Kaa kimya

Nakazia:

1. "Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na uovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili"
Mithali 10:19



2. "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu" Mhubiri 7:9



3. "... kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; Wala kukasirika" Yakobo 1:19



4. "Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa..." Mithali 17:27



5. "... kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa" Mathayo 12:37



6. "Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu" Mithali 17:28



7. "... mtu asiyejikwaa katika kunena , ni mtu mkamilifu..." Yakobo 3:2



8. "Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu"
Mithali 21:23
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…