Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,796
- 31,809
Mohamed Abdallah Kaujore
Kaujore hakuhukumiwa na aliendelea kuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi.
Siku za za mwisho wa maisha yake alipata wazimu lakini badala ya kuwekwa ''Mental Hospital,''' akalazwa Mnazi Mmoja Hospital chumba cha faragha.
Humo alianza kula mavi yake mwenyewe na mara kadhaa alijaribu kutaka kujiua kwa kujirusha ghorofani.
Kaujore alifungwa kamba na kuwekewa askari wawili kumlinda asijidhuru.
Kaujore alifariki akiwa katika idhilali hii.
Mtume SAW ametuasa tuiogope dua ya mtu aliyedhulumiwa.
Kisa cha Kaujore tumekileta hapa ili kiwe somo kwa vijana wa leo Mazombie wanaoiga tabia zile zile za waliowatangulia na kwa njia ile ile ya kujificha nyuma ya migongo ya nguvu za siasa wakipita majiani na kuingilia watu majumbani na kuwadhalilisha.
Hawa ndugu zetu wakae wakijua kuwa Allah anawaona na yeye ni mwenye kutimiza ahadi zake.
Waangalie nini ilikuwa khatma za akina Kaujore na Said Washoto.
Said Washoto alimaliza maisha yake akiwa omba omba pale Darajani.
Upo wajibu mkubwa sana wa kuieleza historia hii ili kizazi hiki cha leo ijue Zanzibar imetoka wapi na wao wafanye juhudi kuona kuwa visiwa hivi havirejeshwi tena nyuma kwenye historia ya kufedhehesha.