Mchuja Nafaka G
JF-Expert Member
- Oct 1, 2014
- 763
- 253
Nimepata VIDEO ikimuonesha Samwel Sitta akidai walikataa URAIA WA NCHI mbili kwa sababu kwa upande wa Zanzibari kuna hatari waarabu matajiri kutoka Oman wakarejea na kuchukua Zanzibari. Ndio maana badala yake uraia kwa wananchi wazawa walioenda nje ya nchi utakuwa na hadhi fulani na utatungiwa sheria. Kwa jinsi nilivyoona wataruhusiwa kushiriki kila jambo isipokuwa KUPIGA KURA au KUCHAGULIWA.
Huyu Jussa kama anadhani ni kosa kwa Watanzania kuongea au kushirikiana na nchi ambazo zilikuwa ni koloni la Tanganyika basi hata yeye angekataa kwenda kusoma Uingereza kwenye elimu ya wakoloni.
Kwa hiyo kwa vile Tanzania inashirikiana na nchi zilizokuwa koloni la Tanganyika basi na Zanzibar nayo anataka ishirikiane na nchi zilizokuwa koloni lake. This is absurd to say the least!
By the way, hizi hoja zake zimeishajibiwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ambayo wananchi wako mbioni kwenda kuipigia kura.