Kabla hujamnyooshea mtu kidole

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
KABLA HUJAMNYOOSHEA MTU KIDOLE, KABLA HUJAMLAUMU MTU, KABLA HUJAMLALAMIKIA MTU, JARIBU KUVAA VIATU VYAKE NA UJIULIZE UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI?

Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho, ni kwamba kila mtu mzima na mwenye akili timamu anataka kuwa na maisha bora zaidi ya aliyonayo sasa. au kama aliyonayo sasa ni bora, basi yaendelee kuwa hivyo.

Lakini katika kufikia maisha haya bora, ndio kunakuja changamoto nyingi sana kwenye dunia yetu. Kuna ambao wanatafuta njia rahisi za kufanya hivyo, kuna wengine wapo tayari kusubiri, kuna wengine wanataka sasa na mengine mengi.

Katika safari hii ni rahisi sana kunyooshea wengine vidole na kuona kama wao wana matatizo sana zaidi yetu. Au hawajui kile wanachofanya. Au wanafanya makusudi kutuharibia sisi mipango yetu.

Ni rahisi kufikiria hivi kwa juu juu, lakini ukipata nafasi ya kuvaa viatu vya watu hao, utaona ni kwa nini wanajikuta wanafanya hivyo. Wakati mwingine hawafanyi kwa sababu wanapenda, ila wanafanya kwa sababu inabidi.

Kitu kimoja nataka nikuambie ni kwamba kila mtu unayemwona ana matatizo na changamoto zake, ana vita yake anayopigana ndani yake au hata na watu wengine.

Unaweza kumwona anacheka lakini ndani ana vitu vingi vinaendelea, ambavyo kama angeamua kuvipa nafasi basi asingestahili kucheka.

Hivyo kabla hujalaumu mtu, kabla hujanyoosha vidole, kabla hujalalamikia mtu, jaribu kuvaa viatu vyake na uone wewe ungefanya nini.

Kama ungeweza kufanya tofauti, basi badala ya kumlalamikia utakuwa mshauri mzuri. Utamwambia kwa mimi kama ningekuwa kwenye hali hii uliyo sasa, basi ningechukua hatua hii.
 
Last edited by a moderator:
kila kitu na wakati wake in rightplace.
unabwabwaja tu.

swissme
 
Nin sabab ya kuandika haya yote?it seems kipo kinachokutatiza moyon,sivyo?go direct to the point at least to free your heart,,sawa mwaya eeee
 
Back
Top Bottom