Kabila la Wakutu (kutoka Morogoro)

Kabila la Wakutu (kutoka Morogoro)

Wakutu wameshajichukulia kama kabila ila kiuhalisia wakutu ni Waluguru wa bondeni ambao ndio wametoa wazaramo. Wazaramo wengi wanalijua hilo kuwa asili yao ni ukutu, na wakutu nao wanalijua hilo kuwa asili yao ni Uluguru. Wakutukila kuhisi, ni kiluguru kikimaanisha wamedondokea bondeni. Na ndio uhalisia. Zamani jamii ziliishi katika makundi ya koo, hakukuwa na makabila. Ila koo hizo zilikuwa zikifanana katika mambo mengi na pia zilikuwa zikihamahama kwa sababu mbalimbali. Wakutu ni baadhi ya koo za Uluguruni zilizoelekea maeneo ya bondeni. Ukichunguza vizuri koo za wakutu na wazaramo, utagundua kuwa zaidi ya asilimia 90 ni koo za Kiluguru, na kuna koo chache sana ambazo haziko uluguruni, Na Waluguru wana koo nyingine ambazo haziko kwa wakutu na Wazaramo na Wakwere. Hitimisho. Ukitaka kujua nani ni muhasisi wa hizi jamii, jaribu pia kuchunguza tamaduni nyingine kama Ngoma na maeneo ya tambiko. Wakutu, Wazaramo na Wakwere wote wanatambua kuwa kwenye mzimu wao ni Kolelo ambako ni Uluguruni. Ili kupata uthibitisho wa hili, tafuta wale wazee haswa wanaojua historia za jamii zao.
Shukran kwa nyongeza nzuri
 
Ukifuatilia sana utakuta kuwa Tanzania tuna makabila machache sana. Ila wengine walihama wakajiita kabila, na koo zingine zikajiita kabila.

Hii Habari kutoka Kitabu Masimulizi Juu ya Wazaramo. Utaona kuwa Zaramo ni kabila jipya tu.

PAZI KILAMA KATIKA UZARAMO

WAZARAMO ni jumla ya mchanganyiko wa makabila ya Kibantu. Sehemu kubwa ya mchanganyiko huo ni Wakutu na watu wengine wenye asili ya Mwambao. Neno hili 'Uzaramo' linatokana katika 'Kuzalama' na maana yake ni 'Kusehelea'. Kwa hivi, Wazaramo hasa maana yake ni Waseheleaji, yaani watu waliotoka katika nchi mbalimbali na kufanya masikani katika nchi hii. Mabadiliko ya neno hili yalitokea kwa sababu ya matamshi ya watu; neno lenyewe hasa ni Zalamo, yaani nchi iliyosehelewa, lakini baadaye ikabadilika na kuwa Zaramo au pengine hutamkwa Zaramu.

Hatuna hakika ya tarehe maalumu ya kusehelea, ila twafahamu hayo katika masimulizi ya mgawanyiko wa koo mbalimbali za Uzaramo ambazo nyingi zinasimuliwa kwamba zimetoka katika makabila mengine ya Kibantu na kujiunga katika Uzaramo. Lakini wazee wengi wanakubaliana kwamba mkubwa wa Uzaramo alikuwa Pazi Kilama Lukali mwenye asili ya Ukutu.

Pazi huyo aliitwa kwa majina mbalimbali ya ushujaa na kutukuzwa kama hivi ‘Pazi Kibamandu, kihabamanduka na Ulanga wela', maana yake, ‘Pazi Kifuniko, Kikifunuka na mbinguni kweupe!' Na tena aliitwa 'Mwana Mkungwi pala' na 'Mwana Mwizila Kumogo', maana yake 'Mwana wa Utukufu' na 'Mwana ajiwaye kwa heshima'. Na katika kutukuzwa kwake aliitwa 'Gulu Jasi' yaani, 'Mfalme Mkuu'.

Pazi huyo asili yake hasa alitoka Kibwemandu, katika Ukutu, nchi iliyo sasa magharibi ya Uzaramo. Kwa upande mwingine ndio sababu aliitwa Pazi Kibamandu. Ukoo wake ni Mulugoma, na mtala wake ni Kilama na Lukali. Baba yake aliitwa Pazi Mvilama. Huyu Pazi Mvilama alimwoa Mulambena katika kizazi cha Nyambiza, akamzaa Pazi Kilama.
 
Wakutu wameshajichukulia kama kabila ila kiuhalisia wakutu ni Waluguru wa bondeni ambao ndio wametoa wazaramo. Wazaramo wengi wanalijua hilo kuwa asili yao ni ukutu, na wakutu nao wanalijua hilo kuwa asili yao ni Uluguru. Wakutukila kuhisi, ni kiluguru kikimaanisha wamedondokea bondeni. Na ndio uhalisia. Zamani jamii ziliishi katika makundi ya koo, hakukuwa na makabila. Ila koo hizo zilikuwa zikifanana katika mambo mengi na pia zilikuwa zikihamahama kwa sababu mbalimbali. Wakutu ni baadhi ya koo za Uluguruni zilizoelekea maeneo ya bondeni. Ukichunguza vizuri koo za wakutu na wazaramo, utagundua kuwa zaidi ya asilimia 90 ni koo za Kiluguru, na kuna koo chache sana ambazo haziko uluguruni, Na Waluguru wana koo nyingine ambazo haziko kwa wakutu na Wazaramo na Wakwere. Hitimisho. Ukitaka kujua nani ni muhasisi wa hizi jamii, jaribu pia kuchunguza tamaduni nyingine kama Ngoma na maeneo ya tambiko. Wakutu, Wazaramo na Wakwere wote wanatambua kuwa kwenye mzimu wao ni Kolelo ambako ni Uluguruni. Ili kupata uthibitisho wa hili, tafuta wale wazee haswa wanaojua historia za jamii zao.
Mzimu wa kolelo ni maarufu sana,je twaweza pata historia yake?
 
Kuna Mkutu kutoka ukoo wa Mamba, anasema kabila lao wana roho mbaya sana.
 
Wakutu ni Kabila linalopatikana mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Pwani. Kwa mkoa wa Morogoro wanapatilana katika wilaya ya morogoro ( Morogoro vijijini ) katika vijiji vya Dutumi, Mvua, kisaki, Ngerengere, Matuli, Kidunda, Kiwege, Lilongwe,Kongwa, Magogoni, Kilengwe, Kwaba n.k.

Katika mkoa wa Pwani wanapatikana katika wilaya ya kibaha( magindu, Dutumi ya kibaha, Chaduma, kisangire na baadhi ya maeneo ya wilaya ya kisarawe na chalinze. Ni Kabila kubwa ila nadra kukutana na watu wa Kabila hili la kikutu, Wakutu wengi wanakopatikana maeneo ya mkoa wa Pwani hujitambulisha kama Wazaramo au wakwere. Na wengine hujitambulisha kama waluguru, hivyo sio rahisi kukutana na mtu wa Kabila la kikutu, japo kuwa ni Kabila kubwa mojawapo kwa mkoa wa Morogoro na Pwani.

Maana ya Kabila la WAKUTU:

Neno Wakutu limetokana na neno la Kiluguru ( wakutuka ), maana yake waluguru waliodondoka au wanaoishi mabondeni. Neno wakutuka ndio limezaa Kabila la Wakutu. Wale wa mlimani ( waluguru ) waliendelea kujiita waluguru na wale wenzao ambao wanaoishi mabondeni waliendelea kuitwa Wakutu na ndugu zao wa mlimani, hiyo ndo chanzo cha Kabila la Wakutu, na mwisho wa siku wakajitenga na kuwa makabila mawili tofauti makubwa.

Zifuatazo ni baadhi ya koo katika Kabila la Wakutu:
1. Wanyange; mwanaume nyanga mwanamke mlanyanga ( kwa waluguru mara chache hutumia nyanga na mlanyanga, waluguru hutumia mkude,au kunga'aro na mwanamke huitwa mwenda )
2. Wanyange; mwanaume huitwa nyange, mwanamke mlanyange.
3. Wa mlali; mwanaume huitwa mlali na mwanamke huitwa mlamlali ( kwa waluguru; mwanaume bwakila , mwanamke mlali au mlamlali).
4. Wabena; mwaume mbena, mwanamke mlambena.
5. Wakiraru; mwanaume kiraru, mwanamke mlakiraru.
6. Wahafigwa; mwanaume mhafigwa, mwanamke mlahafigwa.
7. Mponda; mwanaume mponda, mwanamke mlamponda.
8. Zongo; mwanaume zongo, mwanamke mlazongo.
9. Wa mindu; mwanaume semindu, mwanamke mindu.
10. Wa mng'ango; mwanaume mng'ango, mwanamke mlamng'ango.
11. Wakali; mwanaume mlali, mwanamke mlamlali.
12. Wa chuma; mwanaume chuma, mwanamke mlachuma ( kwa waluguru; mwanaume mponda, mwanamke chuma).
13. Wa kwambe; mwanaume mkwambe, mwanamke mlamkwambe.
14. Wa tebe; mwanamke mlatebe, mwanaume tebe.
15. Wasagara; mwanaume sagara, mwanamke mlasagara.
16. Wahimbwa; mwanaume dihimbwa, mwanamke mladihimbwa.
17. Wa chogeza; mwanaume chogeza, mwanamke mlachogeza.
18. Wakiluwa; mwanaume kiluwa mwanamke mlakiluwa.
19. Wakongela; mwanaume kongela, mwanamke mlakongela.
20. Watonga; mwanaume mtonga, mwanamke mlamtonga.
21. Wa chili; mwanaume mchilo,mwanamke mlamchilo
22. Wa mbali; mwanaume m'bwali, mwanamke mlam'bwali.
Hizo ni baadhi ya koo za Kabila la Wakutu, utaona kwa asilimia zaidi ya tisini zinafanana na koo za waluguru au wazaramo au wakwere.

Lugha ya Wakutu;
Baadhi ya maneno ya kikutu, mfano; aulamke (umeamkaje)? Unajibu anoga ( vizuri), imanye gwegwe ( sijui wewe). Ausindile ( ushindaje)?, Ukae ( nyumbani), ukae kutali ( nyumbani mbali). Kwa ufupi lugha ya kikutu ni sawa na lugha ya kizaramo, kikwere au Kiluguru .
Ngoma za asili za Kabila la Wakutu ni Vanga, mdundiko, n.k. Hayo ni machache yanayohusu Kabila Wakutu, wenyeji wa mkoa wa Morogoro na manispaa ya Morogoro.
Bado mnaoata muda wa kuongelea makabila!!!! Du!!!!
 
Mzimu wa kolelo ni maarufu sana,je twaweza pata historia yake?
Kwa uchache.
Mzimu wa Kolero ni Mungu wa Waluguru na jamii zake.
Mzimu huu uliishi kwenye pango lililo chini ya mlima Lubasazi kando ya mto Lubasazi, kijiji cha Lubasazi kwenye kata ya Kolero tarafa ya Mvuha Morogoro vijijini.
Kolero alikuwa kwenye himaya ya Chifu Hegga wa Kolero, ambaye alikuwa na makazi yake kijiji cha Lubasazi. ( Kijiji cha Lubasazi kilitokana na kugawanywa kwa kijiji cha Kolero)
Mzimu wa Kolero ulihudumia jamii yake kupitia kwa mtoa huduma ( Kuhani Mkuu) aliyeitwa Bibi.
Bibi alikuwa binadamu (mtumishi) aliyekuwa anahudumia jamii hiyo kwa maelekezo ya Kolero mwenyewe.
Waluguru na jamii zao, Wazaramo, Wakutu, Wakwere, Wakami nk, walifika mahali hapo kufanya ibada.
Walienda kuomba, maombi binafsi na pia maombi kwa jamii zao.
Bibi ambaye ndiye aliyekuwa msemaji wa Kolero aliteuliwa na Kolero mwenyewe kutoka kwenye maeneo yake ya kiutawala.
Bibi aliteuliwa vipi, aliishije, aliishi wapi?
Tukutane kwenye uzi maalum unaohusu Mzimu wa Kolero ambao nitauleta hapa Inshaallah tukijaaliwa.
 
Bado mnaoata muda wa kuongelea makabila!!!! Du!!!!
Tunaongelea Makabila kwakuwa yametunza hazina ya historia ya mtu mweusi.
Nia ya uzi huu ni kujua kwa uchache kabila la  Wakutu
Kwasababu hiyo hakuna aliyebaguliwa.
 
Kwa uchache.
Mzimu wa Kolero ni Mungu wa Waluguru na jamii zake.
Mzimu huu ulikuwa unaishi kwenye pango lililo chini ya mlima Lubasazi kando ya mto Lubasazi, kijiji cha Lubasazi kwenye kata ya Kolero tarafa ya Mvuha Morogoro vijijini.
Kolero alikuwa kwenye himaya ya Chifu Hegga wa Kolero, ambaye alikuwa na makazi yake kijiji cha Lubasazi. ( Kijiji cha Lubasazi kilitokana na kugawanywa kwa kijiji cha Kolero)
Mzimu wa Kolero ulihudumia jamii yake kupitia kwa mtoa huduma ( Kuhani Mkuu) aliyeitwa Bibi.
Bibi alikuwa binadamu (mtumishi) aliyekuwa anahudumia jamii hiyo kwa maelekezo ya Kolero mwenyewe.
Waluguru na jamii zao, Wazaramo, Wakutu, Wakwere, Wakami nk, walifika mahali hapo kufanya ibada.
Walienda kuomba, maombi binafsi na pia maombi kwa jamii zao.
Bibi ambaye ndiye aliyekuwa msemaji wa Kolero aliteuliwa na Kolero mwenyewe kutoka kwenye maeneo yake ya kiutawala.
Bibi aliteuliwa vipi, aliishije, aliishi wapi?
Tukutane kwenye uzi maalum unaohusu Mzimu wa Kolero ambao nitauleta hapa Inshaallah tukijaaliwa.
Ahsante Mkuu,naomba ukileta huu uzi unitag
 
Back
Top Bottom