JWTZ miongoni mwa majeshi bora Afrika

JWTZ miongoni mwa majeshi bora Afrika

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
nembo.jpg

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo mwezi huu limetimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Septemba Mosi, mwaka 1964, limetajwa kuwa miongoni mwa majeshi bora na yenye weledi, uzoefu na ujuzi mkubwa wa mapambano katika Bara la Afrika na nje ya Bara hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es Salaam jana, imekitaja Kikosi cha Majeshi Maalum (Special Forces) cha JWTZ kinacholinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa miongoni mwa vikosi bora 30 vya majeshi maalum duniani kwa mafunzo, uwezo na weledi.

TPDF lilihitimisha sherehe za miaka 50 ya uhai wake kwa Onyesho la Medali la Operesheni Maliza Matata lililofanyika kwenye eneo la mafunzo la Jeshi hilo la Langururusu, Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha, ambako Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu, alikuwa mgeni rasmi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo katika miaka yote 50 ya uhai wake, si tu kwamba JWTZ imetekeleza ipasavyo malengo na shabaha zake za msingi kikwelikweli, lakini pia limebakia jeshi imara, lenye uzalendo, lenye utii na nidhamu ya hali ya juu.

"Hizi ni sifa ambazo mataifa mengi hususan katika Afrika zimeshindwa kufanikisha, tunaweza kusema kwa uhakika kabisa kuwa amani, utulivu na usalama wa nchi yetu katika miaka yote 50 umechangiwa sana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania," ilieleza taarifa hiyo ikimnukuu Rais Jakaya Kikwete.

Alieleza kuwa JWTZ limelinda ipasavyo mipaka ya Tanzania na uhuru wake kwa vitendo kwa kuyapiga na kuyasambaratisha kabisa majeshi ya uvamizi ya Idd Amin wa Uganda katika vita ya 1978/79 ambalo kwa mara ya kwanza jeshi la nchi moja limelipiga kabisa jeshi la nchi nyingine na kulifuta kabisa. Shughuli hii iligharimu maisha ya wanajeshi wa Tanzania.

JWTZ limeshiriki kikamilifu kufanikisha harakati za ukombozi barani Afrika kwa kufundisha majeshi ya vyama vya ukombozi, kushiriki moja kwa moja kwenye vita vya ukombozi Kusini mwa Afrika na kuchangia kupatikana kwa uhuru wa Angola, Msumbiji, Zimbabwe, Namibia na Afrika Kusini. Kama ilivyokuwa vita dhidi ya Amin, vita vya ukombozi pia viligharimu maisha ya baadhi ya askari wa TPDF.

Jeshi hilo, limeendelea kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani duniani na kupata mafanikio makubwa kwenye operesheni za kulinda amani katika Liberia, Darfur (Sudan), Lebanon, Ivory Coast, Visiwa vya Shelisheli, Visiwa vya Comoro na sasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako majeshi hayo yamekiangamiza kabisa kikundi cha waasi wa M23.

Wanajeshi wa JWTZ wameshiriki kikamilifu kwa kushirikiana na mamlaka za kiraia katika uokoaji na maafa hususan majanga yakiwemo – ajali ya Mv. Bukoba, ajali ya meli Zanzibar, mafuriko ya Kilosa, Morogoro, ambako Jeshi lilitengeneza hata reli iliyokuwa imezolewa na mafuriko hayo.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi limeendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii katika sekta za elimu na afya. Watanzania wengi wamenufaika na shule na hospitali zinazomilikiwa na kuendeshwa na Jeshi katika maeneo mbalimbali nchini.

Kupitia JKT na JKU, Jeshi la Wananchi limekuza na kuendeleza elimu ya kujitegemea kwa vijana wa Tanzania.

CHANZO: Majira
 
tuwaombee wanajeshi wetu afya njema na lidumu milele,ameen

Kama ni sifa za kweli haya, ila inaonekana kama ni sifa ili majeshi yetu yakiambiwa yaende kwenye vita sehemu nyingine yaende kwa ajili ya kusaka sifa za kijinga. Ni vyema majeshi yetu kwa sasa wakati wa amani wangetumika kujenga nyumba za gharama nafuu kuliko hizi zinazojengwa na N.H.C lakini wananchi wanaozimudu ni wachache. Hii ingekuwa na tija sana kuliko hizo sifa za kwenda kwenye nchi za watu wakati kwenye sekta kama za madini wazungu ndio wanakuja kujichukulia sisi tunasifiwa kwa kwenda kwenye vita.
 
Unategemea ulindwe bure, ujengewe nyumba bure, ulishwe bure,kodi hulipi, wewe ni kubweteka , kula kulala na kujaza septic tank!!
Amka sasa na ujifanyie hayo unayoyasema!!!
 
Kama ni sifa za kweli haya, ila inaonekana kama ni sifa ili majeshi yetu yakiambiwa yaende kwenye vita sehemu nyingine yaende kwa ajili ya kusaka sifa za kijinga. Ni vyema majeshi yetu kwa sasa wakati wa amani wangetumika kujenga nyumba za gharama nafuu kuliko hizi zinazojengwa na N.H.C lakini wananchi wanaozimudu ni wachache. Hii ingekuwa na tija sana kuliko hizo sifa za kwenda kwenye nchi za watu wakati kwenye sekta kama za madini wazungu ndio wanakuja kujichukulia sisi tunasifiwa kwa kwenda kwenye vita.
Kujenga nyumba za bei nafuu si moja ya majukumu ya JWTZ ni kazi ya NHC, labda tukitaka tuanzishe utaratibu wa kila idara na mashirika yote ya umma yanayofanya vibaya yawekwe chini ya JWTZ halafu tuone matokeo yake. Ktk majukumu yake JWTZ inafanya vizuri ila kinachokera ni kuwa hizi taarifa zinazotolewa tunazifahamu na mpaka hazina mvuto tena, sasa sijui anayezileta tena ana lengo gani. Tupewe taarifa mpya juu ya maendeleo ya JWTZ lakini pia si mbaya tukiletewa pia taarifa ya maendeleo ya polisi na mipango yao kuelekea kuijenga Tanzania yenye ustawi. Kutokana na ukweli kuwa taasisi ya JWTZ inafanya vizuri basi watu wanataka kuficha uozo wa taasisi zingine za ulinzi kwa kuleta taarifa za JWTZ hata zilizopitwa na wakati ili watu wapunguze stress zinazotokana na kushindwa kwa polisi kutekeleza majukumu yao kisheria na kwa ufanisi.
 
Inasikitisha Hii taarifa nimeiona weka sawa Kati ya Majeshi 20 Bora Tanzania HAIMO, Tumezidiwa hata na Zimbabwe, Sudan, Kenya, Uganda D.R.C,Angola wa kwanza Egypty .
 
nimewahi kusikia walikuwa na mradi wa kuunga magari alimaarufu "NYATI "Nani anjua hatma yake?
 
Wewe ni tindo kama lilivyo jina lako, kama huma na kuchangia ni bora ukasema na kupita......usituchanganyishie mada hapa
 
Taarifa ya Ikulu lazima iseme jeshi ni bora, ulishawahikuona wapi Taifa linasema Jeshi langu ni weak kuliko majeshi yote? Hata hivo ni vema kupima Jeshi letu kwa kuwatizama wapiganaji tunaoishi nao huku mitaani, je wana afya bora, wanamorali ya kazi, wanahudumiwa vizuri? kuna mipango yoyote ya kuwafanya wanajeshi wetu wakahusika na innovations za kisayansi zaidi ya mazoezi ya ukakamavu? au wanakaa kufanya mazoezi ya viuongo kujenga misuli? dunia imebadilika ulinzi sasa ni digital, enemies have drones we have masular soldiers! can they fight a drone? anyway just thinking aloud may be we have what we need.
 
Kwani changamoto zinazolikabili jeshi letu mbona sijaziona?
Kwa mfano miaka ya hivi karibuni kumetokea milipuko ya mabomu kule mbagala na gongo la mboto lakini sijapata kusikia wala kuona chanzo chochote cha habari kikieleza matukio hayo yalisababishwa na nini?
Pengine ni siri kutoa taarifa za kijeshi lakini hata wahanga walioumizwa na milipuko, wakapoteza makazi na kupata hasara za kila aina bado hata serikali inawalipa fidia isiyotosha kununua hata kilo mbili za unga wa dona/sembe, kuna mtu amelipwa 1,950TZS kama fidia jamani.
Naona hii taarifa ni nzuri kwa kuisoma lakini imekaa kisiasa tu kwa kuzingatia wakati tuliona nao ni wakati wa uchaguzi 2015.
 
Nikiona thread imekaa kwenye jukwaa la siasa, naaza kuwa na mashaka na mtu aliyeiazisha.

Kwamba ni kibaraka wa CCM, wanataka kujiosha.
 
Inasikitisha Hii taarifa nimeiona weka sawa Kati ya Majeshi 20 Bora Tanzania HAIMO, Tumezidiwa hata na Zimbabwe, Sudan, Kenya, Uganda D.R.C,Angola wa kwanza Egypty .

Mkuu. Bayebe mambo mengine na wewe utumiage akili za kuzaliwa hata kama hujaenda shule,au hata bila kusoma hzo ripoti za wazungu..

Hivi na wewe kwa akilibzako kweli D.R.C,Sudan na Uganda wametuzidi.!!
Hata Zimbabwe wenyewe wametuzid Jeshi la Anga tu..
 
Last edited by a moderator:
Watu wakikaa kwenye keyboard wanaropoka wanavyojisikia.

Nani hajui operation za JWTZ Afrika na Duniani kwa ujumla.

Pamoja na mapungufu yake Lakini JWTZ ni kati ya majeshi bora kabisa barani Afrika, na ni kati ya Majeshi machache yenye midhamu.

Pamoja na operation zote za JWT funga kazi ni kwa M23 muulizeni Kagame mpaka leo haamini kilichotokea kwenye misitu ya Kongo pamoja na kuingiza jeshi lake kwa mgongo wa nyuma.
 
Taarifa ya Ikulu lazima iseme jeshi ni bora, ulishawahikuona wapi Taifa linasema Jeshi langu ni weak kuliko majeshi yote? Hata hivo ni vema kupima Jeshi letu kwa kuwatizama wapiganaji tunaoishi nao huku mitaani, je wana afya bora, wanamorali ya kazi, wanahudumiwa vizuri? kuna mipango yoyote ya kuwafanya wanajeshi wetu wakahusika na innovations za kisayansi zaidi ya mazoezi ya ukakamavu? au wanakaa kufanya mazoezi ya viuongo kujenga misuli? dunia imebadilika ulinzi sasa ni digital, enemies have drones we have masular soldiers! can they fight a drone? anyway just thinking aloud may be we have what we need.
Umeeleza vizuri ila mwishoni umeshangaza kulinganisha nchi kama yetu na Marekani hasa ulipotaja innovation na Drones. Tena sio ktk mambo ya kijeshi tu bali hata kazi yako unayofanya au biashara au chochote ulichonacho wewe huna jeuri yakujilinganisha na Taifa kama lile.
 
Back
Top Bottom