Kabla ya kuwapa watu ID ni lazima kuwe na utaratibu wa kuwa na anwani. ID bila anwani ni kama picha tu. Hapa USA kwa mfano tuna anwani za nyumbani kwenye ID na kama hiyo haiwezekani basi waweke ZIP Code. Nilisikia miaka miwili iliyopita serikali ya German iliwapeleka wafanyakazi wa posta kusomea jinsi ya kuweka ZIP code Tanzania. Ni muhimu kwa ID kuonyesha unaishi wapi ili ziweze kutumika kwenye vitu vingine vya maendeleo kama Mikopo ya Bank, Statistics, Insuarance, education na security. Sasa Tanzania wanataka kuweka ID bila anwani itakuwa ni uwekezaji mbovu.