Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 857
- 926
Habari za wakati huu.
Nimeona nichangie jambo moja kuhusu msamiati wa kipagani ulioingizwa katika midomo ya baadhi ya wafuasi wa dini za kiislamu na kinaswara (kikristo) kwa kusema kuwa kaburi ni nyumba au makazi ya milele!
Mara nyingi maneno haya yamekuwa yakitolewa na watangazaji washereheshaji kupitia vyombo vya habari ya kwamba marehemu anaenda kupumzishwa katika makazi yake ya milele.
Sio sana bali sijawahi kusikia kiongozi wa dini ya kiislamu au ya kinaswara akitamka maneno haya!
Na hii ni kutokana na ukweli ya kwamba kulingana na imani ya kiislamu na kinaswara kaburi sio makazi ya milele kwa kuwa dini zote mbili hizi zinaamini kwa sura tafautitafauti habari ya wafu kufufuliwa siku ya qiyama (siku ya mwisho).
Wapagani wasioamini kuwa wafu watafufuliwa siku ya mwisho na kulipwa kwa yale waliyoyafanya duniani ndio huona kuwa mtu anapozikwa kaburini amewekwa kwenye makazi ya milele.
Kwa mujibu wa Imani ya kiislamu makazi ya milele ni pepo
(mabustani mazuri) iliyoandaliwa watu wema baada ya kufufuliwa na kuhukumiwa siku ya qiyama au moto ulioandaliwa kwa watu waovu ambao pia watauingia baada ya kufufuliwa na kuhukumiwa siku ya qiyama kila mmoja kulingana na uovu wake alioufanya duniani.
Mara chache ambazo nimekuwa nikiangalia maziko ya manaswara (wakristo) kupitia vyombo vya habari nimekuwa nikisikia viongozi wa dini hiyo pia wakihubiri kuwa marehemu watafufuliwa siku ya mwisho.
Kwahiyo kwa maneno haya inabaki wazi kwamba habari ya kaburi kuwa nyumba au makazi ya milele ni Imani ya kibagani inayopenyezwa kidogokidogo ndani ya wafuasi wa dini za kiislamu na kinaswara kupitia wanahabari ambao mara nyingi hawana elimu ya kutosha kuhusu mambo ya Imani za dini kwa sababu wapagani hawaamini kama watafufuliwa siku ya mwisho.
Naomba kuwasilisha.