Kabla Rais hajakuteua, ni lazima upate taarifa mapema?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Habarini Wakuu!

Kwa nafasi za uteuzi chini ya Mhe. Rais, mteuliwa ni lazima utafutwe na kupewa taarifa mapema kabla ya uteuzi au unaweza kushtukizwa tu?

Je, wakikushtukizwa halafu baadae usipatikane hewani itakuwàje?

Je, wakikushtukiza halafu baadae ukawa hauitaki hiyo nafasi inakuwaje?
 
Ulisikia katibu mkuu alivyo hadithia? Ye alifuatwa akapewa ticket ya ndege akambiwa aende uwanja wa ndege anahitajika home chap ndo akaja kujua akiwa ktk uwanja wa ndege kwa kutizama taarifa ya habari, unapokua serikalin unataikiwa uwe awea na kila taarifa, every second ujue majukumu ya kila ngazi kwan ye maa Samia alijua atakua rais
 
Hata mimi sikuwa na taarifa kabisa
 
Nafikiri kuna nafasi hushauliwi ali mradi wakubwa wamejiridhisha kwamba unatosha kwa sababu huteuliwi tu, kuna vetting hufanywa
 
Ndio serikali ilivyo mkuu, unaweza ukawa mfanyakazi wa Songea ukaamka asubuhi ukaambiwa uhamie Bukoba.
 
Kumpa mtu muda wa kutafakari uteuzi wake na jambo jema zaidi
 
Kuhamishwa kituo cha kazi ni tofauti na kupangiwa nafasi nyingine ya kazi.
Ndio serikali ilivyo mkuu, unaweza ukawa mfanyakazi wa Songea ukaamka asubuhi ukaambiwa uhamie bukoba
 
Ulisikia katibu mkuu alivyo hadithia? Ye alifuatwa akapewa ticket ya ndege akambiwa aende uwanja wa ndege anahitajika home chap ndo akaja kujua akiwa ktk uwanja wa ndege kwa kutizama taarifa ya habari, unapokua serikalin unataikiwa uwe awea na kila taarifa, every second ujue majukumu ya kila ngazi kwan ye maa Samia alijua atakua rais
Umechanganya kidogo.

Jamaa alikuwepo Tanzania akijiandaa kurudi Japan, na alikuwa na ticket ya Japan tayari,

Ila ndo akafuatwa na kuelekezwa kwenda airport na kupewa ticket ya Dodoma, akiwa waiting louge ndipo akafahamu kuhusu uteuzi.

Lakini hii ni kwa watumishi wa uma ambaye anakuwa kama kahamishwa.

Kwa amabao si watumishi wa uma, nadhani huulizwa au hupewa prior notice.

Kama nakumbuka RC wa kilimanjaro mama Mgwila alisema alipigiwa simu na hayati, akamwambia anataka amsaidie kazi, akakubali ila hakujua ni kazi gani hadi alipoona uteuzi.
 
Mara nyingi huwa wanastukizwa

Prof Juma Othman Kapuya aliteuliwa kuwa Waziri wa Michezo mara ya kwanza 1995 akiwa Jukwaani anashangilia mechi ya Simba Uwanja wa Taifa,

Huu utaratibu sio Mzuri kabisa kwa kuwa

a) inawezekana Mhusika akakataa kama yule jamaa wa Tigo aliokataa Uteuzi wa UDC halafu ikaonekana eti kadharau Mamlaka ya Amiri jeshi na baadae Mtendaji Mkuu wa Tigo akashauriwa amfukuze kazi ili asije akapigwa Tax Audit kwa mtumishi wake kukataa heshma aliyopewa na Rais

b) inawezekana mhusika ana makando kando mengi ambayo kama ingejulikana kuwa karibia anateuliwa Raia wema wanaweza kujulisha Mamlaka, mf US wenzetu kule utaskia kabisa Rais anatarajiwa kumteua Fulan kuwa Waziri wiki ijayo

Samia mwenyewe anakiri alistukizwa kuwa Mgombea Mwenza

Mzee Makamba alipostukizwa kuw Katibu Mkuu wa CCM akiwa Mkutanoni anapiga soga bila ya habari

Atleast Sumaye anasema aliitwa na Rais saa moja kabla ya kutangazwa na kujulishwa

Mizengo Pinda alipoteuliwa kuwa PM anasema alikuwa zake kwake na Rafiki yake Paul Kimiti wanajadili nani atakuwa PM muda mchache kabla ya Jina kufikishwa Bungen akashangaa Gari za Ikulu zimeingia kwake anahitajika aingie ndani ya Gari kwenda kwa Rais, Paul akamwambia ''Kikombe tayari kimekuangukia'

Kuna Bregadier wa Jeshi aliwahi kutangazwa kuwa Mnadhimu wa Jeshi enzi za Mwalimu akiwa Nachingwea anacheza zake mpira
 
Hakuna formula, ila nafasi za juu kama PM huwa wanapewa taarifa kabla ya kutangazwa hata mpango I guess alijua kabla ya kutajwa bungeni.
 
Zamani ilikuwa inafanyika vetting na unaweza kupigiwa simu na Rais akakuuliza kama utakubali endapo utapewa nafasi flani ili akufikirie. Ukisema ndyo anainclude jina lako kwenye vetting.

Ila siku hizi ni nani anaweza kukataa cheo jamani. Habar unakutana nayo juu kwa juu. Tena mama mjanja anajua habari zinaweza mvujia kigogo.
 
Ulisikia katibu mkuu alivyo hadithia? Ye alifuatwa akapewa ticket ya ndege akambiwa aende uwanja wa ndege anahitajika home chap ndo akaja kujua akiwa ktk uwanja wa ndege kwa kutizama taarifa ya habari, unapokua serikalin unataikiwa uwe awea na kila taarifa, every second ujue majukumu ya kila ngazi kwan ye maa Samia alijua atakua rais
Kwani kifo kina taarifa? Wewe nae
 
Back
Top Bottom