Kabla hujaagiza gari, pitia hapa kujua gharama kamili za ushuru na bandarini

MAGARI7

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
2,401
1,298
Habari za muda huu,

Pamekuwa na thread nyingi sana za watu kuomba ushauri/ elimu hasa kwenye suala zima la budget halisi/ kamili ambayo mtu anahitaji kuwa nayo kuweza kumiliki gari.

Kwa bahati mbaya, wengi wamekuwa wakipewa gharama kubwa tofauti na uhalisia hiyo yote kwasababu hawajui. Nimeona ni vyema tukafungua huu uzi, Na mimi nimeamua kujitolea kutoa elimu hiyo kwa kadri ya uzoefu wangu.

Naamini si mimi tu ninayefahamu, bali wapo wengine pia, lengo ni kusaidia wote wajue gharama halisi wanazotakiwa kulipia kuweza kumiliki gari.

Nitakuwa hapa kukusaidia mahesabu halisi ya ushuru na gharama zote za bandari unazotakiwa kulipia kwacajili ya kuweza kumiliki gari lako.

NOTE:
Hakikisha unapouliza, unakuwa na mfano halisi wa gari husika ili uweze kupata hesabu halisi ambazo sio za kufikirika. Mfano, unaulizia bei ya Toyota IST, kama gari hiyo labda umeiona mtandao fulani wa kuuza magari (be forward, enhance etc), unanipatia link tu ya gari husika, kisha nakusaidia kuipigia mahesabu halisi.

Kinyume na hapo, yatakuwa ni mahesabu ambayo sio halisi (ya kufikirika)

Ahsante, naamini na wengine wenye uelewa/ufahamu watajumuika hapa kwa ajili ya kusaidia wanaohitaji kujua gharama halisi za ushuru na gharama za bandari wanazohitaji kulipia kwa ajili ya magari yao.

Karibu, tusaidiane!
 
Mfano, unaulizia bei ya Toyota IST
Hapa tuongeze na kipengele cha mwaka pia, kuna tofauti ya bei kutegemea mwaka husika.
===
Naomba mchanganuo wa gharama kwa hii gari
TOYOTA MARK X ya mwaka 2009
LINK: Used 2009 TOYOTA MARK X 250G S PACKAGE/DBA-GRX120 for Sale BG179330 - BE FORWARD

1071861
 
T1986MCK,
Habari Mck,
Kwa mujibu wa TRA calculator
Ushuru wa gari yako ni 11,029,645.19
Na bei ya kuifikisha gari hadi bandari ya Da es salaam, kwa sawa sawa na screenshot yako ni 10,742,976.
11,029,645.19 (Ushuru)
10,742,976 (CIF)
Inakuwa : Tshs 21,772,621.19

Handling ni $7 jumlisha VAT (18%) per cbm (cubic meters)
Ile gari ina 14.621 CBM

Kwahiyo unafanya $7*14.621 = $104 plus VAT (18%)
$122.72
Kwahiyo handling inakua $122.72

CORRIDOR LEVY ;
$0.3 plus vat per cbm

$0.3*14.621 = $5 + 18% VAT = $5.9

Kwahiyo Corridor levy inakua $5.9

WHARFAGE :
Hii huwa ni 1.6% ya thamani ya cif
Cif value ya gari yako ni $4,640

$4,640*1.6% = $74.24

Kwahiyo wharfage ni $74.24

TUJUMLISHE

Handling = $122.72
Corridor levy = $ 5.9
Wharfage = $74.24

= $202.86

Ukichange kwa TZS inakua Tshs 476,000
Jumlisha agency fee (200,000)

Inakuwa Tshs 676,000

USHURU NA GHARAMA ZA KULETA HII GARI TULISEMA JUMLA NI

Tshs 21,772,621.19

Kwahiyo Tshs 21,772,621.19 jumlisha 676,000

Inakuwa TSHS 22,449,000 (Hiyo ndiyo budget kamili ya kumiliki hilo gari, yaani hadi kuwa nalo mikononi. Bima haijajumuishwa)
 
Hapa tuongeze na kipengele cha mwaka pia, Kuna tofauti ya bei kutegemea mwaka husika.

**************
Naomba mchanganuo wa ghalama kwa hii gari
TOYOTA MARK X ya mwaka 2009
LINK: https://bit.ly/2UkpSXA

View attachment 1071861
Hapa utakua umesaidia wengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jeep wrangler
Cc 2700
Year 2009
hivi calculator ya TRA haifanyi kazi hadi tuulize kienyeji!?
nilitegemea jamaa aweke link ya hicho kikokotoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

TOYOTA VOLTZ

Cif = Tshs 6,891,000
Ushuru = Tshs 7,048,000= 13,039,000

Handling = $7*12.348 = $86.436+ 18% vat = $102
Corridor levy = $0.3*12.348 = 4 + 18% vat = $4.72
Wharfage = 1.6%*2,976 = $47.616

= $155 = Tshs 364,000

Pllus agency fee 200,000

= Tshs 564,000

13,039,000 + 564,000

= Tshs 13,603,000

(Hapo hadi kuitoa bandarini na kuwa mikononi mwako, bima haijajumuishwa)
Na labda kama budget inakua imebana kwa sababu za wingi wa kimajukumu

Unaweza kuiagiza gari hii kupitia Semsella ENTERPRISES
Badala ya kulipia 13,603,000
Unalipia 10,202,250 tu
Gari ikifika, unakabidhiwa

3,400,750 iliyobakia unaimalizia kwa instalment
Ya muda wa miezi 7
Kila mwezi 486,000

Instalment zinaanza mwezi mmoja baada ya kukabidhiwa gari lako.


Semsella Enterprises/ecarstanzania
P.o.box 63178, Dar es salaam
Shekilango, nhc plot number 242
Block number 1,1F
Call/text/Whatsapp text us 24/7
+255745229947
 
hivi calculator ya TRA haifanyi kazi hadi tuulize kienyeji!?
nilitegemea jamaa aweke link ya hicho kikokotoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari ndugu,

Calculator inafanya kazi sawia kabisa .. na ndio hiyo tunayoitumia.
Lakini, elewa kwamba, baada ya ushuru, kuna gharama zingine za bandari n.k
Gharama ambazo huzikuti kwenye kikokotoo cha Tra.

Kwa sababu hiyo, watu wengi wamekua wakipewa gharama kubwa ambazo sio sahihi na baadhi ya watu (wakutoa magari/kuagiza) ambao sio waaminifu.

Ndio maana nimejitolea kufafanua hizo gharama hapa.

Natumai umenielewa.

Ikiwa kuna mahali unaona labda napotosha kwa namna iwayo yote ile
Nakuomba, unisahihishe.

Ahsante.
 
Aweke kikokotoo halafu yeye akale wapi???hii ni project ya mtu na anategemea kupiga hela yake saaaafi!
http://gateway.tra.go.tz/umvvs/Default
ipo wazi tu ni mwenye gari ajaze hilo Jedwal mwisho agonge Calculate anapewa jibu ndipo amuombe agent km huyu MAGARI7 (Semsela Agency) amtolee hilo gari ndipo aongezee km laki tano hivi ya mahesabu ya ke
  • Handling ni $7 jumlisha VAT (18%) per cbm (cubic meters)
  • CORRIDOR LEVY ; $0.3 plus vat per cbm
  • WHARFAGE :Hii huwa ni 1.6% ya thamani ya cif
  • Jumlisha agency fee (200,000)
  • BIMA 3rd part km 118,000/
  • Plate no kibao 40,000
 
Mkuu MAGARI7 hebu jaribu kumuwekea hesabu zake proskaeur kwa hii MURANO inayokaribiana na mahesabu yake, maana ushuru milioni 9.8 manunuzi milioni 8 gharama za kuitoa kwa Kampuni yako
Bima na Plate no, itafikia ngapi?
Used 2008 NISSAN MURANO 350XV/CBA-PZ50 for Sale BG187367 - BE FORWARD
View attachment 1072032
View attachment 1072026
Hii ni kama ifuatavyo

Cif = Tshs 8,000,000
Ushuru = Tshs 9,802,000= 17,802,000
Handling = $7*15.066= $106+ 18% vat = $125
Corridor levy = $0.3*15.066 = $5 + 18% vat = $5
Wharfage = 1.6%*$3,470= $55.52

= $186 = Tshs 436,000

Pllus agency fee 200,000

= Tshs 636,000


+ 636,000

= Tshs 18,438,000 plus 30,000 ya plate number

Jumla Tsh 18,468,000
(Hapo hadi kuitoa bandarini na kuwa mikononi mwako, bima haijajumuishwa)
Na labda kama budget inakua imebana kwa sababu za wingi wa kimajukumu

Unaweza kuiagiza gari hii kupitia Semsella ENTERPRISES
Badala ya kulipia kwa awamu awamu ya hadi miezi 7
Unalipia 13,851,000 tu
Gari ikifika, unakabidhiwa

4,617,000 liyobakia unaimalizia kwa instalment
Ya muda wa miezi 7
Kila mwezi 660,000

Instalment zinaanza mwezi mmoja baada ya kukabidhiwa gari lako.

Semsella Enterprises/ecarstanzania
P.o.box 63178, Dar es salaam
Shekilango, nhc plot number 242
Block number 1,1F
Call/text/Whatsapp text us 24/7
+255745229947
 
Back
Top Bottom