Kaazi kweli kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaazi kweli kweli

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nyani Ngabu, Jan 5, 2012.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Haya watetezi wa ndoa na uvumilivu teteeni na hii!

  Jamaa kafumaniwa na mkewe. Jamaa anacheat na mke wa mtu! Halafu kuna watu bado wanaapia wanawake huwa hawacheat. It beats me how delusional some people are.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahaha. . . .
  Haya mambo ya kucheat sijui lini watu wataamua hata kupunguza.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,652
  Trophy Points: 280
  Binafsi siamini mwanamke YOYOTE!Naamini kuwa wanaume ni afadhali kuliko wanawake!
   
 4. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ebwana wee....yaani mie nilishajijuliaga hapa kuwa ukioa kupitiwa mbavuni ni lazima ssa cha msingi mie naweka vimada pembeni na kuenjoy navyo alafu hamna kuzaa na wife. ili siku nikifumania namtoa nduki haraka iwezekanavyo
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Inachekesha na kutia huruma. Mama wa watu kachitiwa na kudundwa kadundwa!

  It's a double whammy. Sasa hapo tuseme mume wa mwanamke anayecheat na jamaa naye awafumanie halafu naye adundwe vilevile....lol

  Oh boy...what has this world come to!?!?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  As bad as it may sound, I kinda agree with you.
   
 7. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sasa ungejiuliza kwanza reason gani mpaa iwafanye wa cheat.

  Si unajua baadhi ya wanaume ni malevi yakifika kitandani yanalala tu....mana yanazini hovyo nje.

  Ulisikia wapi mke wa Shekhe aka cheat....Mana wale wakitoka msikitini hawana kazi nyingine zaidi ya kufanya mchaka mchaka chumbani kwao.

  Babu yangu alikuwa anasema; Mwanamke kama anapenda kula nyama, basi aolewe na butcher man....Kama anapenda ulevi aolewe na mlevi mwenzie...Lakini kama anapenda kuchapwa na mpweke basi atafute masheikh hapo atakuwa kafikishwa.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nadhani hao cheaters wote wawili ndio wanaohitaji kipondo. Kumpiga huyo mama ni kumuonea, ila kama nae ni mmoja wa wale wanaosema "acha mume afanye atakayo alimradi asiniletee kimada ndani" basi hilo linatakiwa liwe fundisho kwake na huruma yangu simpi.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kucheat hakuna cha nani wala nani.

  Kwani sheikh akiwa msikitini mkewe hawezi kucheat? It only takes a matter of minutes and sometimes just seconds and it's all done and over with.

  I have seen enough to know not to put anyone past cheating especially in this day and age of the information superhighway. If you think certain types of people don't cheat then you are in for a rude awakening!
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  @Nyani Ngabu pole yake huyo anaeapia kuwa wanawake huwa hawacheat....mwambie atembee aweze kujionea, wanawake wa siku hizi wengi mishipa ya aibu imewakatika tena usishangae kusikia wanaongoza kwa kucheat...wanaume hawajifichi sana ndio mana wepesi kujulikana...


  @Lizzy wazee wetu wanasema ni afadhali ya enzi zao kuliko sasa..watu hawana aibu wala woga.
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Utaishi hivyo mpaka lini?
   
 12. G

  Geka Senior Member

  #12
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rudia tena!!!! Diwani afumaniwa na mke wa sheikh, ilikuwa ni kama tarehe ya leo mwezi huu mwaka 2010

  DIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tunduru amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mmoja wa masheikh mkoani hapa. Katika fumanizi hilo la aina yake, sheikh huyo alipigwa na butwaa baada ya kumshuhudia diwani huyo akiwa amejifunga kiunoni kitenge ambacho alimnunulia mkewe mara baada ya kubisha hodi.

  Tukio hilo limetokea juzi saa nane usiku baada ya mume wa mke huyo kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mkewe ameonekana katika nyumba ya diwani huyo (jina tunalo).
  Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, diwani huyo alikiri kutokea kwa fumanizi hilo lakini akadai kuwa ni njama zilizopangwa na washindani wake wa kisiasa ili kumchafua.
  Baadhi ya watu waliodai kushuhudia tukio hilo walisema kwamba mikakati ya kumfumania ilipangwa na majirani baada ya kuona mke huyo wa sheikh ameingia ndani kwa diwani huyo.

  Walidai diwani huyo ana tabia ya kula na wake za watu na hiyo imemjengea uhasama kwa watu wengi kiasi kwamba ilibidi watoe taarifa kwa sheikh huyo ili kumkomoa.
  Mara baada ya shehe kupata taarifa hizo aliongozana na mwenyekiti wa kitongoji cha Raha leo, Mkwanda Mussa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Kitani, Nyenje Madefu hadi nyumbani.
  Kwa mujibu wa mashuhuda hao, jopo hilo lilipofika kwenye nyumba walimokuwemo ndani na kubisha hodi, diwani huyo alifungua mlango akiwa amejifunga kitenge cha mke wa shehe huyo kiunoni na kuwataka waeleze shida waliyoijia.

  Walisema diwani huyo alipigwa na butwa na kuonekana kuwa na kigugumizi baada ya jopo hilo kumueleza kuwa limefika kumtafuta mke wa shehe waliyehisi kuwa yumo ndani.
  Kabla hajajibu lolote waliingia ndani na kumkuta mke wa sheikh akiwa amelala kitandani na ikawa ni ushahidi wa kumkamata diwani huyo hadi ofisi za kata ili kumhoji.
  Baada ya mahojiano ya muda mrefu, inadaiwa kuwa diwani huyo alikiri kosa la kulala na mwanamke huyo na ikaamuliwa alipe Sh300,000 kama faini kwa sheikh.

  Alifanikiwa kupata Sh150,000 na kuahidi kiwango kilichobaki atakilipa hara iwezekanavyo.
  Baadhi ya wakazi wa kata anayoongoza diwani huyo, walidai kuwa amekuwa akitumia wadhifa alio nao kwa ajili ya kula na wake za watu.

  Habari hii imeandikwa na Joyce Joliga, Songea

  Na: Yasinta Ngonyani kl
   
 13. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mpaka nitakapo kufa....kwani waliokuwa kwenye ndoa na kuwa cheated on wanaishi mpaka lini? sii mpaka wanakufa
   
 14. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Every married man wishes to have a good wife, I have never seen in my life Sheikh ameowa malaya (prostutor is prostutor).


  Mtu anaye toka nje ya ndoa ni malaya tu.

  Na hebu nipe hint wapi uliona mke wa sheikh anafanya hayo...Au unaongea tu.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Wewe ni sheikh nini?

  Haya hebu soma bandiko la Geka, bandiko namba 12.
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wewe unafurahia kuishi na mke bila kupata mtoto eti kisa unahisi anakucheat? Kama ni hivyo si bora usingeoa kabisa uendelee na vimada, mke wa nini sasa? Malengo yako ni nini?...
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nashindwa kuelewa mtu kama huyo ameoa ili iweje.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Jan 5, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kwani wanaooa na kuolewa halafu wanacheat walioa na kuolewa ili iweje?
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sifa labda.
  Wakati wangeweza wakabaki single na kutembea na yeyote aliye tayari bila presha za kujikagua kabla ya kuingia ndani na kuficha simu.
   
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kama wewe ni sheikh na mke wako hafanyi basi shukuru mungu...ila bado sio kigezo cha kukufanya wewe uamini kuwa wake wote wa masheikh hawafanyi. Kucheat ni tabia ya mtu haijalishi kaolewa na sheikh au mchungaji, na ukumbuke tabia haina dawa.
   
Loading...