Kabla hamjaanza kumsifia Magufuli kwa kulipa Walimu mishahara miezi 2 lazima mtambue haya

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,959
36,968
Nina hakika CCM itashinda chaguzi nyingi zijazo na kuendelea kuiongoza nchi hii ya Tanzania.

Sababu kubwa ni ujinga + upumbavu wa Watanzania wengi. Samahani najua nimewakwaza wengi kwa neno upumbavu na ujinga ila haya maneno hayana undugu na matusi.

Leo unatoa shukrani kwa Rais kisa amelipa mshahara wa walimu takribani miezi 2 bila kufundisha watoto. Hii sentensi ni kama kumpa mamlaka zaidi Rais juu ya fedha za nchi hii.

Shule binafsi baadhi zimeshindwa kulipa mishahara kwa walimu kwakuwa biashara ilisimama huku Serikali haieendeshi Shule zake kibiashara. Tena Shule za serikali zingekuwa hazijafungwa zingeifanya Serikali itumie fedha nyingi zaidi kuziendesha kwa hiyo miezi 2.

Pia ikumbukwe kuna nchi zililazimika kuwalipa hata walimu wa shule binafsi ili kuwatia moyo watu wa sekta binafsi.

Kwa katiba ya Tanzania ni kweli Rais anamamlaka hata ya kusimamisha au kuzuia mshahara wa mtumishi yoyote wakati wowote kwakuwa yeye ndiye chief treasure.

Tanzania viongozi sasa kazi yao ni kujikomba kwa Rais na si kuwatetea wanaowaongoza.

Hii hamjaanza leo but awamu ya tano imezidi. Miaka fulani nyuma mimi na wenzangu tulichaguliwa kuandaa Risala kwaajili ya mgeni rasmi kwenye ghafra fulani. Cha ajabu siku ya tukio Risala ilibadilishwa kwa 75% na boss kwa sababu za kujipendekeza na kutafuta cheo zaidi huku challenges tulizoziorodheshwa zikifutwa ilhali zipo mpaka leo.
 
Hapo kuna wamiliki wa shule wawezeshwe, kule kuna wenye mahoteli nyuma kuna waliojiajili kutokana na kusimama shuguli za watalii na nk, wote wanatakiwa kuwezeshwa siyo walimu/wenye shule binafsi tu.

Unapoangalia issues za jamii fulani ionewe huruma fungua pazia la kichwa chako utizame mbele zaidi ndipo utajua kuna wakati kila mtu abebe msalaba kwa upande aliopo.
😷
 
Wamiliki wa Hotel, Biashara nk wameathirika natural na janga ila wamiliki wa shule wanaathirika kwa Tamko la funga shule tofautisha hivyo vitu.
 
Namshangaa katibu anasema hamna haja ya nyongeza ya mshahara kama madaraja yanapandishwa je wangapi wananufaika na kupanda madaraja.

Hata mimi nikiambiwa nichague kupandishwa daraja kwa wakati na kuongezewa mshahara, nitachagua kupandishwa daraja (Kila mfanyakazi ana sifa hiyo kila baada ya miaka 3)

Mshahara anaweza kukuongezea elfu 20 tu! Lakini kiwango kinacho ongezeka kwenye upandaji wa madaraja huendana na muda wa mfanyakazi kazini. Na unakuta siyo chini ya laki 1!
 
binadamu buana MNA kazi,, asinge walipa mngetia neno kawa lipa mnatia neno tena si kwa kuona kuwa amefanya jambo zuri,. Kumbuka kuwa hao walimu wanawakuwategemea nyuma yao.

ungenambia kwenye kuwaongezea na kuwapandisha madaraja,hapo unge kuwa umenena sambamba na watanzania, ila kila MTU anamaoni yake,
 
Wamiliki wa Hotel, Biashara nk wameathirika natural na janga ila wamiliki wa shule wanaathirika kwa Tamko la funga shule tofautisha hivyo vitu.
Nilitaka kupotezea ila nimeona nijifunze kutoka kwako.

Kwa hiyo unataka kuuambia umma "kutokana na comment yako hapo juu" kuwa kutokana na janga la covid shule hazikupaswa kufungwa?.
Kisa "Tamko la funga shule tofautisha hivyo vitu"
 
Wamiliki wa Hotel, Biashara nk wameathirika natural na janga ila wamiliki wa shule wanaathirika kwa Tamko la funga shule tofautisha hivyo vitu.

Mkuu tamko la kufunga Shule halija sababishwa na Janga kuwepo?
 
Back
Top Bottom