Kabla ya kufikiria harusi, weka haya akilini!

Kabla ya kufikiria harusi, weka haya akilini!

Mambo ya kuchangishana na kukimbizana na watu huwa sipendi kabisa naona kama ni kuoneana sema tatizo linakujaga kuwaelewesha ndugu wa pande zote mbili especially upande wa mke ni shida sana kukuelewa, tena kwa watu wa ukanda wa pwani hawato kuelewa kabisa mkuu
Mimi harusi yangu ntafunga asubuhi jumuiyani ntamwita padri kwenye jumuiya itashereheshwa na wanajumiya na ndg wachache wa pande mbili. Jambo hilo nimeshamweleza ila anasema ati simpendi.!
Ukweli ni kwamba mimi nimechangia watu wengi sana ikafika mahali nikaacha.

Ukiniambia nifunge harusi ya ukumbini Mzee wangu hataudhuria (ninavyojua) sasa yanini ufanye Harusi uibue hoja za watu kukujadili kuhusu wazazi wako? Haina maana.
 
Kuna mtu ataangalia hiyo picha , afu ataenda kwenye ule uzi wa kupata tunda kimasihara na atatunga stori alikua mpiga picha wa harusi mara akala tunda kimasihara.
 
Mwanaume pambama wewe....maisha ni kitu gani haya bana....kujibanabana...tafuta hela fanya harusi, andaa sherehe watu wafurahi, wale, wanywe....sherehe ya harusi ndo sehemu ambayo unakutanisha ndugu wa pande zote mbili kwa wakati mmoja..watu watajuana hapa....ndo maana wanatambulishana...Acheni kulialia vijana na kujifanya mnajua sana budget na kupanga maisha....
Andaa sherehe ,,chakula, maji etc..kwa ajili ya sherehe ya ndoa yako...na Mungu atawabariki na atawarudishia....
Kuandaa harusi ndo kipimo cha kwanza cha mwanaume halisi....ni kipimo cha jinsi alivyo na ushirikiano na jamii na watu wanaomzunguka..
Kama huyo uliyenae ulimpima kwa kipimo hicho, kongole kwenu
 
Kwa kiasi kikubwa pana kaukweli ila si kweli kwamba tajiri anatumia kama masikini.
Acha wajidanganye hao.

Wanakariri viquote vya motivation speakers.

Ulinzi wa hao matajiri ni bajeti ya mishahara na posho za wizara nzima hapa bongo.

Gharama za vaccation zao unaweza angusha appartments za kutosha nje kidogo ya mji.

Elimu za watoto wao kwa mwaka ni mshahara wako kwa miaka almost 10 hadi 20.

Uziri wa hao jamaa wana bajeti kali sana na wanaziheshimu. Pia, wana financial discipline ya kutosha. Wanajua wanachofanya.

Hakuna billionea akatumia kama masikini.
 
Zama hz ukitaka kuoa n heri ujigharamie mwnyew michango na ufanye shereh iliyo ktk uwezo wako... Ukitegemea michango ya watu bas jipange na kulipa madeni mana watakuangusha tuu...
 
Ndoa Ina thamani zaidi ya sherehe lakini hii haimzuii mtu kufanya sherehe kubwa.
Kila mtu yupo na interest zake ..kuna wengine wanapenda sherehe,Kuna wengine hawapendi.
Cha muhimu watu wafanye wanavyotaka.
Naahidi kukufanyia sherehe kubwa kadri utakavyotaka.

Will you marry me ?[emoji101]
 
Kuna mtu aliandika hapa juzi kati kama itakulazimu kufanya sherehe basi garama nzima isizidi nusu ya kipato chako kwa mwaka. Nilimuelewa sana.
Hii michango inafanya tunashindwa hata kuwanunulia maharusi zawadi za kumbukumbu maana ukiwaza ulishangia mchango wa maandalizi. Zawadi umpelekee nani sasa.
Kuna mtu amesema haya mawazo yote yanaletwa na umaskini. Sijui kweli
 
Kuna watu wanapenda sherehe halafu binafsi uwezo kugaramia hata nusu ya garama ya sherehe hawezi. Yani michango yake na familia yake na watu wake wa karibu na bado garama ya sherehe haitimii. Ndio hapo unaanza kuwapigia watu simu hata ulikua huna mawasiliano nao miaka kibao. Zaidi ya kuangaliana WhatsApp status hamna salamu.
Mkuu inaonekana ili suala la kuangalia whatsapp status halafu napita kimya kimya huwa linakukera sana. Kuanzia usiku wa leo nitaanza kukusalimia
 
Back
Top Bottom