Jussa ajiuzulu Unaibu Katibu Mkuu (ZNZ) ili 'kusaidia Zanzibar kupata Uhuru Wake'

Sababu alizoziandika ni za msingi sana, kwani atapata wakati wa kuwatumikia wananchi wake kwa uwezo mkubwa zaidi.

Hizi ni habari mbaya kwa wale wanaoutaka muungano fake. Safai hii analivalia njugu suala la muungano kisheria mpaka uundwe muungano unaofahamika na kukubalika na pande zote mbili. Sisi watanzania bara ni wanafiki, kwa sababu hata sisi hatuupendi huu muungano ulivyo lakini tunasemea pembeni tu. Ni muhimu kuwa muwazi na kutumia vyombo vya kisheria kusema manunguniko yetu.

Kwa wale viongozi wanafiki wa Zanzibar wanaocheza kote kote, kwao itakuwa brake. Kwa sababu kwa mpango huu wa Jusa, kila mmoja atalazimika kuonyesha yuko wapi awe CCM au CUF. Manunguniko ya suala la Muungano si suala la UAMSHO, bali ni suala la Wazanzibar wote, hivyo wote wale wanaojificha nyuma wakiutanguliza UAMSHO mbele kama hawana pa kuisemea watapata pa kusemea. Hii ni kutokana na kuanzishwa chombo maalum kitachoshughulikia suala la Muungano wa mkataba.

Hayo ni machache tu, bali yapo mengi atayoyashughulikia. Hii ni habari njema.
 
Iweje ruzuku ya zanzibar iendeshe shughuli za chama bara kulikozo zanzibar,
Kafuata nyao za A.Rashid.
Sasa ukweli unaonekana kuwa chama kimepoteza dira bila kujitoa mwanga CUF yafaaaaaa
 
Jussa kaza buti uikomboe nchi yenu kutoka kwenye huu muungano 'fake'

Go Jussa go!
 
hii inanikumbusha enzi za mrema!! ilibaki kidogo sana tumpe urais!! mwisho wa siku tunashukuru mungu hatumpa nchi!!
Leo hii twapata mwingine mwenye hulka za mrema huyu anatumia njia za simba kuwagawa nyati ili awararue!!
Kazi kwenu wazenji!!
JE, MTAKUBALI MPANGO WAKE WA KUWAPELEKA UARABUNI KWA SULTANI AU MTAMKATAA?
 
Hivi kudai z'bar huru ni uamsho hizo ni chuki zenu watanganyika dhidi ya z'bar mara mkivunja muungano unguja na pemba zitatengana yaani hamwishi propaganda za baba yenu nyerere kama kudai z'bar huru ni uamsho na iwe hivyo hadi kieleweke hongera jusa
 
Kwa mbaaaaaaaaaaaali,naiona Tanganyika Yetu,isiyokuwa na Matatizo ya Uamsho nk,Hongera nenda kadai pemba yenu wawape hao wazanzibara!

Naipenda sana hiyo bendera ya Tanganyika.Nchi ya Zanzibar ni yetu sisi Watanganyika ila baadhi ya watu aina ya Jusa si wetu hao wana kwao ndiyo maana wanajaribu kuleta uamsho ndani ya nchi hii takatifu ya Tanganyika(Zanzibar inclusive)
Swala la kutengana na haliko wakitaka watuachie nchi yetu Zanzibar na wao waende kwao oman na Pakstani au Afganistani watu wabaya sana hawa.
icon8.png
icon13.png
icon4.png
 
Nitauliza maswali mawili tu
1. Zanzibar inaongeza uchumi gani kwa Tanganyika?
2. Tanganyika inaongeza thamani gani kwa Zanzibar?

Nafikiri Tanganyika ina add values ikiwepo peace and stability Zanzibar

Ukweli huu Muungano uishe. Hawa wenzetu waliokunywa sumu ya waarabu wanaopenda kugawanyika hadi familia waondoke na hizo tabia zao wakagawanyike huko. Watagawanyika mpaka wengine watakaa juu ya miti kama makazi. To hell Zanzibar.
 
Huyu jamaa mnafiki sana, namjua..... Vuteni subira atajitanabaisha tu kwa unafiki wake!
Kwa kiasi fulani anajiandaa kutengeneza mazishi ya CUF!
 
hivi anacheo gani kwenye kile kikundi cha kigaidi kinachochoma makanisa na bar za wabara..

Ni mchumia tumbo,na pia ni Aibu ya Katibu yaani Maalim Madevu cheo ambacho ametakiwa kujiuzulu.hali si shwari ndani ya KAFU.
 
ha ha ha! kuna watu wengine ni hopeless kabisa,anasema "nataka niibane serikali ndani na nje itekeleze wajibu wake kwa wananchi"
>kwani CUF sio chama mshirika kuongoza serikali huko zanzibar?
> wana makamu wa rais huko,anafanya kazi gani?
>wana mawaziri wanafanya kazi gani?
>Kama mna wanachama ambao wanaongoza serikali ya zanzibar sasa mnataka kupambana na nani? mnapambana na kivuli chenu?
Mkiambiwa mmeolewa hamna maamuzi mnakasirika,ona sasa mnageuzwa mabwege kwa hii NDOA yenu feki.
THIS WAS A POLITICAL SUICIDE,THEREFORE YOU HAVE TO BEAR ITS CONCENQUENCES UNTIL YOU LEARN TO USE YOUR BRAINS.
 
James Bond na Wana JF,
Mimi Binafsi sijamwelewa hapa, namnukuu,

“Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

Muungano wa Mkataba ndio Upi ??
Nawakilisha.


Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe.

“Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar , uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

“Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

“Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

“Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

“Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

“Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

“Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.”

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
Zanzibar
05 Oktoba, 2012
 
hivi anacheo gani kwenye kile kikundi cha kigaidi kinachochoma makanisa na bar za wabara..

Yeye ndiye muasisi wa uamsho na mhamashaji wa kuyachoma makanisa na kuharibu mali za "wazanzibara" Na sasa anakwenda "Kufanya kweli" yaani kuhakikisha wasio na asili ya Zanzibar wote kuwafanyia vituko hadi waondoke; na baada ya hapo na yeye pia kutimuliwa kama mbwa maana si mzanzibari yule; ni mu Irani!
 
Back
Top Bottom