figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali Palamagamba Kabudi, amewaasa wanasiasa waache kujadili watu hasa Viongozi wetu Wastaafu kwani haitasaidia chochote na Baadala yake Walete maoni na Mawazo nini kifanyike ili kurekebisha Sheria za madini sababu rais amesharuhusu kufanya hivyo. Kujadili watu hatusaidia kama taifa.
"Hakuna mahali hata pamoja panapowataja Wazee wetu Waliostaafu kwenye repoti. Kuwatajataja na kuwaingiza itatuondoa kwenye jambo muhimu tulilonalo sasa". Amesema kabudi.
Kabudi kaongeza kwamba "Kazi kubwa tuliyonayo sasa ni kubadili Sheria ya Madini, Kama mlivyomsikia Rais kaagiza Sheria ya Madini ifanyiwe Malekebisho, iwe sheria ya madini bora inayotusaidia kuziba ile mianya tuliyokuwa nayo.
Kabudi katoa wito na anasema anheshukuru na anaomba kila mtu ashiriki katika hili "Naomba Watanzania wote na hao wengine, badala ya Kuwajadili Viongozi Wastaafu, sasa tulete maoni yetu, mawazo yetu ya aina gani ya mabadiliko tunayoyataka katika Sheria ya madini, Sheria ya Petroli, Sheria ya Gesi, Sheria za Kodi ili kweli mwisho wa siku tufaidike na laslimali hizi maliasili hizi ambazo wanaoamini Mungu kama mimi Mwenyezi Mungu alitupa.
Kaongeza "Wamefikisha nchi mahali ilipo na sisi tupo salama. Marais wote wameondoka kwa amani, hata bara la Afrika sisi ni katika nchi chache ambazo Marais wastaafu, Mawaziri Wakuu Wastaafu na viongozi wote wastaafu wapo pamoja na Wanaongea. Nchi nyingine Afrika hawana bahati hiyo".
Kasema ni wakati mwafaka kufanya marekebisho. Na kweli kuna mambo yamepungua, Leteni Maoni tufanyie marekebisho hizo Sheria na tuwaache hawa wazee wapumzike.