Kabidhi Wasii Mkuu aivunja Bodi ya Udhamini ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania

KISHINDO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
2,202
Reaction score
1,957
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Wadiventista Wasabato Tanzania kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kubaini Bodi hiyo kushindwa kusimamia ipasavyo mali na majukumu yake na hivyo kutoa siku saba kwa uongozi wa kanisa hilo kuwasilisha majina kumi (10) ya waumini watakaopendekezwa kuwa wajumbe wapya wa kamati ya mpito itakayosimamia mali za kanisa hilo hadi itakapopatikana Bodi mpya ya Wadhamini.

Bw. Kanyusi ametoa agizo hilo hii leo Februari 24, 2026 Jijini Dar es salaam wakati wa kupokea ripoti ya ukaguzi maalum wa kiuchunguzi wa mali za Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kufuatia malalamiko yalivyowasilishwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo katika ofisi ya kabidhi Wasii Mkuu na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi wakilalamika kuwepo kwa ubadhirifu wa mali za kanisa na matumizi mabaya ya madaraka.

Bw. Kanyusi amebainisha kuwa, taarifa hiyo ni hatua muhimu iliyochukuliwa kwa kushirikiana na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa kutoka wizara ya mambo ya ndani kuamua kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kiuchunguzi ili kujiridhisha na usahihi na ukweli wa malalamiko yaliyowasilishwa na waumini wa kanisa hilo.

Bw Kanyusi ameongeza kuwa, taarifa hiyo itafanyiwa kazi kwa haraka na kuwasilishwa kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi ili wale wote waliobainika katika taarifa ya CAG kuhusika na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na mali za taasisi hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa amesema kuwa ofisi yake ilipokea malalamiko kuhusu viongozi wa kanisa hilo kutowajibika katika kusimamia majukumu yao hivyo kuwasiliana na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ili kuchukua hatua za haraka kwa upande wa wajumbe wa bodi za wadhamini na viongozi watendaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania.
 
WASABATO NI DHEHEBU PEKEE ILIYOKUWA MFANO KWA MADHEHEBU YA KIKRISTO.SAHIVI NAO WAMEKUWA WAPIGAJI
 
Huko wanakula bila kunawa hata mikono. Huku kwetu je, nako wanaenda kukagua au huwa wanashibishwa mkate na mvinyo?
 
Kwanza kulikuza jina la kanisa kuliko kulikuja jina la Kristo ni kosa sana.
Wasabato wanatukuza usabato kuliko kumtukuza Kristo.
Lazima Mungu awaumbue.
Imefika wakati viongozi wajue
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Wadiventista Wasabato Tanzania kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kubaini Bodi hiyo kushindwa kusimamia ipasavyo mali na majukumu yake na hivyo kutoa siku saba kwa uongozi wa kanisa hilo kuwasilisha majina kumi (10) ya waumini watakaopendekezwa kuwa wajumbe wapya wa kamati ya mpito itakayosimamia mali za kanisa hilo hadi itakapopatikana Bodi mpya ya Wadhamini.

Bw. Kanyusi ametoa agizo hilo hii leo Februari 24, 2026 Jijini Dar es salaam wakati wa kupokea ripoti ya ukaguzi maalum wa kiuchunguzi wa mali za Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kufuatia malalamiko yalivyowasilishwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo katika ofisi ya kabidhi Wasii Mkuu na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi wakilalamika kuwepo kwa ubadhirifu wa mali za kanisa na matumizi mabaya ya madaraka.

Bw. Kanyusi amebainisha kuwa, taarifa hiyo ni hatua muhimu iliyochukuliwa kwa kushirikiana na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa kutoka wizara ya mambo ya ndani kuamua kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kiuchunguzi ili kujiridhisha na usahihi na ukweli wa malalamiko yaliyowasilishwa na waumini wa kanisa hilo.

Bw Kanyusi ameongeza kuwa, taarifa hiyo itafanyiwa kazi kwa haraka na kuwasilishwa kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi ili wale wote waliobainika katika taarifa ya CAG kuhusika na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na mali za taasisi hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa amesema kuwa ofisi yake ilipokea malalamiko kuhusu viongozi wa kanisa hilo kutowajibika katika kusimamia majukumu yao hivyo kuwasiliana na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ili kuchukua hatua za haraka kwa upande wa wajumbe wa bodi za wadhamini na viongozi watendaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania.
Nilibatizwa kwenye usabato na nikawa active sana enzi hizo nikiamini wachungaji wa kisabato ni watumishi wa kweli wa Mungu.
NIlianza kujiuliza upya nilipomsikia mchungaji Mwasomola enzi zile akisema toa zaka hata kama unafanya biashara ya bangi..kwa kweli hapo nilianza kujiuliza iwapo niko mahali sahihi au nifanye mambo yangu tu.
Hivi karibuni namsikia mch huyo huyo analaani wanaotoa zaka kutokana na kazi zisizo halali.
Nilichojifunza mafundisho ya utoaji yanaambatana na vitisho vingi kiasi kwamba injili haihubiriwi tena bali tamaa za mali za washiriki.
Hakuna mtu anaweza kukueleza kwa nini wachina na waarabu wanakuwa mabilionea na si wasabato wala wakristo na kwa nini Mungu alaani watu weusi tu kwa kutotoa zaka.
Mwisho wachungaji waache ubinafsi na upendeleo huku mapato ya kanisa wakiyatumia kifisadi.Tunajua wengine humo ni wachawi kabisa na wanashika nyadhifa kubwa tu kanisani
 
Kanisa lina mali nyingi kama shule, hospitali, Vyuo, lakini faida yake hata haionekani.

Maana hata kujenga tunakamuana wenyewe, tena wanatudanganya kujenga makanisa makubwa yanayotuzidi uwezo.

Kama huamini anza kupita kwenye makanisa ya wasabato. Kati ya makanisa 10 basi lililokamilika ni moja au hakuna kabisa na hii ni kila mahali.
 
Bado kkkt na RC, Islamic Foundation, Bakwata, ahmadia, Aghakan etc ..

Hizi taasisi za kidini zote ni corrupted, sema waumini wao ndio mazombies.

Hawa RC Kuna kipindi walikutana na PM wajaliwa wakimuomba serikali isichunguze Mali zao
 
Nimesikitishwa sana na hii habari ya wasabato. Kwangu mimi wasabato ni watu wema sana ukilinganisha na wakristo wengine. Miaka mingi iliyopita nikiwa nimepigika vibaya mno kiuchumi niliponea wa wiki nzima msosi wa wasabato kwenye sherehe zao za makambi pale kanisa la mjini kati Arusha jirani na shule ya Winning. Toka wakati huo huwa ninajihisi nina deni kwa wasabato. Kuhusu kinachowasibu ninawaombea kwa Mungu awavushe salama bila kuleta mgawanyiko. Ikumbukwe kanisa la wasabato ndo kanisa lisilokuwa na upande wowote kwenye siasa za nchi hii.
 
Kwanza kulikuza jina la kanisa kuliko kulikuja jina la Kristo ni kosa sana.
Wasabato wanatukuza usabato kuliko kumtukuza Kristo.
Lazima Mungu awaumbue.
Imefika wakati viongozi wajue

Nilibatizwa kwenye usabato na nikawa active sana enzi hizo nikiamini wachungaji wa kisabato ni watumishi wa kweli wa Mungu.
NIlianza kujiuliza upya nilipomsikia mchungaji Mwasomola enzi zile akisema toa zaka hata kama unafanya biashara ya bangi..kwa kweli hapo nilianza kujiuliza iwapo niko mahali sahihi au nifanye mambo yangu tu.
Hivi karibuni namsikia mch huyo huyo analaani wanaotoa zaka kutokana na kazi zisizo halali.
Nilichojifunza mafundisho ya utoaji yanaambatana na vitisho vingi kiasi kwamba injili haihubiriwi tena bali tamaa za mali za washiriki.
Hakuna mtu anaweza kukueleza kwa nini wachina na waarabu wanakuwa mabilionea na si wasabato wala wakristo na kwa nini Mungu alaani watu weusi tu kwa kutotoa zaka.
Mwisho wachungaji waache ubinafsi na upendeleo huku mapato ya kanisa wakiyatumia kifisadi.Tunajua wengine humo ni wachawi kabisa na wanashika nyadhifa kubwa tu kanisani
Kuacha Imani kwa sababu ya matendo ya mtu au mchungaji ni uchanga wa Imani. In sawa na kukimbia shule kwa graduation ya chekechea.

Kesho utaacha kusoma biblia kwa sababu umengundua Daudi aliwahi kuzini na kuua alafu bado Mungu anamuita Daudi huyohuyo ni mkamilifu na mfano wa kuigwa.

Wasabato wanaojenga Imani katika wachungaji kama walokole siku sio nyingi Mungu ataruhusu waone mengi ili wajifunze ujinga wa kuamini viongozi badala ya aliyewaweka na kipngozi mkuu wa kanisa Yesu kristo.
 
Back
Top Bottom