Juzi Kikwete mlimmiss leo mnamgeuka

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
Watanzania tuna unafiki wa hali ya juu na kuishi kama bendera fuata upepo
Tangu mwaka huu uanze umekua wa matukio linatoka la Bashite linaingia la Vyeti feki linatoka la Vyeti feki na sasa limeingia la Makinikia ya Dhahabu

Nakumbuka wakati Bunge linaanza Rais mstaafu alienda bungeni akashangiliwa Sana na wabunge kumwambia wamemmiss, hata Kwa upande wa wananchi nao mitaani wanadai wamemmiss JK kutokana na utawala wake kudai maisha yalikua Rais

Hivi majuzi limeibuliwa suala la mchanga wa dhahabu na kushtumu tawala na viongozi waliopita ndio walioshirikia kusaini mikataba mibovu na tawala hizo ni za awamu ya 3 na 4 ,Ila hii ya 4 ndo inaonekana ina makosa,Yule waliemwambia wamemmiss leo wanamponda akisafiri Sana kwenda kusaini mikataba mibovu

Tayari serikali hii imeshatutoa kwenye suala la kufikiria ugumu wa maisha na kupanda Kwa bei ya bidhaa, uchumi kudorora, vyeti feki na Bashite na tumegeukia kwenye suala la mchanga hii ni sawa na bendera fuata upepo.

Jamaa washachimba sana madini tunakuja kuvuta shuka kumekucha halafu mtu anasifia sifia tu eti bora kawabana

Tatizo la nchi yetu ni mfumo mbovu wa kiutawala na sheria nyingi za kulinda rasilimali zetu ni mbovu na nchi hii sidhani kama ina dira kila kiongozi akija anakuja na Sera zake ambazo kimsingi zinachelewesha maendeleo
 
Wakulaumiwa ni akina CHENGE ambao ndio watu wa sheria wanaohusika na kusaini mikataba na kuishauri serikali mambo ya kisheria,huwezi kujua kama jambo la kweli au uongo kama hauna elimu juu ya hilo jambo.Mtu kama CHENGE ni wakunyongwa tu.Kibaya zaidi wabunge ndio wanafagilia mikataba mibovu ikipelekwa Bungeni kwaajiri ya maslahi ya matumbo yao tu.Wanasheria ni watu wa hovyo sana ni mijitu ya rushwa kwenda mbele,hivi wanasheria wakiingiza serikali kwenye mikataba mibovu Rais atalaumiwaje kwakitu ambacho hakijui ila ametoa uamuzi kwaushauri tu wa mwanasheria mkuu wa serikali?

#JK hana hatia
 
Kila mtu ana mazuri na mabaya yake mkuu kwa hiyo usishangae, ndio binadamu tulivyo..Leo watakuchekea kesho watakununia
 
Back
Top Bottom