chang`ombe.

  Kufika hapo, hakuna walichofanya wajumbe hao zaidi ya kujichana misosi ya nguvu pamoja na kunywa watakavyo kabla ya kupewa kadi ndogo (kama za baishara), zenye kumnadi mgombea huyo.

  Baada ya zoezi hilo, mgombea huyo akagawa Sh. 5,000 kwa kila aliyehudhuria.

  Ilipofika mishale ya saa 10:00, mgombea huyo akatumia mabasi madogo matatu anayomiliki, kuwachukua wajumbe hao na kwenda nao kwenye jumba lake moja la kifahari ili wajumbe wajionee jinsi mambo yake yalivyo `supa`.

  Katika kuonyesha minjonjo zaidi, mgombea huyo akaingia ndani ya jumba lake hilo na kuwaacha wajumbe hao nje kabla ya kutoka na gari lake la bei mbaya, shangingi aina ya Toyota VX (namba za gari tunazo).

  Hiyo haitoshi, ilipokaribia mishale ya saa 12:00 jioni, mgombea huyo akaongozana na wajumbe hadi kwenye sehemu yake moja ya biashara pale Kariakoo Jijini na kuwaonyesha mali kibao alizo nazo.

  Baada ya hapo, msafara wa wajumbe hao na wapambe wengine kadhaa ukaelekea katika ukumbi mmoja uliopo Msasani ambako huko wakajichana kwa misosi na vinywaji kuliendelea.

  Cha kushangaza, baadhi ya wajumbe waliohudhuria wakaona wawapigie simu wenzao ili nao wafike ukumbini na kufaidi, jambo ambalo lilifanyika kwani kadri muda ulivyokwenda ndivyo idadi ya watu ilivyoongezeka.

  Mwishoni mwa kula na kunywa huko kulikogharimiwa kwa kila senti na mgombea huyo, kila aliyekuwepo akapewa tena Sh. 10,000.

  Aidha, kadi za kumpigia debe mgombea zikasambazwa tena kwa wale waliozikosa Chang`ombe, huku ikitolewa ahadi ya kupata mshiko mkubwa zaidi endapo atatokea mgombea mwingine atakayetoa pesa zaidi ya dau hilo la elfu kumi-kumi.

  Baadaye, mgombea huyo na wajumbe wengine kadhaa wanadaiwa kwenda kumalizia kujichana kwao kwenye fukwe za bahari ya Hindi, katika mahala kuliko na klabu moja maarufu.

  Wakati hayo yakifanyika, hivi karibuni, CCM kupitia kikao chake cha Kamati Kuu ya Taifa kilichokutana mjini Dodoma kuanzia tarehe 8 na 9 mwezi huu, chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kiliazimia kuwa wagombea wote hawataruhusiwa kutumia vipeperushi wakati wa kampeni isipokuwa asubuhi ya siku ya uchaguzi.

  Pia kikao hicho kilikataza matumizi ya fedha ambayo huashiria vitendo vya takrima na rushwa.

  Alipoulizwa juu ya suala hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wilaya ya Kinondoni, Bi. Angela Kiziga alisema alikuwa na udhuru , hivyo hakuweza kutoa maoni yake.

  Mgombea anayedaiwa kufanya hivyo alipoulizwa, alikana na kudai kuwa hakuwalisha watu vyakula, vinywaji wala kutoa pesa na kadi za kujinadi.
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sikilza mleta mada hii,

  Hapa ni JF, tunaweka mambo wazi. Kutuambia jina tunalo, namba za gari tunazo na vifumbo vingi ni uswahili na umbea ama udaku. Kama ulitaka kutuletea hoja ili tuijadili basi kuwa mkweli na muwazi acha mambo na maneno ya jikoni.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  JF imejijengea heshima ya ukweli na uwazi. Kama hutaki kututajia jina na mahali. Nakushauri peleka umbea wako kwanye magazeti ya udaku na sio hapa JF.

  Kwa vile na wewe ni mmoja wa waliopokea takrima ya mheshimiwa huyo kwa sababu ya kuendekeza njaa, mshauri kama nafasi anayogombea wazazi ni uenyekiti, mshauri asipoteze vijisenti vyake bure. Mhe. Mkono alishamaliza kazi tangu matawili walikotoka na ndiye anayegharimia mkutano huo mkuu kwa kukikopesha chama,
   
 4. K

  Kakulwa Senior Member

  #4
  Nov 15, 2008
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  juakali,kipya kiko wapi hapo mkuu?
  Hayo mambo ya kugawa pilau na kanga mbona ya kawaida sana ccm huko.
   
 5. F

  Fataki Senior Member

  #5
  Nov 15, 2008
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  HUO NI UDAKU MTUPU. PELEKA UDAKU HUO RAI NA MAGAZETI ALIYOYAANZISHA KARAMAGI NA WENZAKE YA TAIFA, UMMA, NYUNDO, TAZAMA n.k. Wewe umeshiriki katika ulaji mchafu halafu unajitoa na kuripoti kuhusu walaji uchafu wenzako. Nani atakuamini? You have lost moral authority to tell us anything!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Typical udaku, wasiliana na Shigongo ur in wrong place, JF hutuintertain mambo haya Jina tunalo, namba za gari tunazo jina tunalo, uswahili na umbea mmhhh sisi huwa tuna taja kila kitu hadharani....

  pole sana
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu tupo ukurasa mmoja hapa, naona kwenye huu msafara kuna makenge pia yanajichomeka sometimes yaone tutasema nini, wakuu wote mliomjibu saafi sana.
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Jina lako halisi lipo kapuni, lakini bado tu macho yamekutoka pima kwa woga,unaogopa kutaj jina la mgombea.
  Huo si woga wa kawaida, huu ni woga aina mpya kabisa.
  Yaani woga wa kujiogopa mwenyewe.

  Kam si woga, basi ni habari isiyo na kichwa wala miguu
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kanuni ya kutotaja majina inakwenda hivi:

  a. Kutotaja jina, cheo, au wadhifa wa chanzo cha habari nyeti ili kulinda soource hiyo for future use au kulinda ajira ya mtu pale ambapo kumtaja kutamharibia kazi yake, au kumletea matatizo mengine kazini au katika kupata ajira huko mbeleni.

  b. Kutotaja jina la watoto wadogo (chini ya umri wa kisheria) wanapofanyiwa vitendo vibaya au wanaposhtakiwa kwa makosa ya kihalifu. Lengo ni kuwalinda.

  c. Baadhi ya sehemu hawataji majina ya victims wa vitendo vya ubakaji lengo ni hilo hilo la kuwalinda.

  d. Kutotaja jina pale ambapo haitakiwi kisheria kwa mfano outing an intelligence officer. Katika TAnzania ukiondoa Mkurugenzi wa Ujasusi, maafisa wengine wa TISS hawatakiwi kutambulishwa hadharani kwa mujibu wa sheria. Ni kama ile issue ya Valerie Plamer

  Kwangu hayo ndiyo mazingira ya kuangalia. Inapokuja kwenye suala la habari inayomhusu mtu fulani haina maana yoyote ya kuficha majina ya wahusika wenyewe wa habari kama haiko katika maeneo hayo manne hapo juu. So, I totally agree with those who have criticized hiyo article.
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Mkuu.. jamaa katoa hii habari kwenye gazeti la udaku.... alasiri. Labda kafanya kosa la kutokuweka source ya habari. By the way hata kama huyo mjumbe kafanya hivyo si anafuata nyayo za bosi wake Kikwete? Kwani Kikwete si anachaguliwa kwenye mkutano wa CCM kwa kutembeza fedha???
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Katembeza pesa akijua Baba wa Taifa hayupo mtu ambaye alisema akasikilizwa wengine akina Warioba wanasema lakini impact bado kiasi .Anasambaza mapesa akiwa na uhakika kwamba si JK wala Makamba aliye safi katika hili so anafanya atakavyo na mwishoni atachaguliwa .Kumficha jina ina maana mleta habari anataka jamaa achaguliwe ndipo amtaje hapo atakuwa hajasaidia Nchi hii .Atajwe sasa amulikwe leo na maamuzi yafanyike kesho kwenye kura .
   
 12. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #12
  Nov 16, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145

  Sasa habari kama hizi sisi hatuzitaki hapa JF. Kwani sisi hatuwezi kusoma huo udaku kwenye hayo magazeti hadi atuletee hapa?
   
Loading...