Kaanzisha mahusiano mengine akiwa na mimba

Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,037
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,037 2,000
Wakuu habari ya asubuhi.

Moja kwa moja niende kwenye mada, huyu mwanamke nimekuwa naye kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa, kuna wakati alishika ujauzito, tukakubaliana kulea mimba hiyo, basi tukalea mpaka ilipofika miezi mitatu ndio balaa likaanza, yeye kutaka tuachane.

Kuna siku alikuja kunitembelea, alipofika akawa anachat sana na simu nikamuuliza vipi mbona uko busy na simu? Akanijibu "hata hivyo ni simu yangu" nilichukizwa na jibu hilo nikanyamaza, nikampa muda zaidi, nilivyoona kazidisha nikamnyang'anya hiyo simu nikaiweka pembeni, basi tukaendelea na mazungumzo, wakati simu yangu mimi iko pembeni ilipigwa na sms ziliingia ila sikupokea wala kusoma sms, baada ya muda nikasema ngoja niichungulie, nikajibu sms za muhimu kwa dakika chache, nikamrudia tukaendelea kuongea, tukamaliza tukaagana akaenda.

Alipofika nyumbani, akaniuliza hivi ulinionaje pale ulivyokuwa unajibu sms mimi nipo pale, nikamueleza vizuri kuwa nilijibu kuwa kuna ujumbe wa muhimu nilitumiwa, basi akaanza kusema hanitaki tuachane, sikumtilia maana nikihisi ni hali ya mimba, ila aliendelea kukaza msimamo wake, baadae nilikuta ameniblock njia zote, sms, calls whatsapp, njia zote za mawasiliano nikawa simpati, hiyo hali ikaendelea kwa week mbili.

Jana ndipo alinitumia sms ya kunijulia hali, nikamuuliza mustakabali wa mahusiano, akanijibu kuwa kashaanzisha mahusiano mengine, yana wiki moja, na amemueleza huyo mwanaume kuhusu mimba akakubali kuilea, nikamuuliza sababu ya kufanya hivyo endapo mimi mhusika wa mimba hiyo nipo na nimekubali kuilea akaniambia ni kwa sababu mimi hawezi kunitambulisha kwao kama baba wa mtoto, nikamueleza sio vizuri alivyofanya, nikamuuliza kuwa kuhusu suala la clinic akasema kuwa nikitaka nitampeleka au nisipotaka huyo jamaa atampeleka! akiwa katika mizunguko yake na huyo jamaa siku ya jumatatu nimpitie nimpeleke clinic.

Nikauliza kuhusu hatma ya mtoto alichonijibu kuwa mtoto atakuwa na baba yule atakayefahamika kwao kama baba mtoto na mimi nitakuwa kama baba mzazi, kitu asichoweza ni kunitambulisha kama baba mzazi wa mtoto na yule jamaa anafahamu hilo kuwa mimba ni yangu ila yeye ni mlezi, sasa wakuu niko njia panda.

Mtu aliyeamua kuwa nae ni doctor wa hospital ambayo nimekuwa nikimpeleka kwa ajili ya kucheck ultrasound scan, mwanzoni nilikuta mawasiliano yao akasema amemcheck kwa ajili ya issue za kiafya nikamzuia asiwasiliane naye, kumbe hakufanya hivyo aliendelea kuwasiliana nae kwa siri, ndipo imefikia mahali hapa.

Nifanyeje.
 
godimpare

godimpare

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Messages
1,998
Points
2,000
godimpare

godimpare

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2014
1,998 2,000
Don't take a serious every word from woman ,unauhakika kwamba anamtu mwingine? kama anae how you can prevent it? Cha msingi mtafute ukimkumbuka mtimizie anachokitaka, Fanya mambo yako ya muhimu,
 
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
1,674
Points
2,000
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
1,674 2,000
Pole sana. Huyo amekuona "Zoba". Wanawake akili zao za kushikiwa sana, sasa inaonekana weww ulikuwa unampeleka "kidemokrasia" sana, akawa anakuona ni zoba.

Hiyo mimba ni yako, na mtoto ni haki yako hawezi kukunyang'anya hiyo.

Wewe achana nae, ila mtoto atakapozaliwa nakushauri uweze kuongozana na mzee mmoja, uende kwa wazazi wake ukaeleze kilichotokea na kuwa yule ni mtoto wako; Ili aitwe na yeye tuone kama atakukana mbele ya wazazi wake....
 
Antonio de Guzman

Antonio de Guzman

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Messages
5,888
Points
2,000
Antonio de Guzman

Antonio de Guzman

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2016
5,888 2,000
Hatari sana mkuu na piga kimya temana nae maana mapenzi hayalazimishwi
 
bbade

bbade

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Messages
6,576
Points
2,000
bbade

bbade

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2013
6,576 2,000
Kuwa mvumilivu ujauzito unatubadilisha sana wanawake......
Subiria mtoto azaliwe ndio ufuate sheria.....

Kama kuhakikisha jina lako liko kwenye cheti za mtoto......mengine yatafuata.

Usiache kuhudumia kwa sasa....
 
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,037
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,037 2,000
Pole sana. Huyo amekuona "Zoba". Wanawake akili zao za kushikiwa sana, sasa inaonekana weww ulikuwa unampeleka "kidemokrasia" sana, akawa anakuona ni zoba.
Hiyo mimba ni yako, na mtoto ni haki yako hawezi kukunyang'anya hiyo.
Wewe achana nae, ila mtoto atakapozaliwa nakushauri uweze kuongozana na mzee mmoja, uende kwa wazazi wake ukaeleze kilichotokea na kuwa yule ni mtoto wako; Ili aitwe na yeye tuone kama atakukana mbele ya wazazi wake....
Sawa mkuu, ni kweli nimekuwa nikimpeleka kidemokrasia, wacha nitulie nione.
 
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,037
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,037 2,000
Devion

You will never handle a woman who cannot submit to you.

If you really love her, let her go! Let her be free, let her go. Give her what she wants.

Kumbuka, penye mto hapakosi samaki.
Sure bro you nailed it, hakika ni ngumu kuweza kumhandle.
 
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Messages
5,423
Points
2,000
zipompa

zipompa

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2014
5,423 2,000
kama ngekuwa mimi ile kufahamu ni yeye kanitafuta angechezea block, hakuna cha kutaka kujua zaidi alee mimba na huyo jamaa (kama yupo) kama ni mawenge ya mimba atajua yeye ila kifupi nisinge hangaika nae (mambo ya mtoto atalelewaje,sijui damu yangu yangekuja badae
 
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,037
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,037 2,000
kama ngekuwa mimi ile kufahamu ni yeye kanitafuta angechezea block, hakuna cha kutaka kujua zaidi alee mimba na huyo jamaa (kama yupo) kama ni mawenge ya mimba atajua yeye ila kifupi nisinge hangaika nae (mambo ya mtoto atalelewaje,sijui damu yangu yangekuja badae
Ilikuwa ngumu mkuu kupotezea akiwa na kiumbe, ambacho nina imani ni changu, ila hii ya sasa hivi naona imezidi kipimo.
 
Emery Paper

Emery Paper

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2019
Messages
640
Points
1,000
Emery Paper

Emery Paper

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2019
640 1,000
Dah ! Dunia ina watu wenye ujasiri. Yaani unamuacha mtu uliyedumu nae miezi kadhaa tena ukiwa na kiumbe wake kwa ajili ya mwanaume uliyekuwa nae kwa wiki tena ukiwa na kiumbe cha mtu mwingine tumboni.

Sioni huyu dada akiwa na mwisho mzuri. This i guarantee you. Atakuja kukulia when it's too late.
 
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,037
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,037 2,000
Kuwa mvumilivu ujauzito unatubadilisha sana wanawake......
Subiria mtoto azaliwe ndio ufuate sheria.....

Kama kuhakikisha jina lako liko kwenye cheti za mtoto......mengine yatafuata.

Usiache kuhudumia kwa sasa....
Daah kweli ujauzito unaweza kumfikisha mtu katika step hii? Basi kama ni hivyo hii ni hatari.
 

Forum statistics

Threads 1,335,545
Members 512,359
Posts 32,509,256
Top