Kaburu wa kampuni ya uranium katika kashfa nzito ya ubakaji; sheria zinasemaje?

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Messages
1,670
Points
1,195

Felixonfellix

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2010
1,670 1,195
Kaburu wa kampuni ya uranium katika kashfa nzito ya ubakaji

Mwandishi Wetu
Ruvuma
15 Jun 2011
Toleo na 190
  • Abaka visichana vidogo wilayani Namtumbo
  • DC akiri kwamba wageni hao ni hatari
  • Wanavijiji wapoteza imani na vyombo vya dola
WASICHANA katika Kijiji cha Likuyu, Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, hawana mtetezi wala mlinzi wa usalama wao kutokana na udhalilishaji wa kijinsia wanaofanyiwa na Mzungu, raia wa Afrika Kusini.
Udhalilishaji wanaofanyiwa wasichana kijijini hapo, wakiwa na umri wa chini ya miaka 18, ni pamoja na kubakwa na kutendewa kinyume cha maumbile, lakini hadi leo hii hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa pamoja na baadhi ya wasichana hao kulalamika kwenye uongozi wa kata.
Miongoni mwa wasichana hao wapo wawili ambao walitoa maelezo yao kwa maandishi, mmoja akifanikiwa kumtoroka Mzungu mbakaji, lakini wa pili alijikuta akifanyiwa unyama kwa kulazimishwa kufanya ngono kinyume cha maumbile. Juhudi zao kupata msaada ziligonga mwamba, na hivyo kuamua kutoa kilio chao kupitia Raia Mwema.
Uchunguzi wa hospitali

Uchunguzi wa hospitali kwa mmoja wa wasichana waliotendewa unyama huo, uliofanyika katika Zahanati ya Likuyu Seka, unathibitisha kuwepo kwa michubuko sehemu za siri za msichana huyo pamoja na kuwepo majimaji yaliyochanganyika na damu.
Mganga aliyemchunguza msichana huyo alilithibitishia Raia Mwema kijijini hapo kuwa yule binti aliingiliwa kwa nguvu na kinyume cha maumbile.
Uchunguzi huo ulifanyika baada ya Afisa Mtendaji, Kata ya Likuyu Seka, kumwandikia barua Mganga Mguu, Zahanati ya Likuyu Seka, akimtaka kuwafanyia uchunguzi wa kiafya wasichana wawili waliobakwa.
“Vijana hao hapo juu wana matatizo ya kiafya mara baada ya kufanyiwa vibaya kimapenzi kinyume na maumbili na Mzungu ambaye yuko kwenye kampuni ya Mantra. Naomba mara baada ya kuwachunguza nipewe taarifa yao,” inasema barua hiyo.
“Sehemu ya mwisho ya maelezo ya msichana huyo inasema: “Tangu siku ile sijisikii vizuri na nikaenda kupimwa mimba, nikaambiwa nina mimba. Naomba serikali inisaidie kwa hili, umri wangu ni miaka (17) kumi na saba.”

Katika maelezo yao kwa Afisa Mtendaji, Kata ya Likuyu Seka, waliyoyatoa kwa maandishi Machi 28, mwaka huu, wasichana wawili waliofanyiwa unyama huo wanabainisha kuwa katika kufanikisha kuwapata wasichana, kaburu huyo humtumia mzee mmoja fundi seremala kijijini hapo (jina tunalo).
Serikali inasemaje

Mzungu anayetuhumiwa kuhusika na unyama huo ni raia wa Afrika Kusini (jina tunalo) mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 50, na kwa sasa ni mmoja wa mameneja katika kampuni inayotafiti madini ya uranium kwenye mbuga ya Seleous upande wa Wilaya ya Namtumbo.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Zaveli Maketa, alisema hana taarifa zozote kuhusu unyama huo lakini wakati huo huo akibainisha kuwa Wazungu wale ni hatari, anasema:

“Taarifa hizo sina, tena tarehe moja nilikuwa nasuluhisha mgogoro wa wafanyakazi wa Sogea (Kampuni nayojenga Barabara ya Songea-Namtumbo kwa kiwango cha lami) waligoma kufanyakazi. Hizo sina kabisa, ningekuwa nazo ningetuma vyombo vyangu vya dola. Nashukuru sana umenipa pa kuanzia, na kesho nina ziara huko nitafuatilia. Tukithibitisha tunamfukuza. Hawa watu hatari sana, kesho nitakujulisha.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda, naye alieleza kutokuwa na taarifa zozote kuhusiana na kuwepo kwa vitendo hivyo, lakini akabainisha kwamba huo ni ukiukaji wa sheria na hao Wazungu hawako juu ya sheria.
“Kama yupo ni vitendo vya ukiukaji sheria na hao hawako juu ya sheria. Nitaongea na OCD Namtumbo afuatilie na tutachukua hatua,” anasema Kamanda Kamhanda.
Naye Afisa Upelelezi Wilaya ya Namtumbo aliyejitambulisha kwa jina moja la Justine, akifuatilia sakata hilo baada ya kupata maagizo kutoka kwa mkuu wake wakazi, alipiga simu Raia Mwema akisema hawakuwa na taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa unyama huo, na akabainisha kuwa yawezekana waathirika hao walitoa taarifa kwa afisa mtendaji wa kijiji kutokana na umbali uliopo kutoka kijijini hapo hadi mjini Namtumbo kilipo kituo cha polisi.
Uchunguzi wa Raia Mwema kwa takribani mwezi mmoja sasa kuhusu ukweli wa kuwepo kwa uhalifu huo umebaini kuwa wananchi katika kata hiyo ya Likuyu Seka hawana imani na viongozi wao wa serikali pamoja na vyombo vyake vya ulinzi na usalama.
“Hatukutoa taarifa wilayani kwa sababu wakifahamu mapema watawasiliana na Wazungu wa Mantra halafu wanazima kesi,” anasema mwananchi mmoja kijijini hapo.
Mbali ya tukio lililohusu wasichana hao wawili, inaelezwa kuwa wapo wasichana wengi tu wenye kudhalilishwa, wakilazimishwa kufanya ngono na wageni hao ikiwemo kinyume na maumbile, lakini hazitolewi taarifa kutokana na hofu ya kudhalilika pale itakapofahamika na vile vile kukosa imani na viongozi wa siasa, serikali na jeshi la polisi.
Mzungu anafanikiwaje katika mchezo huo, binti muathirika anasimulia;

“Siku moja mwezi wa pili, siku ya Jumapili, niliitwa na Mzee ….. (anamtaja) ambaye anafanya kazi ya useremala, aliniambia niende kwake. Nilipokwenda aliniuliza; unataka kazi? Nikajibu naitaka, baada ya hapo aliniambia niende uwanja wa ndege Kalulu. Nikaenda nikitanguzana na yeye hadi huko. Baadaye alinionyesha eneo la kwenda kulisafisha na hela atanipa.
“Nilimwambia nikachukue jembe, akasema subiri kwanza. Baadaye gari lilitokea, likasimama tulipo; kisha Mzungu akateremka. Mzee huyo na Mzungu wakawa wanaongea Kiingereza. Baada ya hapo niliambiwa nipande gari kuelekea mwisho wa uwanja wa ndege.
“Kabla ya mwisho wa uwanja, Mzee aliteremka na kuniacha mimi na Mzungu, kisha mzee huyo aliniambia mtanguzane na Mzungu hadi njia ya zamani ya kurudi kwenye nyumba za Kalulu. Kabla ya kufika huko, Mzungu akapeleka gari porini na kulisimamisha na kunifungulia mlango niliko mimi.
“Akawa ananiambia kwa Kiingereza lakini nilikuwa sielewi. Nikawa nakimbia naye akawa ananikimbiza, nikaanguka kisha akanishika na kunifanyia suala la ndoa kinyume na maumbile. Baada ya hapo, nilipanda kwenye gari hadi alipo mzee huyo; naye akapanda kwenye gari, nami nikashuka. Yule Mzungu alimpa Yule mzee Sh. 50,000. Mzee yule aliniambia baadaye niende nyumbani kwake. Sikuweza kwenda kwa sababu nilikuwa naumwa. Wazazi waliponiuliza juu ya homa yangu nikawa nimeficha. Hali ilivyozidi kuwa mbaya nikamwambia mama mdogo.”

Kijiji cha Likuyu Seka kipo umbali wa takribani Kilometa 28 kutoka Namtumbo mjini yalipo makao makuu ya wilaya hiyo pamoja na Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya, wakati makazi ya kampuni hiyo ya Mantra ni kilometa takribani 50 kutoka kwenye lango kuu kuingilia kwenye hifadhi hiyo ya Selous upande wa Namtumbo ambapo kijiji chao cha kwanza watokapo kwenye makazi yao, ni Likuyu Seka.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
3,057
Points
1,500

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2009
3,057 1,500
Kwanza la kujiuliza hao anaowabaka huwapata wapi? Huwakamata barabarani au vipi?

Ikiwa munao uhakika kwa nini hamumkamati mukampa kichapo? Oooooops samahani kwa kwenda nje ya sheria!
 

Forum statistics

Threads 1,353,230
Members 518,297
Posts 33,075,371
Top