Mwambelamwanitu
New Member
- Aug 24, 2025
- 1
- 1
Habari zenu wana Jamii
Kuna fursa kubwa inaonekana ipo kwa serikali au private sector kuwekeza na wananchi wakanufaika. Ukiangalia huwa kuna space kubwa na pana inapatikana juu ya Barabara za mabasi ya mwendo kasi plus zile Barabara za njia mbili kila upande za kupita magari ya kawaida.
Sasa what if zikijengwa nguzo kubeba barabara za juu za kulipia (express way) juu ya ile space inayopita Barabara za mabasi ya mabasi ya mwendo kasi na zile Barabara za njia mbili kila upande za kupita magari ya kawaida?
Yaani barabara za juu zifuate stream ile ile ya mabasi ya mwendo kasi mfano kutoka kibaha kupitia kimara to Ubungo then posta, ingine kutoka Bunju/Tegeta kupitia Mwenge then to Posta na branch ingine inaenda hadi ubungo.
Na pale Ubungo kunakuwa na interchange kubwa yenye tawi lingine linaloenda hadi airport huko au Gongo la mboto. Na makutano mengine makubwa kama Mwenge, Morocco, Magomeni, n.k. pia zijengwe interchange za juu kubwa kuruhusu flow ya magari bila kupoteza muda.
So inakuwa hivyo na kwa network zingine za Barabara za mabasi ya mwendo kasi pia.
Faida Zake:
Au pengine huko mbeleni njia ya mabasi ya mwendo kasi ibadilishwe na kutandikwa reli nyepesi kwa ajili ya tram ya umeme wakati pendekezo la kujenga express way za juu za kulipia lizingatiwe ili kukidhi hitaji hilo linalokosekana.
Asanteni, na mawazo zaidi yanakaribishwa kuliboresha wazo hili tukiamini wahusika upande wa serikali kama Waziri wa Ujenzi na ndugu Kafulila watazingatia andiko hili kwa vitendo na wabunge walichukue pia kulipigia chapuo.

- Itasaidia sana kupunguza foleni na misongamano barabarani sababu kuna Kundi kubwa la watu wenye kipato cha kuweza kulipia hizo Barabara huku wakiwa na uhitaji wa kuwahi kwenye majukumu yao watakuwa wanachagua kulipia hizo Barabara na kupunguza stress na foleni pia kwa watumiaji wa Barabara za kawaida wasiokuwa na haraka au uwezo wa kulipia hizo express way. Mfano mtu ana Private Car anatoka huko ushuani kwake Bunju au Mbweni na anataka kuwahi majukumu yake posta au sehemu ingine anachotakiwa kufanya ni kuifikia tu hiyo main branch ya express way kisha ni kumwaga moto tu na kufika chap anakoenda.
- Ukiangalia eneo linaloelezewa hilo la juu ya ile space inayopita Barabara za mabasi ya mabasi ya mwendo kasi na zile Barabara za njia mbili kila upande za kupita magari ya kawaida yaani unaona kabisa ni uchumi ule umelala pale sababu huo ni mradi unaoweza ukawa unaingiza hela zake wenyewe kwa life time yake na ni rahisi hata kuvuta interest za private sector kuwekeza au kuchukua mikopo ambayo mradi wenyewe utakuwa unaurejesha huo mkopo.
- Mradi utakuwa umeongeza huduma ingine muhimu ya miundo mbinu ya kiusafirishaji kwa wananchi wake kwa mfano sasa kwa Dar es Salaam tuna hiyo option ya mabasi ya mwendo kasi ambayo imekuwa ni hatua muhimu na ya mbele kusaidia mahitaji ya usafiri wa haraka kwa wananchi wa kawaida. Lakini sasa unajiuliza vipi kwa mtu mwenye usafiri wake binafsi na anahitaji awahi kwa haraka kwenye majukumu yake au appointment zake za kibiashara? Hivyo express way za juu za kulipia zitaingia kusaidia kundi hili la wahitaji na kuweka balance ya mahitaji ya kiusafiri
- Dar es Salaam kwa sababu imejengeka na ni vigumu kupata nafasi ya kujiachia kujenga hizo express way then njia rahisi na ya kuepuka kulipa gharama zingine kubwa za fidia kubomoa structure zilizopo ni kujenga express way za juu kupita juu ya ile space inayopita Barabara za mabasi ya mabasi ya mwendo kasi na zile Barabara za njia mbili kila upande za kupita magari ya kawaida na ambayo mtandao wake tayari sasa hivi umeenda kwenye pande zote za kuingia na kutoka jiji la Dar es Salaam.