Jussa ajiuzulu Unaibu Katibu Mkuu (ZNZ) ili 'kusaidia Zanzibar kupata Uhuru Wake'

Chama chochote cha siasa hakiwezi kumtegemea mtu mmoja, hivyo mwanachama yoyote ana uhuru wa kufanya uamuzi wowote anaotaka hata ikibidi kuondoka kwenye chama. Chama ni muhimu kuliko mtu binafsi. Hongera Jussa kwa ukomavu wako wa kisiasa.
 
..Jussa amelenga mbali.

..huko tunakoelekea, kwenye "muungano wa mkataba",inawezekana usajili wa vyama vya siasa usiwe suala la muungano.

..kwa msingi huo CUF na CCM itabidi vijisajili upya katika pande mbili za muungano.

..swali ni, je, vyama hivyo vitaendelea kuwa, CCM, na CUF, kwa upande wa ZNZ, au vitarudi kwenye asili yake ya ASP na HIZBU??

..zaidi, huku Tanganyika CCM itaendelea na jina hilo au itarudi na kuwa TANU???
 
Amewajibika baada ya kuhoji matumizi ya mabosi zake kuja honeymoon arusha huku walinzi wakiwa na wanachama wa Buguruni.
 
wacheni maneno nyie..hakuna kitu kama hicho..nyie mtaendelea kua mkoa kama mikoa mingine ya tanzania...
hakuna mkoa wenye Rais wake, bendera yake, baraza na bunge lake Zanzibar ni nchi kamili ni Wanyonyaji wakuu kumbuka wao wanahudumiwa na serikali mbili tofauti bali sisi tunayo moja tu nayo ya ... na mzigo mkubwa kuiendesha
 
[h=1][/h]
ismail-jussa-ladu-350x272.jpg

Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe.

“Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar , uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

“Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

“Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

“Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

“Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

“Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

“Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.”

HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
Zanzibar

My Take. Jee siasa zake za udini zimemponza, kumbuka tamko lake alilolitoa baada ya uchaguzi wa Uzini.
Karibuni kwenye mjadala.
05 Oktoba, 2012
 
Mkimaliza kutengana na Tanganyika, mtaanza kuulizana hivi wewe Jusa ni wa wapi? Mtagundua ni Mhindi flani then mtamtimua kama mbwa. Halafu mtamuuliza nawe Karume ni wa wapi? Mtagundua ana asili ya Kigoma Ujiji, mtataka naye akupisheni. Mwisho wa yote mtajikuta wote hamna asili ya Unguja wala Pemba, kumbe wengine asili yao ni Komoro, Tumbatu, Ngazija, Moroni, Mayote, Mafia, na Tanga (Tanganyika). Fanyeni fasta mtupishe, nasi Watanganyika tutawataka wanaojiita wazenji walioko huku wachague moja kati ya kurudi Zenji au kuchukua uraia wa huku.
hizi ni chuki za kipumbavu na ujinga wa watanganyika
tanganyika kesi za ngombe tu watu munauwana muna makabila zaid ya miia kuna uisilamu na ukristo sensa tu balaa
bakwata kunafukuta mfumo kristo waisilamu wameushitukia
sasa soma hostoria nya zanzibar ubaguzi unafanya na ccm kupitia kachorora na kisonge lakini wazanzibar wako kitu kimoja
daa siasa za chadema hizoooo mwangosi kumwaga machangooo
 
hizi ni chuki za kipumbavu na ujinga wa watanganyika
tanganyika kesi za ngombe tu watu munauwana muna makabila zaid ya miia kuna uisilamu na ukristo sensa tu balaa
bakwata kunafukuta mfumo kristo waisilamu wameushitukia
sasa soma hostoria nya zanzibar ubaguzi unafanya na ccm kupitia kachorora na kisonge lakini wazanzibar wako kitu kimoja
daa siasa za chadema hizoooo mwangosi kumwaga machangooo
 
Naipenda sana hiyo bendera ya Tanganyika.Nchi ya Zanzibar ni yetu sisi Watanganyika ila baadhi ya watu aina ya Jusa si wetu hao wana kwao ndiyo maana wanajaribu kuleta uamsho ndani ya nchi hii takatifu ya Tanganyika(Zanzibar inclusive)
Swala la kutengana na haliko wakitaka watuachie nchi yetu Zanzibar na wao waende kwao oman na Pakstani au Afganistani watu wabaya sana hawa.
icon8.png
icon13.png
icon4.png
Kaaaaaaaaaaaaaaama Boko - Halal vile au Al-Shadaaaaad!
 
Back
Top Bottom