Kaburi la Sheikh Yahya lavunjwa Dar

Kaburi la Sheikh Yahya lavunjwa Dar

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,695
Reaction score
59,198
kaburi.jpg

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiangalia kaburi la aliyekuwa Mnajimu maarufu Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein linalodaiwa kubomolewa na mgambo wa jiji usiku wa kuamkia jana katika Makaburi ya Muhimbili. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Watu wasiojulikana wamevunja makaburi, likiwamo la marehemu Sheikh Yahya Hussein lililopo jirani na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mtoto wa Sheikh Yahya, Hassan Yahya Hussein alisema ameambiwa kwamba kaburi la baba yake na mengine yamevunjwa na askari wa jiji wanaoendesha bomoabomoa katika eneo hilo.

Alisema mbali na kaburi la Shekh Yahya, pia watu hao walivunja kaburi la Sheikh Kassim Bin Juma lililipo jirani na kaburi la baba yake.

"Kwa kweli hadi sasa sielewi kwa nini askari hao wamefanya kitendo hicho," alisema Hussein.

Alisema Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba ametuma ujumbe kwenda kwa meya na viongozi wa Manispaa ya Ilala.
Akizungumzia suala hilo kwa simu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alisema yeye na viongozi wa Manispaa ya Ilala na wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) walitembelea eneo hilo.

Alisema walichobaini ni kwamba makaburi hayo hayakuvunjwa na tingatinga la jiji, bali uchunguzi umeonyesha kwamba yamevunjwa na watu.
Alisema Serikali imeiagiza Manispaa ya Ilala, Bakwata na familia kuandaa ujenzi wa makaburi hayo ili yaweze kuwa kama mwanzo.

Alisema makaburi hayo yamevunjwa na watu ambao wanachukizwa na bomoa bomoa inayoendelea jiji zima la Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema amepata taarifa za tukio hilo kutoka kwa waandishi wa habari.

"Tuwe makini na tukio hilo kwa sababu wanaovunjiwa vibanda hawafurahishwi, hivyo wanaweza kutumia mwanya huo kufanya hujuma zozote ili ionekane askari wa jiji wamefanya kitendo hicho," alisema.

Source:Mwananchi
 
Mh wahusika wamefika mbali....ya nin kwenda kumsumbua marehemu...
 
shehe yahya ni Mnajimu wa Ikulu ni lazima watawala walalamike hata kaburi lake linapo guswa!!
 
walikosa mahali pa kumzika wakaja kumzika mahali ambapo ni kijiwe cha bangi cha wahuni?, wasilalamike sana, hakushahili kuzikwa swhwmu isiyo na heshma kama hiyo.
 
walikosa mahali pa kumzika wakaja kumzika mahali ambapo ni kijiwe cha bangi cha wahuni?, wasilalamike sana, hakushahili kuzikwa swhwmu isiyo na heshma kama hiyo.

na ukizingatia alikua mtu mashuhuri africa mashariki nzima
 
Kwa nini hawakwenda kuzikwa vijijini kwao!mjini sii sehemu ya makaburi
 
Wangemchoma tu moto halafu wahifadhi majivu yao ili wale wanasiasa alikuwa anawatabiria wawe wanaenda kusujudia majivu!!!! Kweli kama serikali inaamini ramli hata kuitolea press release basi tumekwisha!!!
 
wamevunja wao jiji..mgambo wao hawana nidhamu kabisa wanavunja na kuiba ni vibaka tu.
anapofanya uhalifu mfanyakazi wako ni wewe uliemtuma ndio unahusika.
walichofanya ni fitina na kuwafitinisha wananchi na serikali yao hakuna mambo ya usafi hapa tusidanganyane ....
 
Ngoja afufuke aje atutabirie serikali mbili au Tatu?
 
Si Mila wala desturi zetu Waafrika kubughuzi sehemu Za makaburi, hii sasa imekuwa comon kila mahali hapa Tanzania..... Na hii ni kutokana na mmomonyoko wa Maadili, kuanzia kwa viongozi hadi wananchi.
Kweli tumeshindwa kuheshimu sehem Za makaburi?????
 
Wangemchoma tu moto halafu wahifadhi majivu yao ili wale wanasiasa alikuwa anawatabiria wawe wanaenda kusujudia majivu!!!! Kweli kama serikali inaamini ramli hata kuitolea press release basi tumekwisha!!!

Harafu mnajimu Jr analalama mpaka Anita media kuwa kaburi limebomolewa na City!!!!!!, harafu serikali nayo anaandaa mipango ya kulijengea?????!!"!"". Wonders will never end, only in Tz
 
Back
Top Bottom