Juventus Special Thread

Half time
Juventus 0-1 Madrid.

Dybala kaenda mapumziko na kadi ya manjano.

Mpira bado mgumu kila timu inanafasi ya ushindi leo.
 
Paulo dyabala atolewa kwa kadi ya pili ya manjano 65'.

Juventus wabaki pungufu uwanjani.

Miujiza hapa tu Kama ya moses kutawanya bahari ya shamu ndio itawasaidia kuibuka na ushindi leo hii.
 
Watu wengi hudai Marefa wengi huzibeba timu kama real Madrid na Barcelona lakini hili linahitaji mjadala mpana.
 
72' Marcelo Juventus 0- 3 Real Madrid.


Sasa kinachofatia hapa ni kipigo cha kudhalilishwa.
 
Full time:
Juventus 0- 3 Real Madrid.

Watoto wa mjini wanaita tatu bila tatu bila tatu bila wamebana wameachia.
 
Mtangazaji mmoja anasema goli la CR 7 litazungumziwa miaka 100 ijayo hili sijui ni kweli.Ronaldo na Messi hawa siyo watu
 
Mechi ilikuwa nzuri sana japo kadi nyekundu ilidhoofisha ushindani kwa wakati flani.


Real Madrid wamestahili ushindi wa mechi ya leo.

Sasa Juventus anamlima mkubwa pale Santiago bernabeu!!

Aliyeshinda na apongezwe hongera Real Madrid.

Mpira ni burudani Mpira ni furaha.

Usiku Mwema wote wapenda soka..One nation,One love,One Tz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom