Jussa ajiuzulu Unaibu Katibu Mkuu (ZNZ) ili 'kusaidia Zanzibar kupata Uhuru Wake' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jussa ajiuzulu Unaibu Katibu Mkuu (ZNZ) ili 'kusaidia Zanzibar kupata Uhuru Wake'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jamesbond007, Oct 5, 2012.

 1. jamesbond007

  jamesbond007 Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Ismail Jussa, muda mchache uliopita, ikielezea azma yake ya kujiuzulu nafasi hiyo. Hata hivyo, Jussa anabakia na nafasi zake nyengine kwenye Chama, ikiwemo ya ujumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, na pia nafasi yake ya kuchaguliwa na wananchi ya kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jimbo la Mji Mkongwe.

  “Leo asubuhi nimewasilisha kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba barua ya kuomba kujiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar , uamuzi ambao nimeomba uanze kutekelezwa rasmi tarehe 10 Oktoba, 2012.

  “Nimechukua uamuzi huu baada ya kuzungumza na kushauriana na viongozi wangu wa juu wa Chama ambao ni Mwenyekiti, Profesa Lipumba, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Machano Khamis Ali na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad takriban miezi miwili iliyopita. Nawashukuru baada ya kunitaka niwape muda wa kulitafakari walinikubalia lakini wakaniomba nibakie hadi tutakapokamilisha baadhi ya shughuli muhimu za Chama katika kipindi hichi.

  “Sababu kubwa zilizonisukuma kukiomba Chama kiniruhusu niachie nafasi hii ni kutokana na muda mrefu sasa kuhisi kwamba majukumu niliyo nayo ya kuwa msimamizi mkuu wa utendaji wa Chama kwa upande wa Zanzibar na wakati huo huo kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe hakunipi fursa ya kujifaragua na kutumikia nafasi zote mbili kwa ufanisi unaotakiwa. Nataka kuona kazi ya kuibana Serikali ndani na nje ya Baraza ili iwajibike zaidi kwa wananchi inaimarika zaidi.

  “Sambamba na sababu hiyo ni kwamba nimekusudia kutumia muda mwingi zaidi kutoa mchango mkubwa zaidi katika harakati za wananchi wa Zanzibar zinazoendelea za kuhakikisha kuwa Zanzibar inarejesha mamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na kuwepo kwa Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa.

  “Harakati zinazoendelea Zanzibar kwa njia za amani na za kidemokrasia kwa kutumia mchakato wa Katiba Mpya zinahitaji kuungwa mkono na kupewa msukumo wa dhati na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar kwenda kusimamia maslahi yao na ya nchi yao. Nimetafakari na kuona kwamba nikiwa sina majukumu mengine ya kiutendaji nitakuwa na muda kutosha wa kulifanya hili mimi na Wawakilishi wenzangu tunaotoka CUF na CCM, vyama viwili vya siasa vilivyomo Barazani.

  “Nafurahi kwamba leo nimetimiza azma yangu hiyo. Pamoja na uamuzi huu, naendelea kubaki kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

  “Nawahakikishia viongozi na wanachama wenzangu wa CUF kwamba tutaendelea kushirikiana pamoja katika shughuli nyengine zote za kisiasa za Chama na kwa pamoja tutafanya kazi kuyatimiza malengo tuliyojiwekea. Naahidi kumpa ushirikiano kikamilifu mwanachama yeyote atakayeteuliwa kujaza nafasi ninayoiwacha.”

  HAKI SAWA KWA WOTE

  ISMAIL JUSSA
  Zanzibar
  05 Oktoba, 2012
   
 2. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nendeni tu hata sisi tumewachoka
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa balaa,inabidi aangaliwe sana asitupeleke pabaya.
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kutaka Zanj ijitenge, nahisi bado anamambo kadhaa nyuma yake, kuna nchi zipo nyuma yake.
   
 5. m

  malaka JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sasa si angejiuzulu na uwakilishi kabisa?? Kaona unaibu katibu hauna hela hana lolote.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anaweza pia kuwa anatupeleka pema maana ni kweli wengi, hata huku Bara tumeuchoka huu muungano wa manung'uniko
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wacheni maneno nyie..hakuna kitu kama hicho..nyie mtaendelea kua mkoa kama mikoa mingine ya tanzania...
   
 8. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Jiuzuru nafasi zote ikiwamo ya baraza la uwakilishi ili uwe na mda wa kutosha kuikomboa znz.
   
 9. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Mkimaliza kutengana na Tanganyika, mtaanza kuulizana hivi wewe Jusa ni wa wapi? Mtagundua ni Mhindi flani then mtamtimua kama mbwa. Halafu mtamuuliza nawe Karume ni wa wapi? Mtagundua ana asili ya Kigoma Ujiji, mtataka naye akupisheni. Mwisho wa yote mtajikuta wote hamna asili ya Unguja wala Pemba, kumbe wengine asili yao ni Komoro, Tumbatu, Ngazija, Moroni, Mayote, Mafia, na Tanga (Tanganyika). Fanyeni fasta mtupishe, nasi Watanganyika tutawataka wanaojiita wazenji walioko huku wachague moja kati ya kurudi Zenji au kuchukua uraia wa huku.
   
 10. b

  bodachogo Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimegonga Like
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi anacheo gani kwenye kile kikundi cha kigaidi kinachochoma makanisa na bar za wabara..
   
 12. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Idara ya usalama wa taifa inahangaika na akina ulimboka inawaacha akina J ussa wanaharibu nchi hapa.
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Cold war imeisha, kwa nini tunaendelea kuing'ang'ania hii 'nchi' inayoitwa Zanzibar???
   
 14. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Kwa mbaaaaaaaaaaaali,naiona Tanganyika Yetu,isiyokuwa na Matatizo ya Uamsho nk,Hongera nenda kadai pemba yenu wawape hao wazanzibara!
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,795
  Trophy Points: 280
  Kweli ni habari mpasuko!
   
 16. P

  PLAN B Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao tumewachoka nenda zenu
   
 17. T

  Taso JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,649
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Utasemaje "fanyeni fasta mtupishe" halafu hapo hapo unawatisha kwamba wakiwa peke yao wataumia? Wewe ndio unaogopa?

  Watanganyika ndio mnaogopa kuwa peke yenu, Mzanzibar akitangaza uhuru mnasema "ondoka...nenda" kumbe kwa ndani mnatetemeka. Tanganyika ni sawa na mke anaetaka kuachwa, anajifanya kujibu "ondoka ondoka" lakini kiundani anaogopa kuanza maisha mwenyewe, anamtaka mumewe, Zanzibar.

  Jussa will go down in history as a single most valiant voice for Zanzibar's liberty, a champion of the inalienable rights and interests of the Island's people. He has unmatched balls and brains and love of country.

  Wakati anaisaidia Zanzibar ananisaidia na mimi Mtanganyika kukomboka from the hellacious shackles of the botched Muungano.

  Let Tanganyika go!
   
 18. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Huyu anataka Muungano wa Mkataba....wasiwasi ni kwamba sijui kama ana wafuasi...maana ADC inawenyewe tayari, CUF iko kwenye ndoa CDM hawezi tina maguu, labda ajiunge na Mch Mtikila
   
 19. P

  PLAN B Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nenda zenu tumewachoka tanganyika yetu ibaki salama nyie waarabu mnamatatizo
   
 20. M

  MTK JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Mwanauamsho huyo;
   
Loading...