Bi. Kiroboto
Member
- Dec 22, 2011
- 36
- 6
Kuna kakitu kanaitwa Banjuka kwenye matumizi ya internet ya TTCL kamenifanya niibiwe mchana kweupe na kampuni hii. Wanasema wanatoa unlimited bundles: Tsh 1000/hr kuanzia saa 12 asbh - 12 jioni, Tsh 800/hr saa 12j ioni - 3 usiku na Tsh 500/hr kuanzia saa 3 usiku - 12 asbh. Kiukweli nilivutiwa sana, nikanunua modem yao nakuanza kutumia. Wizi ulianzia pale nilipoanza kudownload nikakuta speed inashuka hadi 0.15kbps wakati waliniambia speed yao inafika 3Mbps. Kiukweli max. downloading speed niliyoona hapa ni 70kbps tena mara chache sana. Kiukweli saa inakatika ukiwa hujafanya lolote la maana.