"Kachero" na Hatima ya CCM 2020

CC kwa Balozi Mombo
CC kwa Balozi Nchimbi
 
Chakaza

Hizi ni fikra zangu juu ya JPM na CCM.

Hana uzoefu wa kuongoza chama cha siasa kama CCM, achilia mbali TADEA. Mambo makubwa matatu yanamsumbua kuhusu CCM.

Kwanza ni uwezo wa kuwa na ushawishi na kumudu nafasi ya uenyekiti bila kutumia nguvu. Hakujiandaa kuwa mwenyekiti. Unapokuwa mwanaCCM unayegombania nafasi ya uRais tayari unakua umeandaa katibu mkuu wako, makamu, uenezi, n.k. Tayari unajiandaa kuwa mwenyekiti wa chama.

JPM hakujiandaa kwenye hili. Uenyekiti umemkuta na sasa hajui yupi amuweke wapi na yupi amtupe. Huyo atakayemtupa, je atamfanyia fitna?

Mwisho wa siku anakosa ushawishi na kubakia na kina Bashite, Polepole, na kaliba hiyo ambayo haina ushawishi ndani ya chama zaidi ya kuonekana vituko.

JPM kwa sababu ana hofu na hana imani na wanaCCM kuhofia kumzunguka amebakiza silaha moja tu kuimarisha uenyekiti wake - Dola.

Kwa sasa CCM ipo chini ya dola si juu ya dola kama zamani ambapo katibu mkuu au mjumbe wa NEC ana nguvu kuliko Kamanda Siro. Meza imegeuka na wanaCCM wamekuwa wapole na hawana furaha ukiacha wale wanaokula sasa.

Pili muundo wa serikali ulioasisiwa na Nyerere umeifanya CCM kuwa kubwa kuliko nchi. Katika uteuzi wowote ule idara zote muhimu lazima zishikwe na chama na si mtu mwingine.

Enzi hizo CCM ndiyo Tanzania, sasa Tanzania ndiyo CCM-Mwenyekiti.

Tofauti ni kwamba CCM ndiyo walitoa viongozi wa idara zote muhimu. Sasa idara muhimu zinapewa watu wasiokuwa hata na uCCM lakini wanapaswa kuiabudu CCM-Mwenyekiti. WanaCCM wanaona wanabaguliwa kwa kulishwa makombo ya teuzi.

Tatu na mwisho ni hofu juu ya upinzani hususani CHADEMA. Iwapo CHADEMA hakitaishiwa nguvu mpaka 2020 kitampa shida JPM.

Shida ni Lowassa mwingine kujitoa kwenye chama. Kama Lowassa ametoka na sisi tuliobaki hatuoni faida ya kuwa CCM kwa nini tubaki?

Hivyo ni "hekima" na "busara" kwa Mwenyekiti kutumia nguvu kuua upinzani ili iwapo kuna mwanaCCM mwenye ushawishi atakapotaka kutoka akose pakwenda.

Kwa hiyo leo ikionekana Membe ni tishio ataandamwa na kufanywa mfano ili mwingine asiige. Tanzania iwe CCM-Mwenyekiti kwa kupenda au la!

Kuna kiza mbele.

cc JokaKuu Mchambuzi Mag3
 
Usicheze na nguvu ya Rais. Kile kiti mtu akishakaa pale ndio ameshakaa, anakula miaka 10 yake. Mtu ana state apparatus zote unamzuia vipi ndani ya Chama asipite 2020. Huyo Kachero anaweza kuwekwa house arrest mpaka uchaguzi ukapita 2020nna hakuna cha kufanya zaidi tutasikia tetesi kwenye Magazeti na kwa Mange kimambi basi. Labda wapinzani wa nje ila sio wa ndani ya Chama.
 
Kweli, ingawa nae ngosha kawaamisha wengi sana waliopo ikulu kawapeleka huko mikoani, nae anajua kwenye system kuna watu wa watu ndio maana ana tibua tibua
System ni system tu hawawezi kuona nchi yao inaharibika wakakubali iharibike haiwezekani. Muhimu na kubwa kuliko yote ni ustawi wa nchi yetu akionekana mmoja anaharibu misingi aliyeweka nyerere asemwe mpaka asimame kwenye msitari sahihi
 
mwanzoni mwa utawala wake Mkuu alikuwa na sapoti fln kutoka kwa wapinzani na umma kuliko hata ccm yenyewe, kwa u -turn aliyoipiga anabaki no man's land!
 
mwanzoni mwa utawala wake Mkuu alikuwa na sapoti fln kutoka kwa wapinzani na umma kuliko hata ccm yenyewe, kwa u -turn aliyoipiga anabaki no man's land!
 
Wale waliomo ndani ya viroba wametambuliwa jamani?..nauliza nimeamka usingizini tu.

Habeeb Marhan
 
Mtoa mada umejitahidi kuuchimba ukweli uliyokatika kisiwa kisichofikika. Kuna mengi yanayoendelea ktk harakati za kumtoa aliyepo kitini. Kachero anacheza kwa nafasi yake lakini pia wale wengine hawajazima mitambo Yao pia.
Kwa ufupi tu, mkulu amezungukwa na maadui kila kona. Hili analijua fika na ndo maana kuna wakati anajikuta akipiga kampeni kwenye ziara za uongozi.
Mwaka 2019, utakuwa mwaka wenye pilikapilika nyingi za kisiasa ndani ya chama kikongwe cha Tanzania, pilikapilika hizi zitaendana na kuchafuana. Aliyeshika mpini amejiandaa vyema kutumia nafasi yake kudhoofisha wote waliojitokeza kutoa ushindani msimu uliopita na kwa hakika hata hawa wachache waliobaki kwenye teuzi, watalia na kusaga meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe mwizi tu na fisadi hana lolote wala hana mbinu km tunavyojiaminisha

MTU hatar ccm alikuwa ni mzee lowasa tu

Hata kikwete sio mzee wa mipango km lowasa

Membe hana mbinu yeyote hata km angehudumu usalama wa taifa miaka mia

Magu nae atakuwa wa hovyo km ataruhusu kuyumbishwa na membe

Japo magufuli na membe wote ni viongoz wabovu

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
kwa magufuli kila goti litapigwa wakuu. kama kuna mtu amekaa mkao anajidanganya kwamba atampinga 2020 ajue ataishia kama anavyoishia Mr. zero sasa hivi.
 
Huyu alieleta thread hii naona kama bado anajidanganya...mkuu mfarakano uliotokea 2015 hauji kutokea tena kamwe katika chama hichi subirin 2020 mchapwe tena

Sent using Jamii Forums mobile app


wewe unona ni mfarakano tu... wa watu wawili..

ukweli mwenyekiti wa ccm alikuwa hajajiandaa kuongoza chama... sasa ndani ya chama upo mgongano wa kimaslahi maana wapo wanao athirika na utendaji wa mkuu name wananguvu ndani ya chama... pia wapo wanaomkubali mwenyekiti...
 
Nimeona picha polepole ndio kampokea Naibu Balozi wa Marekani. Kiprotocal balozi ni mtu mkubwa sana nilitegemea akutane na Katibu mkuu kama hayupo basi makatibu wakuu wasaidizi/naibu mmojawapo angekutana nae.

Badala yake kakutana na mtu wa propaganda kwa lugha nyepesi Pole pole ndio Ag. KM.

Swali la kujiulize katibu mkuu yupo wapi? Naibu katibu mkuu bara au visiwani wko wapi?

I guess kuna shida ndio maana hawapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…