Ahmed Omar_
Senior Member
- Jul 17, 2012
- 128
- 195
Hawa watu inabidi tuwacheke tu. Wako usingizini. Wanadhani bado propaganda na fitna za kijinga na kipumbavu kama hizi zitaisaidia CCM. La ajabu ni kwamba juzi tu wamemkaribisha kwa heshima zote Rais wa Ujerumani (nchi iliyokuwa ikiitawala Tanganyika) na katika fakhari kubwa za Marais wote walotawala Tanganyika kuanzia Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa hadi Jakaya Kikwete basi ni kutembelea Uingereza (nchi nyengine iloitawala Tanganyika) na kupiga picha na Malkia na Waziri Mkuu wake.
Tanzania mpaka leo huwa inatoa matoleo mbali mbali ya stempu za kumuadhimisha Malkia wa Uingereza. Yote hayo ni sawa kwao. Lakini inapokuja Zanzibar basi ni kosa kubwa kuwa na mahusiano na Oman au Nchi za Kiarabu. La ajabu tena ni kwamba miaka miwili hii imeshuhudia Jakaya Kikwete, Mizengo Pinda, Anna Makinda, William Lukuvi na Bernard Membe wote wakipanga foleni kuzuru Oman lakini wakifanya viongozi wa Zanzibar linakuwa kosa.
Alhamdulillah, la kufurahisha ni kwamba Wazanzibari na khasa Vijana wa kizazi kipya wamekwisha kuzifahamu na kuzibaini mbinu hizi chafu na ovu. Wote wimbo wao sasa ni mmoja tu: "Tunataka nchi yetu, sasa tumechoka". Akina Samuel Sitta na wenziwe wasubiri kushuhudia MAAMUZI Oktoba Inshallah.
Msikilize Samuael Sitta akimuunga mkono Lukuvi na upate zaidi mjadala huu kutokea facebook:
https://www.facebook.com/ismail.jussa?fref=nf