Jussa: Hakuna "kupatana" na Watanganyika

LET THEM GO TO hELL ILA DHAMBI YA UBAGUZI HAITAWAACHA SALAMA
 
Kubeli zinamsumbua huyu muajemi, Wazanzibar wanafursa ya kutoa maoni yao juu ya muungano na katiba.Kama yeye hapendezwi na maoni ya wengi arudi Irani.
 
Kwenye facebook wall yake ametupia kitu hiki:
"Wakati tunaelekea India wiki iliyopita tukiwa Uwanja wa Ndege wa Dubai wakati tunabadilisha ndege, tulikutana na mmoja wa Makamishna wa Tume ya Katiba kutoka upande wa Tanganyika ambaye ni msomi wa hali ya juu.....

My take
Naanza kuona kwamba Tanganyika inafaidika na huu muungano kuliko zanzibar.Kama isingekuwa inafaidika,basi wangejitokeza hadharani wanaharakati (kutoka Tanganyika wanaotambuliwa na serikali) kufanya harakati kama hizo za akina Jussa na Maalim Seif kuhusu Tanganyika huru.

Hivi akina Lipumba na Mtatiro huwa wanasemaje kuhusu hili au ni MABUBU mbele ya akina Jussa na Maalim?

Mkuu: Si kawaida yangu kutumia lugha ya jazba lakini kwa leo nitasema hapo "MY TAKE" unazungumza **** na NONSENSE. Mimi ni Mtanganyika na sijaenda Zanzibar au Pemba kwa miaka mingi ingawa hutembelea sehemu nyingine za dunia na sijaona umuhimu wa kufanya hivyo na wala sijui ni nini ninachoweza kufaidika nacho kutoka huko visiwani. Na tuko wengi sana kwa mamillioni wa namna hiyo.

Sasa unaposema eti unahisi Tanganyika inafaidika na huu muungano sijui unazungumzia Tanganyika ipi. Jitoeni haraka lakini msitegemee kampeni kutoka kwa wa Tanganyika katika kufanikisha malengo yenu.
 
Huyu hayuko serious.. tumempa njia zote za kuirejeshea Zanzibar "mamlaka kamili" lakini hataki.
Mkuu, Jusa hana tofauti na WZNZ wengine. Ukisoma maoni ya akina Baru baru na Nonda inaonekana kuwa tatizo la ZNZ siyo mamlaka kamili bali uwepo wa Tanganyika.
Hili linafanyika makusudi kwa hofu kuwa kuvunja muungano Tanganyika itakuwepo lakini hakutakuwepo na mahali pa kujibanza kama wanavyotaka wao.

Mzee Nasor Moyo amesema BLW lililokasimiwa madaraka na Baraza la Mapinduzi ndiyo wenye dhamana ya kuiokoa Zanzibar kutoka katika'ukoloni'. Jambo la kushangaza mzee wa watu ameshambuliwa hata kuitwa Kibaraka, juha asiye na elimu, na wengine wamekwenda mbali na kusema hajawa waziri kiongozi au Rais kwahiyo uelewa wake ni mdogo sana.

Hao wanaomkashifu mzee Moyo ndio hao hao wanaomshangilia Jusa ambaye hajawahi kuwa hata waziri au katibu mkuu.
WZNZ waelewe kuwa tatizo lao si uwepo wa Tanganyika ni wao kutaka kuvunja muungano.
JF imetoa options nyingi sana za kufanya hivyo lakini hakuna hata mmoja anyethubutu kuzitumia.

Jusa anayeongea akiwa India hakuwahi kuongea ndani ya Bunge au BLW ambako yeye ni mwakilishi.
Hajajaribu kuwasilisha hata nusu karatasi ya mswada wa kutaka ZNZ yenye mamlaka na kuvunja muungano.

Mwenzetu baru baru anasema kisheria ZNZ haiwezi kuvunja muungano. Hoja hii inachekesha sana kwasabababu kisheria ZNZ ilishavunja muungano. Kuridhia kuanzishwa kwa serikali ya kitaifa bila kushirikisha upande wa bunge na kukiuka katiba ya JMT inatosha kuwa mfano kwa mwenye weledi.

Kichekesho zaidi ni pale ZNZ inapofanya mambo yake yenye masilahi bila kuingiliwa lakini inapofika ukweli wa kuvunja muungano kila mmoja anarudi nyuma. Ni wakti huo ndipo tunasikia vituko kama vya EU, Senegambia na Uswiss.

Sijui kwanini ZNZ hawakubali kuwa wanaihitaji Tanganyika kuliko wanavyohitajika, vinginevyo kwa dharau, uchoyo na kiburi cha wenzetu wangeshaondoka siku nyingi.

Mafuta yaliposemwa yapo hoja ya kuvunja muungano ilikuja kwa kasi sana, hatukusikia mkataba au serikali 3.
Tukasikia hata kama mafuta ni kijiko kimoja muungano uvunjwe.
Leo jeuri imekwisha na WZNZ wanAtaka mkataba na nchi ya Nyerere wasIyetaka hata kumsikia.
Ukipenda boga penda na maua yake.
 
Mimi naona wangepatikana watu 20 tu waTanganyika wenye uthubutu kama wa Tindu Lissu Kwenye Bunge la Muungano basi mambo yangekuwa sawia kabisa.

Hebu pitieni kwenye ansard za Bunge muone maneno yake haya.

``Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara.

Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara.".....

kidogo sense imekurudia.Naona unamkubalia uliyemiwta kuwa si wakili mwenye uzito.
 
Mkuu, Jusa hana tofauti na WZNZ wengine. Ukisoma maoni ya akina Baru baru na Nonda inaonekana kuwa tatizo la ZNZ siyo mamlaka kamili bali uwepo wa Tanganyika.
Hili linafanyika makusudi kwa hofu kuwa kuvunja muungano Tanganyika itakuwepo lakini hakutakuwepo na mahali pa kujibanza kama wanavyotaka wao.

Mzee Nasor Moyo amesema BLW lililokasimiwa madaraka na Baraza la Mapinduzi ndiyo wenye dhamana ya kuiokoa Zanzibar kutoka katika'ukoloni'. Jambo la kushangaza mzee wa watu ameshambuliwa hata kuitwa Kibaraka, juha asiye na elimu, na wengine wamekwenda mbali na kusema hajawa waziri kiongozi au Rais kwahiyo uelewa wake ni mdogo sana.

Hao wanaomkashifu mzee Moyo ndio hao hao wanaomshangilia Jusa ambaye hajawahi kuwa hata waziri au katibu mkuu.
WZNZ waelewe kuwa tatizo lao si uwepo wa Tanganyika ni wao kutaka kuvunja muungano.
JF imetoa options nyingi sana za kufanya hivyo lakini hakuna hata mmoja anyethubutu kuzitumia.

Jusa anayeongea akiwa India hakuwahi kuongea ndani ya Bunge au BLW ambako yeye ni mwakilishi.
Hajajaribu kuwasilisha hata nusu karatasi ya mswada wa kutaka ZNZ yenye mamlaka na kuvunja muungano.

Mwenzetu baru baru anasema kisheria ZNZ haiwezi kuvunja muungano. Hoja hii inachekesha sana kwasabababu kisheria ZNZ ilishavunja muungano. Kuridhia kuanzishwa kwa serikali ya kitaifa bila kushirikisha upande wa bunge na kukiuka katiba ya JMT inatosha kuwa mfano kwa mwenye weledi.

Kichekesho zaidi ni pale ZNZ inapofanya mambo yake yenye masilahi bila kuingiliwa lakini inapofika ukweli wa kuvunja muungano kila mmoja anarudi nyuma. Ni wakti huo ndipo tunasikia vituko kama vya EU, Senegambia na Uswiss.

Sijui kwanini ZNZ hawakubali kuwa wanaihitaji Tanganyika kuliko wanavyohitajika, vinginevyo kwa dharau, uchoyo na kiburi cha wenzetu wangeshaondoka siku nyingi.

Mafuta yaliposemwa yapo hoja ya kuvunja muungano ilikuja kwa kasi sana, hatukusikia mkataba au serikali 3.
Tukasikia hata kama mafuta ni kijiko kimoja muungano uvunjwe.
Leo jeuri imekwisha na WZNZ wanAtaka mkataba na nchi ya Nyerere wasIyetaka hata kumsikia.
Ukipenda boga penda na maua yake.

Nguruvi3.

Naona umenikimbia kwenye uzi wetu ule BARAZA YA AHMED RAJAB na unajaribu kurejea hapa.

OK . kama nilivyobainisha kwako SIKU ZOTE USISIMAMIE KUWA MOYO kasemaaje, NYERERE kasemaje au KARUME kasemaje. Kinachotakiwa kwako kama Great Thinker ni kujenga hoja za kitaalamu kuhalalisha maneno yako.

Na siku zote usipende kuupotosha umma wa wasomaji kwa kutumia majina ya watu wengine. KUMBUKA mimi niliposema kuwa BLW halina mamlaka hata kidogo kuzungumzia Muungano sikutoa angani au kinywani mwangu hayo maneno bali nilifafanua kwa kina sana kutumia sharia zenu na historia ya muungano wenu na nilifikia mpaka kusema

MUUNGANO WENU NI KHARAMU. na nikaendelea zaidi kusema Muungano uliridhiwa bara tuu na sio Zanzibar!.

USHAHIDI na ufafanuzi wa kauli zangu huu hapa.
Sio lazima kila mkataba uwe ni wa maandishi, lakini mkataba wowote wa ardhi, land au pango, lazima uwe wa maandishi!. Wewe unaweza kununua gari na kumzawadia mpenzi/mke/ ndugu au mzazi kwa kauli tuu na ukawa ni mkataba halali!.

Lakini kama una land yako, ukiamua kumzawadia yoyote, hata ukimzawadia kwa kauli, lazima maandishi yafuatie ndio yatakayo halalisha hiyo kauli!.

Mzizi asili haswa wa muungano ni kauli, ya Nyerere na Karume.

Nyerere " Sisi ni ndugu, kwa nini tusiungane?".
Karume " Tuungane, wewe rais. mimi makamo".

Shughuli ilianza na kumalizika in a split of a second!.

Kwa vile hizi ni nchi mbili tofauti zenye uhuru wake na zote ni Jamuhuri huru, kauli pekee haitoshi kuziunganisha, lazima kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kuhalalisha nia na kauli hizo, ndipo zikaandaliwa hizo articles of union!.

Articles zile japo zilikosa sifa ya kisheria ya kuutwa mkataba "contract" kutokana na tatizo la kisheria liitwalo "privity of contract", articles zile zilikuwa na sifa zote za kuitwa ' international treaty" kuunganisha nchi mbili, na ili any international treaty kupata uhalali na nguvu ya kisheria, ni lazima treaty hiyo iwe ratified na mabunge ya nchi husika!.

Ratification is a process ambayo hufanywa kwa procedures maalum na kufanywa in writing!.

Bunge la Tanzania lilifuata sheria, taratibu na kanuni zote ku ratify zile articles of union kwa maandishi!.

Zanzibar, walikuwa ndio kwanza wametoka kwenye mapinduzi, hivyo hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa kila kitu!. Lilipaswa kuziridhia zile articles of union kwa ratification ambayo hufanywa kwa maandishi!. Vikao vyote vya BLM vina hansard, lakini hilo halikufanyika na hakuna kumbukumbu yoyote ya maandishi kwamba ratification ilifanyika!.

Kisheria Muungano ni wa bara tuu, ndio maana Dourado alipomtonya Jumbe kuhusu Zanzibar kutouratify muungano na wakataka kuweka mambo sawa, Jumbe alishughulikiwa ipasavyo!.

Yani natamani huyo jussa, cuf na hao uamsho siku uwekwe mdahalo ambapo tundu lissu, nguruvi3 na mzee mwanakijiji wamchachafye hadi aisome namba

Nafikiri umfahamu Jussa wewe. naamini kabisa Jussa na Tundu Lissu kwa kuwa wote ni wanasharia mahiri watazungumza lugha moja kama wanavyozungumza hadharani au wakiwa Bungeni. Lakin hao wengine sioni kama wana jipya. FUATILIA UZI wa BARAZANI KWA AHMED RAJAB uone wanavyogaragazwa kwa hoja za kitaalamu sio porojo.

Huyu hayuko serious.. tumempa njia zote za kuirejeshea Zanzibar "mamlaka kamili" lakini hataki.

Naomba uziweke hapa ili tuzijadili kwa kina.

Kwani kwa upande wangu kwa kuwa Muungano ni kitu cha kisharia zaidi sio KISIASA ,nikiichambua Katiba ya TZ au ile ya Znz sijaona kitu na ukiziangalia sharia za Kimataifa ndio hakuna kabisa njia ya BLW kuweza kuzungumzia Muungano wenu. Nakuomba pitia uchambuzi wa kisharia niliomjibu ahali yetu Nguruvi3 hapo juu.

Tunakuomba kwa ihsani yako utubainishie.

Nawaunga mkono wazanzibari katika kila hatua,tuwaachie nchi yao wajiamulie mambo yao muungano sio lazima iwe hiari yao
 
Mimi naona wangepatikana watu 20 tu waTanganyika wenye uthubutu kama wa Tindu Lissu Kwenye Bunge la Muungano basi mambo yangekuwa sawia kabisa.

Hebu pitieni kwenye ansard za Bunge muone maneno yake haya.

``Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Rasimu ya Muswada hayakubaliki kwa sababu yanaweka mchakato wa Katiba Mpya kwenye huruma na/au fadhila ya Rais wa Zanzibar na siasa za Zanzibar kwa ujumla. Kwa mapendekezo haya, Rais wa Zanzibar asipokubaliana na jambo lolote linalohitaji ridhaa yake basi mchakato mzima utasimama au kusitishwa. Aidha, endapo katika kura ya maoni inayopendekezwa, theluthi mbili ya Wazanzibari hawatakubaliana na Katiba Mpya basi Katiba hiyo haitapitishwa hata kama inakubaliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa Tanzania Bara.

Mustakbala wa taifa letu hauwezi kuwekwa tena rehani kwenye siasa za Zanzibar na kwenye matakwa ya Wazanzibari kwa kiasi hicho. Kuhusiana na jambo hili, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar ahusishwe tu katika masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Nje ya masuala hayo, Rais wa Zanzibar hana sababu yoyote ya kuhusishwa na mchakato wa kikatiba unaohusu mambo ya Tanzania Bara."

Aidha, wajumbe wa Tume ya Mapitio ya Katiba ambao watatoka Zanzibar wahusike tu katika mchakato wa masuala ya kikatiba ambayo ni ya Muungano tu. Vile vile, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wananchi wa Zanzibar washiriki katika kura ya maoni inayohusu mfumo mpya wa Muungano tu. Hii ndio kusema kwamba, kama vile ambavyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Tanzania Bara hawajashirikishwa katika mchakato wa kikatiba wa Zanzibar kwa sababu ulihusu mambo yasiyokuwa ya Muungano, vivyo hivyo viongozi, wawakilishi na wananchi wa Zanzibar wasishiriki katika mchakato wa kikatiba wa mambo yasiyokuwa ya kikatiba kwa upande wa Tanzania Bara.``

Barubaru Wazanzibar ni Wanafiki. Tundu Lissu alipotoa hiyo hoja aliitwa kila aina ya Tusi na Wazanzibar. Wazanzibar ni POPO ( Si Ndege si Mnyama)

Kama wanataka kujitoa si wapeleke Muswada kwenye Balaza la Wawakilishi (BLW). Yaani kupeleka Muswada kwenye Baraza la Wawakilishi kunahitajika Tundu lisu?
 
Jussa apeleke Muswada wa Kujitoa Zanzibar katika Muungano na si kupiga Porojo.
 
..............Katika majibu ya kustaajabisha wakati nilipomuuliza vipi hali ya utoaji maoni inaendelea, alitujibu kuwa inaendelea vizuri na pamoja na kwamba upande mmoja (nna hakika alikusudia Zanzibar) unatoa madai makubwa, yeye haimpi tabu kwa sababu anajua wanaofanya hivyo wanajipa nafasi kubwa ya kuja kupatana (alitumia neno la Kiingereza 'bargaining') ili kupata muafaka wa kati na kati.

Bahati mbaya mawazo kama haya ya Kamishna huyu ndiyo mawazo mgando ya watunga sera na sheria wengi wa Tanganyika wanaojiona kama ni watawala au wamiliki wa Zanzibar na hivyo kujipa matumaini kuwa...............

Kwa maelezo ya Jussa aliyoyatoa kama ulivyomnukuu, inaonekana huyu jamaa ana vitu vyake kichwani kuhusu muungano. Nashangaa kwa nini hakuchukua hatua ya kumuuliza zaidi huyo kamashna kuwa kwa kusema "upande mmoja" alikuwa anamaanisha nini. Maana naona mtanzania huyu Jussa anaweza akawaanamlisha maneno kamishna. Kuna uwezekano kamishna kwa kusema upande mmoja alimaanisha CUF dhidi ya CCM au CHADEMA dhidi ya DP, au hata wazee dhidi ya vijana n.k.

Kwa nini mtanzania huyu arukie suala la kusema Zanzibar ndiyo aliyoizungumzia kamishna? Vinginevyo maelezo yake hayajitoshelezi.
Lakini pamoja na hayo, Mtanzania Jussa aelewe suala la katiba sio suala la Uzanzibari na Uzanzibara au Utanganyika na Uzanzibari.

Suala la katiba mpya ni suala la watanzania wote katika kutafuta mstakabali wa nchi yetu wote bila kujali unatoka sehemu gani ya nchi ya Tanzania. Najua suala muungano ni muhimu katika katiba tunayotaka ilikufikia Tanzania tunayoitaka. Umuhimu huu usifanye baadhi ya watanzania kuona kile wanachokiwaza ndicho sahihi tu juu ya muungano.

Mtanzania Jussa
hasitake kulazimisha hoja ya kugawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vipande vipande kama njia sahihi ya kuwa na Tanzania tunaoitaka, atuache watanzania wote tuamue kwa pamoja kipi kinafaa kwa kulinganisha hoja, yenye manufaa kwa watanzania wote, iliyoko kwenye kila maoni ya mtanzania.
 
Barubaru Wazanzibar ni Wanafiki. Tundu Lissu alipotoa hiyo hoja aliitwa kila aina ya Tusi na Wazanzibar. Wazanzibar ni POPO ( Si Ndege si Mnyama)

Kama wanataka kujitoa si wapeleke Muswada kwenye Balaza la Wawakilishi (BLW). Yaani kupeleka Muswada kwenye Baraza la Wawakilishi kunahitajika Tundu lisu?

Kwa mujibu wa Sharia zenu ambazo zimebainishwa katika Katiba zote mbili Ya Muungano na ile ya Znz. BLW halina mamlaka kujadili mambo ya Muungano.
PITIA uchambuzi niliobainisha pale nilipomjibu Nguruvi3 hapo juu utaliona hilo.

Lakin kwa kukusaidia ni Lazima ile Sharia ya Muungano lazima iridhiwe na BLW kwanza kisha watakuwa huru kuweza kuujadili muungano. Kwani Muungano wenu umeridhiwa Bara tu na sio Znz.

kama zanzibar ikiwa nchi hata sie wakerewe tutadai ukerewe iwe nchi....kwani nacho ni kisiwa tena kina watu wengi kuliko zanzibar...KAZI NI KWENU TANGANYIKA NA ZANZIBAR...NA SIE UKEREWE TUPO TUNAWAANGALIENI.
 
Kwa mujibu wa Sharia zenu ambazo zimebainishwa katika Katiba zote mbili Ya Muungano na ile ya Znz. BLW halina mamlaka kujadili mambo ya Muungano.
PITIA uchambuzi niliobainisha pale nilipomjibu Nguruvi3 hapo juu utaliona hilo.

Lakin kwa kukusaidia ni Lazima ile Sharia ya Muungano lazima iridhiwe na BLW kwanza kisha watakuwa huru kuweza kuujadili muungano. Kwani Muungano wenu umeridhiwa Bara tu na sio Znz.

Je BLW linaweza kujitungia Sheria ambazo zinakinzana na Katiba ya Muungano?
 
Muungano ni maslahi ya viongozi wa CCM wa Tanganyika wala hakuna lingine.
Hawa mawaziri, makati makatibu wakuu na wakurungezi mbalimbali wa kutoka zenj waliopo kwenye muungano huwa hawazungumzi lolote mpaka muda wao wa utumishi utakapoisha, mfao mzuri ni H.N. Moyo
 
Jussa apeleke Muswada wa Kujitoa Zanzibar katika Muungano na si kupiga Porojo.

Harakati za kudai haki zao Znz katika Muungano sio zinaanzishwa na Jussa , Bali zilianza toka eanzi za Jumbe kwa Muasisi wa Muungano huo St Nyerere.

hebu ngoja nikudadavulie kidogo kuhusu harakati hizo.

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.

Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.

Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali “patakatifu” bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.

Naielewa vizuri hali ya mtafaruku iliyofuatia hatua hii na kule kutangazwa “kuchafuka” kwa hali ya kisiasa Visiwani. Lakini pamoja na kurejea kwa hali ya kawaida, bado matatizo ya Muungano yaliendelea kutawala agenda za vikao vingi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Lakin mpaka tunapo andika leo wengi hawajui.
1. Kwanini Nyerere alikataa kuundwa kwa Serikali ya tanganyika kulikodaiwa na Znz na vile vile bunge la Muungano G57?
2. Tanganyika ambayyo imejivika jina la Tanzania, haijaweza kutoa msimamo wake kuhusu kadhia hii.

Sijui wewe unaweza kutujibu masuala hayo mawili hapo juu.

Je BLW linaweza kujitungia Sheria ambazo zinakinzana na Katiba ya Muungano?

Albeto,
kama umenisoma vizuri katika bandiko langu namba 47 la kuchangia mada hii, nimefafanua kwa kina sana.

Lakin kwa kupitia mabadiliko makubwa ya katiba ya Znz yaliyofanywa hivi karibuni sioni kama kuna sehemu wamevunja sharia au katiba ya muungano wenu.

Lakin kwa kukusaidia zaidi ukiwa kama Mtanzania halisi mwenye uchungu wa nchi yako. Tumia kipengele hichi cha Sharia zenu kufungua mashitaka mahakamani ( kama walivyotumia watu wa Arusha katika kesi ya kupinga matokeo ya Arusha mjini (Mbunge LEMA). Kumbuka aliyepinga sio Batilda Buriani bali ni waTz, wakaazi wa jimbo la Arusha town.
sharia na 15 ibara ya 6 ya mwaka 1784 ya katiba ya Muungano . kifungu cha 26 kinabainisha wazi kuwa '' kila mtu ana haki kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sharia, kuchukua hatua za kisharia kuhakikisha hifadhi ya katiba na sharia za nchi''

Una haki kabisa wewe na wana JF wenzako kama yamewagusa mabadiliko hayo ya katiba ya Znz na mnaona yamevunja sharia za muungano basi mahakama zipo wazi. Na kifungu mtakachokitumia nimeshawapa. NENDENI

Back
Top Bottom