JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
617
JWTZ wanakutana na waandishi wa habari muda si mrefu na inatarajiwa kurushwa na TBC1.

JF will be represented.

============
UPDATES:

Jenerali Mwamunyange hakuweza kuitoa bali imetolewa na Mkuu wa Usalama Jeshini (Brig. Gen. Paul Meela) akiwa na maofisa kadhaa.

Anasema NI MAPEMA MNO kujua chanzo cha milipuko hii na si vema kubashiri.

Anasema "Hakuna Atakayejiuzulu, Jeshi si Nafasi za Kisiasa"

Attachment chini inaonyesha Report nzima kama ilivyosomwa.

meela-paul.jpg

kikosi.jpg

Brig. Gen. Meela Mkuu wa Usalama na Utambuzi Jeshini

presentation-blasts.jpg

Meela akieleza kwa kutumia Power Point
gongo-ramani.jpg


Picha kwa msaada wa Google:

gongo-google.jpg
 

Attachments

Mwamunyange anatangaza kujiuzulu au!? Mwambieni hilo ndilo tunataka kusikia kutoka kwake na sio longolongo.
 
kuhusu nini mkuu tu juze sie tyupo oficin je ana jipya kujiuzulu tu
 
tusitegemee lolote.cheo chenyewe cha kupewa na JK hawezi kua na jipya
 
Hakutakuwa na lolote la maana hapo.....usanii mtupu.Rais msanii,wasaidizi wasanii,wananchi wasanii......kila kitu!
 
Huyu jamaa na mwenzake Mwinyi wanasubiri nini? TBC1 kufanya nini? wanatakiwa wawe wameshaondoka madarakani, anatuongezea hasira na simanzi ya wapendwa wetu waliotutoka kwa uzembe wa watu wachache.
 
Hawa jamaa inabidi ifike mahali waache kutuona sisi wendawazimu!! Hapo atatoa blabla tu hamna chochote. We need to look for permanent solutions to many problems we have. I always believe the main problem is with the government aka viongozi wetu. Lakini tunarudi pale pale uzembe na ubinafsi umekithiri. Ila zaidi walishatuona sisi walevi!! nao wamelewa!!
 
Waandishi na JF mtakaokuwepo mumuulize maswali kwanini hajajiuzulu na waziri wake?
 
Kama jambo limeshazungumziwa na Amiri Jeshi Mkuu ambaye yuko juu ya Mkuu wa Majeshi kuna haja gani ya jambo hilo hilo kuzungumziwa na mtu wa chini yake?

Hata hivyo kwa sasa uhuru wa habari umeminywa sana na mgao wa umeme. Ni aibu mtu kama mimi nimejua kuna milipuko kupitia mtandaoni. Yaani BREAK NEWS sikuzipata hata habari za jana asubuhi sikuzipata hadi nilipoingia ofisini.
 
Natoka nje ya mada.

Hebu tujaribu kufuatilia mlolongo wa mambo ambayo yametokea ndani ya miaka kama 5 iliyopita hadi sasa. Inabidi tuone uchungu sana kwa maisha ya watanzania wenzetu walioporwa uhai na serikali, then tuone uchungu kwa hela zetu kuchezewa hovyo.

Hayo mabomu yaliyolipuka hovyo ni hela zetu, pesa zitakazotumika ina one way or another katika operation yote na ukarabati wowote jeshini na kwa wananchi ambao nyumba zao zimebomolewa ni hela zetu. Hizo rambirambi serikali itakazotoa pia ni kodi zetu. Tuna haki ya kuhoji sana. Na hapa simaanishi wafanyakazi au wakulima tu.

Wote kwa pamoja wakulima na wafanyakazi tunalipa kodi kila mtu kwa nafasi yake. Ni haki yetu ya msingi kuhoji!!!
 
Waandishi na JF mtakaokuwepo mumuulize maswali kwanini hajajiuzulu na waziri wake?
Kama Mkwere mwenye jana hajatamka lolote kuhusu waliousika na uzembe we unategemea wao waseme nini?
 
Huyu jamaa hana la kutueleza, nahisi huko jeshini kuna ishu amabzo haziendi fresh, niliwasikia baadhi yao wakilalama kuwa jamaa hawajali kivile yaani mslahi yao yanabanwa, soo inawezekana ndio wameamua kulipua maghala ya mabomu wakitaka Mwamunyange ajiuzulu.
 
Hapa kweli rais ilibidi atuambie kosa ni la nani. Kwa hakika lazima awepo mwenye kosa hapa. Hata kwenye kampuni au shirika lolote inapotokea kasoro fulani inajulikana hiyo inamhusu nani. Hapa inamhusu nani? mambo kama haya yanatakiwa kuwa wazi na ndo maana ilitakiwa watu wajiuzulu hapa kwani kazi wameshindwa! au wanaJF mnaonaje?
 
Kama jambo limeshazungumziwa na Amiri Jeshi Mkuu ambaye yuko juu ya Mkuu wa Majeshi kuna haja gani ya jambo hilo hilo kuzungumziwa na mtu wa chini yake? Hata hivyo kwa sasa uhuru wa habari umeminywa sana na mgao wa umeme. Ni aibu mtu kama mimi nimejua kuna milipuko kupitia mtandaoni. Yaani BREAK NEWS sikuzipata hata habari za jana asubuhi sikuzipata hadi nilipoingia ofisini.
Kama CDF anazungumza baada ya amiri jeshi mkuu, then sijui ni nidhamu ya jeshi gani hilo
 
Uongozi wote wa CCM unastahili kuondoka....kuanzia JK na wasaidizi wake wote
 
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange anakutana na waandishi wa habari muda si mrefu na inatarajiwa kurushwa na TBC1. JF will be represented

umeme umekatika majumbani nani atafuatilia anachoongea TBC1, hata hivyo watu hameshachoka na longo longo za watendaji wa serikali hii hawasemi ukweli.

Ya Arusha - longo longo
Ya Mbagala - Longo longo
Umeme - Longo longo
Na hili la Gomgolamboto - ni longo longo tu - subirini amalize kuongea mchuje hoja zake.

Shida kubwa watanzania wenzangu.
 
We halisi... mbona huyo mkuu wa jeshi hajaongea na hadi sasa ni nusu saa imepita? au soon in sswahili means later?

BTW, nimeona leo saa saba wanahangaika kweli kutokea kawe na lugalo lakini hawakwenda ikulu nadhani waliishia masaki... magari ya jeshi yalikua mengi kuanzi malori, land rover hadi zile pickup zao na taa za hazard
 
Back
Top Bottom