Art
JF-Expert Member
- Nov 13, 2015
- 611
- 88
Habarini Wakuu,
Kuna siku nilikuwa duka flan hivi na pembeni mwa dirisha la duka hiyo kulikuwa na ubishani mkubwa pamoja na matambo kutoka kwa wachagga wawili wakijisifia kuwa wao wanajua sana kuwalisha wake zao pale wanapojifungua kuliko makabila yote Tanzania.
Kwa kawaida mwanamke mzazi wa kichaga akijifungua (na akiwa ameolewa rasmi) huwa anachinjiwa Mbuzi,kondoo au Ng'ombe tena zaidi ya mara moja na kisusio juu na atakaa ndani kunywa mtori hata kwa miezi miwili mpaka mitatu.
Wachagga wakaendelea kusema kuwa mwanamke anapojifungua,anapaswa kunenepa mpaka ashindwe kupita mlangoni,hiyo ni sifa kwa mumewe na jamii itamkubali mwanaume.
Aidha walitamba kuwa hawawezi kuwachinjia kuku au njiwa wake zao au kuwapikia uji wa ukwaju tu kama makabila mengine. Lakini na hao jamaa wa makabila mengine (Viasaka) wakauliza mbona sasa dada zao ndio wenye afya na maumbo mazuri umbo namba 8 na sio wachaga? Mimi mzungu nisiye na kabila nikajiuliza maswali mengi yaliyonishinda nikaona nilete kwenu wadau naamini mnajua zaidi.
Ni kabila lipi ambalo wanaume wake wanajua kuwatunza na kuwajali kwa chakula wake zao pale wanapojifungua?