Just a friend na matatizo yake..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Just a friend na matatizo yake.....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Jan 31, 2012.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna ambao wanafanikiwa kuwa best friends au just friends
  huku ni jinsia tofauti bila kutokea matatizo ya
  wivu,mapenzi,sex na kadhalika?????

  kwa upande wangu naona ni ngumu saana

  siku zote naona kuna mmoja anakuwa 'anaumia' kwa chini chini.....

  je nyinyi mna uzoefu gani na hili??????????
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Kwa nini isiwezekane The Boss? akili yako ukiitwin kingonongono basi utamtamani hata Boss wako ofisini kwako kama ni mwanamke. akili za ngono zikikutawala unaweza hata ukakunja goti lako na ukalifananisha na utupu wa mwanamke!!
  Nina Rafiki alikuwa nawatamani dada zake kwa sababu wamenona, je kama una feelings za kijinga au come unaweza kumfeel dada yako wa damu kimapenzi?
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  umezungumza upande mmoja tu
  as if ni wanaume tu ndo wanashindwa kuwa 'just friends'

  na wadada pia hutokea wakashindwa pia
  na ikasababisha other effects......sijui hapo unasemaje?
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,260
  Trophy Points: 280
  Siwezi kuwa msemaji wao, wapo hapa na watasema wao wenyewe ni vigumu kwangu kufeel hisia zao kwa mwanaume zinabase kwenye nini!! maana kuna mdada aliwahi kuniambia anapenda sana utangazaji wa yule repota wa ITV ambaye umaliziagi kwa kusema Ni mimi Georgeeeeeeeeee Maratooooooooo wa I TEEEEEEEEEEEEVEEEEEEEEEEEEEEEEE!! U can imagine huyu mtangazaji mimi huwa akianza kutangaza tu ni lazim nibadilishe station maana sitaki hata kumsikia.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  h
  iyo ya tv ni tofauti

  mimi nazungumzia watu mliozoeana na kufahamiana tayari
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  inawezekana sana tu.nilikuwa nina rafiki yangu wa kiume,amini usiamini nilishibana nae hasa,sikuwa na feelings nae.nilikuwa namuona mshikaji tu.na kwa upande wake ni hivyo hivyo.ila alipopata girlfriend,urafiki nikaupunguza huyo dada asije akanifikiria vibaya.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Kwa kiasi kikubwa huo ndiyo ukweli!
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mwanamke na mwanamme wakiwa marafiki, at a certain point mmoja atampenda mwenzake na kuumia kimya kimya hadi atakapozoea.

  Kuna muda James atampenda Mary, wakati James keshazoea, Mary naye atampenda James.

  Hii hutokea mara nyingi japo sio sheria.
   
 9. Cyclone

  Cyclone Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This depends on the source of the friendship at the first place.kama ni marafiki na wote mkawa mpo single honestly you may turn up to be a wonderful couple, coz katika ndoa nyingi na mahusiano mengi yanahusisha watu ambao hawakuwahi kuwa marafiki, hii inawanyima fursa ya kusomana vizuri.Dating a friend not bad.

  kwa upande mwingine freindship btn opposite sex holds kama mmoja wenu au nyote mpo kwenye committed relation ship na third parties, na mkawa wazi juu ya hili., U wezekano mwiungine kama kila mmoja ana muona rafiki yake syo type yake hii pia inaweza ku hold.

  Otherwise time will come na mtajua kama ni friends tu au Friends with Benefits(FWB)
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwanza inawezekana sana.
  Kama hamna aliye attracted na mwenzake kuwa marafiki hakutobadilisha hilo. Mtapendana, mtaelewana, mtajaliana ila kila mmoja atapenda kwingine kimapenzi. Na hii ni kwasababu unaweza kumpenda mtu (fikra/mawazo/tabia yake/ushawishi wake) bila kuvutiwa nae kimapenzi.

  Pili Kama mmoja anavutiwa na mwenzake hata wasingekua marafiki bado upo uwezekano mkubwa tu kwamba angevutiwa nae, na kama uwezekano wa kuwa nae nao ungekuwepo basi wangekua pamoja. Sasa bora kipi. . . kufall inlove with your (best) friend, mtu ambae mnafahamiana zaidi ya watu wengine wavyofahamiana au mtu tu anaeibuka out of nowhere?

  Alafu kama hujagundua jaribu kuchunguza msichana na mvulana ambao ni marafiki wazuri/wa karibu sana huku wakiwa wana wapenzi wao. Utagundua kwamba kwa kiasi kikubwa wale wapenzi na bestfriend ni tofauti kabisa. Kama rafiki ni mchangamfu/mchokozi chokozi sana utakuta mpenzi ni mpole, kama mpenzi sio mtu wa movie/music kwa sana utakuta rafiki anapendelea. Kwa maana nyingine watu(sio wote) hua wanakua na marafiki wenye yale wasiyonayo wapenzi wao/yanayowavutia kua mpenzi na mtu ni tofauti na yanayowavutia kwenye urafiki. That way anatengeneza balance. . . akichoka kukaa nyumbani na kuboreka na mpenzi anamtafuta rafiki yake achangamke kidogo, akichoka na maneno mengi kwa mpenzi anamtafuta rafiki yake akili itulie kidogo.

  So ndio inawezekana kuliko ambavyo watu wanapenda kukubali.
   
 11. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  mi naona inawezekana. Mi nnao friends wa kike kibao na hata sina wazo
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hiyo kitu ngumu sana mtaishia ku do tu au at least mta kiss halafu mtakumbushana kwamba bana sisi marafiki tusifanye.
   
 13. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  urafiki unaweza kuwepo mradi tu usiwe na ukaribu kwani ukaribu wowote wa jinsia mbili husababisha tafrani ya ngono baadae ...
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Urafiki mzuri bila ukaribu ni urafiki wa aina gani?
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  The Boss hiyo kitu ni ngumu sana hasa inapotokea wote mko single,
  Hata km haitakuwa haraka ila on the way ya urafiki mtajikuta mkizoena,then mnamissiana then kawivu kanaanza,na ikishafikiaga tu kwenye wivu kwisha habari yenu hapo kitakachofata ni kuhalalisha na mapnz yanaendelea,

  Ila ikiwa kila mtu ana mtu wake urafiki wa hivo unawezekana kbs,
  Na watu wanaheshimiana na urafiki uadumu tu vizuri,
   
 16. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,765
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  chatting na simu ila kama kutakuwa na mazoea ya kuonana itajitokeza hali isiyo ya kawaida
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba matatizo mengi ya watu yanatokea kwenye mapenzi, unakosana na gf/bf au husband /wife na kama wka bahati mbaya una rafiki wa jinsia tofauti ndio anakuwa kimbilio lako.

  Na ogopa sana mtu ambaye yupo kwenye maumivu ya mapenzi anapofarijiwa, awe mwanamke au mwanaume yani ikitokea akaamini kabisa kwamba rafiki yake ndio kimbilio na wa jinsia tofauti hapo lazima wataishia kwenye mambo mengine.

  Kuna mchekeshaji mmoja wa kimarekani anaitwa anaitwa Chriss Rock anasema kila mtu anamjua mtu ambaye atakuja ku "do" na mpenzi wake na inawezekana ushakutana nae huyu jamaa/dada mshapeana mikono au ameshakuja kwako amekunywa juice yako, pilau lako ,wine yako n.k
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  KUchati na simu ndio mbaya zaidi, sababu watu hawaonani watu wakiongea face to face afadhali sababu uso umeumbwa na haya
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo wewe ukiwa na mazoea ya kuonana na mwanamke/mwanaume yeyote yule bila kujali alivyo lazima ijitokeze 'hali isiyo ya kawaida'?
   
 20. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,957
  Likes Received: 20,288
  Trophy Points: 280
  TB, hii inawezekana japokuwa kuna ugumu wake, hutokea masuala ya wivu yanakuwepo tena sana, sio ajabu 'just friend kuwa wapenzi'.

  Iliwahi kutokea 'just friends' kuoneana wivu na mwisho wa siku walikuja kuwa wapenzi na wanaendelea vizuri.
   
Loading...