JWTZ yaandaa mazoezi ya kijeshi ya pamoja EAC

Sir Lindege

Member
Sep 10, 2013
34
150
Dar es Salaam. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeandaa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa maofisa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Mazoezi hayo yaliyopewa jina ‘Ushirikiano imara’ yanawashirikisha wanajeshi na maofisa wa Serikali kutoka Tanzania, Uganda, Burundi, Kenya na Rwanda.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi, Brigedia Jenerali Alfred Kapinga amesema leo Jumanne Desemba 5,2017 kuwa watu 300 wanashiriki wakiwamo makamanda wa jeshi na maofisa wa juu kutoka wizara zaidi ya tatu ikiwamo ya Katiba na Sheria.

Amesema kwa Tanzania wanaoshiriki ni makamanda na maofisa watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Brigedia Jenerali Kapinga amesema kwa upande wa Tanzania washiriki ni 107 na kwamba, mazoezi yameanza jana Desemba 4,2017 na yatazinduliwa Desemba 7,2017 na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

“Mazoezi yanafanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Kunduchi, Dar es Salaam na yamejikita katika mambo makuu manne,” amesema.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni operesheni katika ulinzi wa amani; kupamba na ugaidi; kupambana na uharamia wa aina yoyote ndani ya Bahari ya Hindi; na majanga na maafa.

Amesema lengo la mazoezi hayo ni kuwaandaa na kuwapa uwezo washiriki katika kupanga na kutekeleza majukumu ya operesheni za ulinzi wa amani katika kupambana na ugaidi, uharamia na kukabiliana na maafa.

Brigedia Jenerali Kapinga amesema mazoezi hayo ni ya siku 17.

Chanzo: Mwananchi
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
149,713
2,000
IMG-20171205-WA0011.jpg
IMG-20171205-WA0010.jpg
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
11,743
2,000
nchi inahitaji... special force itakayo husika kimataifa na ndani ya nchi...kwa maslahi ya taifa bila kujari siasa.
Mbona wapo sikunyingi sana? Ni vile identity zao no classified. Hata operation ni classified thats why hamuwasikii.
 

AirTanzania

JF-Expert Member
Mar 17, 2011
1,139
2,000
Magaidi wanawalinda wapo Ikulu, JWTZ ni jeshi la CCM. Lipokimaslai zaidi. Viongozi wake wote wana kadi za CCM na wanazilipia. Wakistaafu huko wanakuwa wakuu wa Mikoa na wilaya, wengine wanapewa mpaka nafasi za ubalozi. JWTZ wanakula mpaka pesa za UN za wanajeshi wadogo wanaopelekwa Kulinda amani. Rushwa imeshamiri huko kama M/kiti wao kwenye chama chao
 

Jay master

JF-Expert Member
Dec 2, 2017
587
1,000
Magaidi wanawalinda wapo Ikulu, JWTZ ni jeshi la CCM. Lipokimaslai zaidi. Viongozi wake wote wana kadi za CCM na wanazilipia. Wakistaafu huko wanakuwa wakuu wa Mikoa na wilaya, wengine wanapewa mpaka nafasi za ubalozi. JWTZ wanakula mpaka pesa za UN za wanajeshi wadogo wanaopelekwa Kulinda amani. Rushwa imeshamiri huko kama M/kiti wao kwenye chama chao

Mkuu umetema nyongo, ,,,Ila Jeshi letu is best kabisa ,, tushauri tu labda wasiingizwe kwenye nafasi za kisiasa,,
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,633
2,000

Daah! video ndefu sana, dk 20 kwa huu usawa wa uncle JPM ni kutiana umasikini.

Itapendeza kama JWTZ wakiwa wanafanya mazoezi zaidi na majeshi ya Marekani, Israel, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Urusi, na China.

Nchi hizo ndo wanaojua kuwashugulikia MAGAIDI vilivyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom